Historia ya Mgambo waliokufa Mbagala

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
11,045
15,379
Zamani kidogo kabla ya mwaka 2010 niliwahi sikia tukio la Mgambo wapatao 5+ (Sina uhakika) Walifariki dunia kwa kula chakula inachosemekana kilikua na sumu.

Hii story niliisikia mara kadhaa mtaani na hivyo sina taarifa kamili.

******Story******
Kama utakumbuka matukio ya miaka ya nyuma ya mama Ntilie kukamatwa na mabwana afya pamoja na mgambo kwa kutozingatia eidha kanuni za afya au matakwa/ maelekezo fulani

Hawa mgambo walikua wakipita mtaani/ kijiweni, Mamalishe walikuwa wanapata taflani kubwa sana. Ikiwa pamoja na kukimbia huku na kule kukwepa mkono wa Dola.

Katika historia naambiwa Mwaka fulano huko mbagala, mgambo kadhaa (5+) walikuwa na tabia ya kwenda kuvamia vilinge vya mama ntilie na kufanya madhira makubwa.

Hali hii ilipelekea mama ntilie mmoja kuchoka na kuamua kupetengeneza tukio lililoua mgambo kadhaa.

Mgambo hao walikuwa na mazoea ya kupokonya vyakula na na kwenda kulia vichakani.

Siku moja mama ntilie huyo alitafuta sumu kali (Sijui ni nyongo ya mamba au) na kuiweka kwenye pilau lake mantashar

Naambiwa mama huyo siku hiyo hakuuza chakula, alikuwa Standby kusubiti Kashkash za mgambo.

Kama kawaida mgambo hao. Walibeba majungu ya Wali na kutokomea nayo kusiko julikana

Baadae mgambo hao wakala msosi wenye sumu na kufa kifo cha kinyama.

Baada ya hapo matukio ya namna hiyo ya Unyanyasaji yalikoma eneo husika.

Je umeshawahi sikia hii hadithi??

Au mnasemaje mods
 
Hao mods unawauliza wao kumbe,

Hebu tuambie huyo mama ntilie aliishia wapi au hao mgambo somba somba yao walijichanganya wakaweka na sumu ya panya
 
Hii ilitokea nakumbuka mwana,humu wengi wameanza kujua mambo soon, washamba
 
Nimesoma sentence ya mwisho nikacheka sana nikijua jamaa ameamua kuwachokoza/kuwatania mods ila nikaja gundua kumbe ni mambo ya signature
 
Huyo mama alikosea ilibidi asiweke sumu ila aweke dawa ya kuharisha weeeeeee siku mbili ili wajifunze
 
Back
Top Bottom