Historia ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda: Kilio Cha Mifereji ya Damu iendayo Ethiopia

Hii ni Kigali Rwanda
poor-district-kigali-rwanda-B9PMP6.jpg
images%20(3).jpeg
 
Mipira ya kondomu yatolewa bure mitaani Rwanda

24 Mei 2016

Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Mshirikishe mwenzako

Image captionVibanda vimewekwa sana katika mitaa yenye viwango vya juu vya maambukizi

Nchini Rwanda, mipira ya kondomu imeanza kutolewa bure katika baadhi ya mitaa jijini Kigali ambayo inaaminika kuwa imekithiri kwa ukahaba na kuwa na idadi kubwa ya walioambukizwa virusi vya Ukimwi.

Vibanda vidogo vimewekwa katika mitaa hiyo kwa ajili ya huduma hiyo inayopatikana kwa saa 24.

Wizara ya afya ya Rwanda inasema asilimia 3 wa wananchi wanaishi na virusi vya Ukimwi na kwamba zoezi hilo litasaidia kupunguza kasi ya uambukizaji.

MATANGAZO

“Tulishuhudia watu wanaoacha kutumia mipira ya kondomu kwa sababu wameikosa, tukaamua kuleta hivi vibanda katika mitaa hii minne ya jiji la Kigali yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi,” anasema Dkt Sabin Nsanzimana, mmoja wa wanaohusika katika mpango huo.

“Kwa hiyo naamini tutafanikiwa kupunguza kasi ya maambukizi.”

Mfumo wa kisasa wa uchukuzi wazinduliwa Rwanda

Wizara ya afya ya Rwanda inasema imekuja na mbinu hii mpya ya kusambaza kondomu kwa bure baada ya kuona kwamba baadhi ya watu hushindwa kumudu bei ya kawaidia ya kondomu na wengine kuona haya kununua kondomu hadharani.

Bei ya kondomu kwenye maduka imekuwa kati ya Franka 300 na 500 za Rwanda ambazo ni karibu nusu dola ya Kimarekani.

Image captionRwanda inapanga kusambaza kondomu milioni moja mwaka huu

Kupitia mpango huu Rwanda inalenga kusambaza mipira ya kondomu milioni moja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Mwandishi wa BBC aliyepo Rwanda Yves Bucyana anasema miaka 5 iliyopita Rwanda ilijaribu mpango ambao haukufanikiwa wa kusambaza kondomu kwa kutumia mashine zilizowekwa katika sehemu za burudani.

Ili kupata kondomu ilibidi kutumbukiza vichele ndani ya mashine hizo ambazo katika sehemu nyingi sasa zimekwishaharibika.
 
KILIO CHA MIFEREJI YA DAMU IENDAYO ETHIOPIA

d954d4c1311a8378eafd4dd9a383321d.jpg


SEHEMU YA 13



Mnamo majira ya kama saa nne kasoro usiku Waziri Mkuu Agathe Uwilingiyimana alimpigia simu Jenerali Dallaire kumjulisha kwamba kwa taarifa za uhakika kabisa alizo nazo ni kwamna ndege iliyodunguliwa ilikuwa ni ya Rais Juvenile Habyarimana na Rais alikuwa ndani ya hiyo ndege.

Dallaire alipiga simu mpaka makao makuu ya UN nchini Marekani kuwajulisha kuhusu taarifa hii na kisha akaelekea kwenye kikao cha kamati ya dharura ya kijeshi iliyoitoshwa na Kanali Bagorosa.



Twende mbele kidogo….



Nadharia: 'nani alimfunga paka kengele'

Kumekuwa na ripoti nyingi mno mno kila moja ikijaribu kuchambua ni nani hasa walihusika kudungua ndege ya Rais Habyarimana.
Na kwa mfano tukisema tuchukue ripoti 100 juu ya kisa hiki… ripoti 50 kati ya hizo zitatuhumu Wahutu wenye msimamo mkali na ripoti 50 zitatuhumu Kagame na RPF.

