jay-millions
JF-Expert Member
- Apr 30, 2015
- 3,473
- 8,186
Watu aina ya kagame au Gaddafi ni adimu sana yaani anaweza tokea mmoja kwenye karne hivyo Ni wa kumtumia vizuri kwa manufaa ya taifa angalia urusi hawamwachii putin, angalia Ujerumani angalia China nk. Usidhani watu kama PK wanapatikana kirahisi au wapo katika kila generationMkuu gadaffi alikuwa mzalendo zaidi ya kagame ila udikteta wake ma kukandamiza wakosoaji huku akiwanyima uhuru wananchi kulifanya apinduliwe na vijana wa kijiweni tu......
Kagame hata kma kafanya maendeleo kwani anashindwa kuandaa mrithi ambaye ana uwezo kama wake wa kuipeleka Rwanda mbele?? Je akifariki ghafla si ndio mambo ya nchi kuingia vitani sababu ya ombwe la uongozi
Ni vyema apishe awaachie hata wahutu muhula mmoja ili tension za ukabila ziishe na baada ya hapo watutsi watawale milele ila kitendo cha kagame kuitawala Rwanda tokea miaka ya 90 mpaka 2034 sidhani kama wahutu watakubali itapelekea vita nyingine huko mbeleni