Lakini kwa wale ambao wanaamini kwamba Wahutu wenye msimamo mkali walitekeleza tukio la kumuua Rais Juvenile Habyarimana hoja yao kuu ambayo wanaitumia ni juu ya ushahidi wa baadhi ya watu wanaodai walishuhudia tukio lile kwa macho.

Kwamba; kuna askari wa kibelgiji ambaye alikuwa juu kwenye moja ya mnara wa kuongozea ndege ambao ulikuwa hautumiki, na wanajeshi waliutumia kama sehemu ya kuweka askari wa ulinzi. Mwanajeshi huyu anadai kwamba wakati ndege ya Rais inafanya 'final approach' ili iweze kutua aliona kitu kama moto (surface-to-air missile) ikitoka ardhini na kwenda kudungua ndege. Sekunde kadhaa baadae aliona moto mwingine ukipamda juu na kwenda kuidungua tena ndege na kuidondosha ardhini kwenye eneo la Ikulu.

Mwanajeshi huyu alipoulizwa aeleze eneo ambalo bomu lilirushwa kutoka ardhini alieleza eneo ambalo liko karibu kabisa na Kanombe Barracks ambayo ni kambi ya kijeshi ya Jeshi la Rwanda.

Pia kuna mwanajeshi mwingine na raia nao wanatoa maelezo kama haya.

Sasa basi kama bomu lilirushwa kutoka eneo la Kanombe Barracks ambalo ni himaya ya jeshi la Rwanda (Maana yake ngome ya Wahutu) hii inawaondoa kabisa RPF kwenye lawama ya kuidungua ndege.

Hii ndio nadharia ambayo inatumika sana kwenye kuhusisha Wahutu wenye msimamo mkali na udunguji wa ndege ya Rais Habyarimana.

Hoja nyingine inayotumika sana ni kama ile ambayo nilieleza awali, kwamba katika kipindi hiki wahutu wenye msimamo mkali walikuwa wanamchukia mno Rais Habyarimana kwa kitendo chake cha kujiingiza kwa migui yote kwenye mazungumzo ya amani jijini Arusha.

Lakini nadharia hii ni ya ujumla mno na inaacha masuala muhimi sana. Uchunguzi wa kisa hiki haupaswi kutegemea ushahidi wa watu na kufikia hitimisho. Watu wanaweza kukaririshwa tu cha kusema na kupotosha.
Kisa hiki kinapaswa kuchunguzwa kitaalamu kwa ushahidi wa Ballistics, acoustics na masuala ya forensic. Ubaya ni kwamba Umoja wa Mataifa ni kama vile hawataki kabisa kulizungumza suala hili. Na serikali ya Rwanda ya sasa chini ya Paul Kagame msimamo wao ni kwamba wahusika wa tukio lile walikuwa ni wahutu wenye msimamo mkali, na serikali haitaki mjadala wowote wala uchunguzi wowoye zaidi.

Pengine nia yao ni njema… hawataki kufukua makaburi ambayo yanaweza kutonesha vidonda na kuiweka nchi yao katika hali tete au kuwarudisha tena kwenye misuguano na chuki za kikabila.

Lakini japokuwa labda suala hili halitakiwi kuguswa kwa sababu za msingi kabisa… lakini wanadamu tumeumbwa na 'curiosity'.! Kiu ya kutaka kujua… na kiu hii ni kama vile upele, mpaka pale utakapojikuna ndipo utaacha kuwasha. Binafsi nadhani suala hili lingeruhisiwa (au kutolewa majibu sahihi) tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000s pengine watu wangekuwa wamesha 'move on' na masuala mengine na kuacha kukuna vichwa juu ya nani hasa alihusika.

Sasa basi, binafsi naliona sula hili kama ifuatavyo;

fe3d143539e3534a19118a08dcb5634e.jpg

Jenerali Romeo Dallaire kamanda wa vikosi vya UNAMIR nchini Rwanda


Kwanza kabisa nionyeshe wasiwasi wangu juu ya hii nadharia kwamba Wahutu wenye msimamo mkali ndio walidungua ndege ya Raia Juvenal Habyarimana.

Kwanza kabisa mpaka sasa kwa chunguzi zote ambazo zimefanyika na ushahidi wa ballistics zinaonyesha kwamba bomu la 'surface-to-air' ambalo lilitumika kudungua ndege ya Rais Habyarimana na kuweza kuidondosha ilikuwa ni aina ya 'SA-16'. Bomu hili lenye uzito wa kilo 11 yalitengenezwa nchini Urusi.

Sasa mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya kuisha vita baridi Urusi waliuza silaha nyingi sana kwa nchi za Ulimwengu wa tatu. Moja wapo ya biashara hizi walifanya na jeshi la Uganda ambalo pamoja na silaha nyingine pia waliwauzi kiasi kikubwa cha mizinga ya SA-16.
Kwa upande wa jeshii la Rwanda halikuwa kununua au kuwa na mizinga aina ya SA-16. Watu pekee ambao walikuwa na uwezo wa kuwa na mizinga ya aina hii walikuwa ni RPF kutokana na uswahiba wao na jeshi la Uganda na Yoweri Museveni ambao waliuziwa mizinga hii na Urusi.

Hii ni suala la kwanza ambalo linafanya kidole kilichonyooshwa kugeukia RPF.


Lakini pia kuna masuala kadhaa ya kuyaangalia na kuyakumbuka tukiwa tunajadili na kujaribu kutegua kitendawili hiki… tuangalie masuala kadhaa haraka haraka.


Wakati wa kuundwa kwa kikosi cha UNAMIR kulitokea mabishano makali sana kwenye baraza la kudumu la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN Security Council) ambapo Marekani alikuwa anapingana na wajumbe wengine wote wa baraza kuhusu uwepo wa vikosi vya UNAMIR nchini Rwanda na akitaka viondolewe haraka. Hoja ambayo walikuwa wanaijenga ni ati kwamba hawataki kitokee kama kile ambacho kilitokea mwaka mmoja nyuma nchini Somalia katika "Battle of Mogadishu" ambayo ilizua mzozo mkubwa wa Kidoplomasia baada ya majeshi ya Marekani kuingila mzozo wa ndani wa nchi ya Somalia.
Hoja hii haikuwa na mashiko sana kutokana na utofauti mkubwa wa asili za oparesheni hizo. Ilikiwa dhahiri kwamba Marekani walikuwa na dhamira nyingine kabisa ambayo hawakuwa wakiisema.

Mwishoni wakafikia 'compromise' kwamba UNAMIR iongezewe muda wa miezi mitatu wakati baraza la Usalama likitafakari kama kuviondoa vikosi hivyo moja kwa moja au viendelee kubaki.
Hivi ndio namna ambavyo uwepo wa UNAMIR uliendelea na mpaka muda wa mauaji ya kimbari yalipoanza. Safari hii ilikuwa ni oparesheni ya muda mfupi na Marekani alipinga kwa nguvu zote na kukataa kuchangia askari.

Hili ni suala la kwanza ambalo nahitaji ulijue na ulikumbuke tunavyojadili suala hili.

Suala la pili ni kwamba katika moja ya nyaraka za siri ambazo zimekuwa 'declassified' na serikali ya Marekani na kuwekwa kwenye programu ya 'National Security Archives' kwenye chuo kikuu cha George Washington inaonyesha balozi wa Marekani nchini Rwanda kipindi hicho aliandika 'memo' kwenda kwa Waziri wa Ulinzi kuonyesha wasiwasi wake kwamba kuna uwezekano wa tukio la hatari kutokea na akasisitiza kama tukio hilo likitokea basi kuna uwezekano wa zaidi ya watu laki tano kuuwawa ndani ya Rwanda. (Sehemu ambazo tukio hilo balozi analitaja zimefutwa kwenye nyaraka).

Hii inathibitishwa pia na nyaraka nyingine za CIA zenye tarehe za mwanzoni kabisa mwa mwaka 1994 (January na February) zikionyesha kutabiri kutokea kwa vifo vya watu nusu milioni nchini Rwanda kutokana na uchambuzi wa mfululizo wa matukio ambao walifanya pamoja na intelijensia ambayo walikuwa nayo.

Kwa hiyo unaweza kuona kwamba Marekani alikuwa ana hakika kabisa kwamba kulikuwa kunaenda kutokea tukio kubwa ambalo litagharimu maisha ya zaidi ya nusu milioni wa raia wa Rwanda lakini ajabu halikuwa kwenye vikao vya baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa anapinga UNAMIR kuendelea kuwepo nchini Rwanda.

Hili ni jambo la pili ambalo nataka ulikimbuke tunapoangalia kutokea kwa tukio hili la ndege ya Rais Habyarimana kudunguliwa na hatimaye mauaji ya kimbari kuanza.

492b01a62e8a738136eacf4f60617080.jpg


Lakini pia trehe 22 January 1994, ndege ya mizigo aina ya DC-8 (wengine huziita McDonnell Douglas DC-8) ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali ikiwa imebeba shehena ya silaha kwa ajili ya jeshi la Rwanda.
Hii ilikiwa kinyume kabisa na mazungumzo ambayo yalikuwa yanaendelea Arusha ambapo kila upande (yaani RPF na Serikali) walitakiwa kuacha kununua silaha au kuongeza ukubwa wa jeshi.

Kuna mtu alimpenyezea taarifa hii Jenerali Dallaire kuhusu ndege hiyo iliyoleta shehena ya mizigo. Dallaire alichukua wanajeshi wake na kwenda mpaka uwanja wa ndege wa Kigali na kuiweka chini ya Ulinzi ile ndege kwa hoja kwamba kilichokuwa kinafanyika ilikuwa ni kinyume kabisa na Makubaliano ya Arusha (Arusha Accords).
Dallaire alituma telegram mpaka UN kuwataarifu kuhusu hiki kinachoendelea. Ajabu ni kwamba UN walimuamuru asijihusishe na chochote kile zaidi ya "kulinda amani". Yalitokea mabishano makubwa sana kati ya Dallaire na wakubwa wake.

UN walikuwa na hoja pengine ya msingi kwamba vikosi vya UNAMIR vilikuwa Rwanda kwa ajili ya kulinda amani na si kujihusisha moja kwa moja migogoro ya nchi ambayo ilikuwa inaendelea.
Lakini Dallaire alijenga hoja kwamba mitaani wanajeshi wa Rwanda walikuwa wameanzisha utaratibu wa kukagua vitambulisho vya raia ili kujua kama ni Muhutu au Mtusi. Aliwaeleza kwamba kuna jambo la hatari linapangwa na wanaweza kulizuia kabla halijatokea. Lakini UN (wakiongozwa na Marekani) waliweka msimamo kwamba hawampi ruhusa ya kukamata shehena hiyo.

Hili ni tukio lingine la nne ambalo tunahitaji tulifahamu na tulikumbuke.

Tuangalie suala lingine muhimu pia…

Kama ambavyo nimeeleza tangu mwanzo wa makala hii kwamba RPF iliundwa nchini Uganda kwa msaada mkubwa wa Jeshi la Uganda na Museveni kutokana na uswahiba wake na kushibana na Paul Kagame na Fred Gusa Rwigyema.

Suala hili la uundwaji wa RPF na msaada wa jeshi la Uganda lilikuwa linajulikana linajulikana vyema na CIA kupitia ofisi yao ya balozi jijini Kampala Uganda kama ambavyo inathibitidhwa na nyaraka ambazo CIA wameziachia kwenye National Security Archive chuo kikuu cha George Washington. Suala hili la uundwaji wa RPF na msaada wa jeshi la Uganda kwenye uundwaji wake ilikuwa kinyume kabisa na UN Charter pamoja na kanuni za Umoja wa Africa.

Lakini CIA hawakuwahi kusema lolote kuufungua macho ulimwengu kuhusu hiki ambacho kilikuwa kinaendelea kwa siri kubwa.

Badala yake kwenye mwanzoni mwa miaka ya tisini Marekani iliongeza kiwango cha misaada ya kiutu na misaada ya kijeshi maradufu kwa Uganda.

Jenerali Dallaire wa vikosi vya UNAMIR alianza kupata wasiwasi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa jeshi Uganda walikuwa wanasaidia wapiganaji wa RPF kinyume na makubaliano ya Arusha, kanuni za Umoja wa Mataifa na UN Charter.

Mwanzoni Museveni alitoa tamko kwamba wanajeshi wote wa Uganda waliokwenda kupigana nchini Rwanda (RPF) hatowaruhusu kuvuka mpaka kurejea Uganda.
Hij ilikuwa ni geresha tu kwani Kagame na wapiganaji wake walikuwa wakivuka kwenda na kurudi mpaka wa Rwanda na Uganda kama watakavyo.

Kwa hiyo hata UN ilipomuamuru Museveni kutosaidia RPF licha ya Museveni kuahidi kwamba hawezi kufanya hivyo, Jenerali Dallaire alikuwa na kila sababu ya kuamini kwamba Uganda bado walikuwa wanasaidia RPF kwa siri.

Ndipo hapa akaomba ruhusa awe anakagua mpaka wa Uganda na Rwanda ili kuhakikisha kwamba hakuna silaha ambazo zilikuwa zinakatiza mpakani hapo kuingia Rwanda. UN walimruhusu. Lakini Uganda walitoa sharti kwamba kabla ya Dallaire na wanajeshi wake hawajaenda mpakani wanapaswa kutoa taarifa masaa 12 kabla ili wawapatie 'escort'.

9e6a5d51b0eab07a426486e8ca12043e.jpg


Dallaire alipinga vikali kwanza akisema kuwa hawahitaji 'escort' lakini pia ukaguzi huo unatakiwa kufanywa kwa 'suprise' kwani kama taarifa ikitolewa masaa kumi na mbili kabla kama kuna shughuli zozote za upitishaji silaha utafanyika haraka au kusitishwa kabla hawajaenda.
Mabishano yalikuwa makali na hatimaye Dallaire hakuwa na namna nyingine zaidi ya kukubaliana na sharti hilo la kutoa taarifa masaa kumi na mbili kabla hawajaenda kwenye uchunguzi.

Katika ushahidi wake ambao Dallaire aliutoa kwa Bunge la Congress nchini Marekani mwaka 2004 alisema kwamba, alipata taarifa pia juu ya uwepo wa ghala kubwa la silaha ambalo lilikuwa linatumiwa na Uganda kwa ajili ya wapiganaji wa RPF. Ghala hili lilikuwa kwenye mji wa Mbarara ambao huko kilomita 80 tu kutoka mpakani.
Dallaire alipotaka kufanya uchunguzi kwenye ghala hili jeshi la Uganda lilikataa katakata.

Masuala yote haya juu ya visanga hivi vya jeshi la Uganda na serikali yake pamoja na msaada wao wa siri wanautoa kwa RPF ulikuwa unajulikana na ofisi za ubalozi wa Marekani jijini Kampala na CIA pia walikuwa wanajua.

Lakini ajabu ni kwamba hawakuwahi kusema lolote na badala yake walizidisha ukaribu na nchi ya Uganda.

Mwanzoni mwa mwaka 1994 kilifanyika kitu cha ajabu na kushitua sana ambapo sasa tukitazama nyuma historia tunaweza kusema kwa hakika kabisa kulikuwa na maslahi yaliyowafanya Marekani kujihusisha kwa siri kubwa kwenye mgogoro wa Rwanda na hata kusaidia kwenye mchoro wa Kudunguliwa kwa ndege ya Rais Habyarimana.
Mwanzoni mwa mwaka 1994 nchi ya Uganda ilifanya manunuzi ya kihistoria ya silaha kutoka Marekani. Manunuzi haya yalikuwa yanazidi kwa mara kumi manunuzi yote ya silaha Uganda iliyofanya kwa Marekani kwa muda wa miaka arobaini iliyopita. Yaani kwamba ukijumlisha manunuzi ya silaha ya Uganda kutoka Marekani kwa muda wa miaka arobaini iliyopita, hayafikii yale yaliyofanyika mwanzoni mwa mwaka 1994 pekee na yanazidi mara kumi manunuzi ya nyuma ya miaka arobaini.
Kwa mwaka huo bajeti ya serikali ilikuwa 48% ya fedha yote ya bajeti ilienda kwenye jeshi huku 13% tu ikitengwa kwa ajili ya elimu na 5% kwa ajili ya Afya.

Kwa wachambuzi wa masuala ya jeshi hii ilikuwa ni dalili tosha kuashiria kwamba kuna maandalizi ya kitu fulani cha kijeshi yanafanyika.

Marekani na CIA walikuwa wanajua kila ambacho kilikuwa kinaendelea na japokuwa suala hili lilikuwa linavunja kanuni za kimataifa Marekani walikaa kimya.
Ni katika kipindi hiki pia ndipo ambapo Marekani waliongoza nchi nyingine kumpigia upatu rais Yoweri Museveni kuwa ni kiongozi bora na mfano wa kuigwa barani Afrika.

Tofauti na sasa ambapo Museveni anapigwa vita na mataifa ya magharibi, hii ilikuwa ni tofauti kabisa na mwanzoni mwa miaka ya tisini ambapo Museveni alipigwa upatu kama shujaa, mwanafalsafa na kiongozi wa kuigwa na wote Afika licha ya masuala yote ya siri yaliyikuwa yanaendelea nyuma ya pazia huki Marekani na CIA wakiyafahamu.

Mwishoni mwa mwezi March 1993… (wiki chache tu kabla ya ndege ya Rais Habyarimana kudunguliwa na Mauaji ya Kimabari kuanza), Rais Yoweri Museveni alisafiri kwenda Minneapolis, Marekani ambako alitunukiwa tuzo ya utumishi uliotukuka ya Hubert H. Humphrey na kisha kutunukiwa shahada ya heshima ya uzamivu (Honorary Doctarate) kutoka chuo kikuu cha Minnesota.

Dean chuoni hapo (ambaye ni afisa mstaafu wa World Bank) alimsifu Yoweri Museveni kama kiongozi mahiri ambaye ni tumaini kwa kurejea kwa demokrasia Afrika. Vyombo vya habari navyo vilimwagia sifa kede kede, kuna gazeti liliandika "Uganda is one of the few flickers of hope for the future of black Africa."
Gazeti maarufu la New York Times walimfananisha Museveni na Nelson Mandela. Huku jarida maarufu la TIME wakimuita Museveni kuwa ni "herdsman and philosopher….. and central Africa's intellectual compass."

Ilikuwa ni ajabu mno kuona utukufu huu ambao Musevi alikuwa anapewa na mataifa ya magharibi wakiongozwa na Marekani ukilinganisha na kile ambacho kilikuwa kikiendelea kwa siri huku Marekani na CIA wakijua.

Baada ya kutoka chuo Kikuu cha Minnesota, Yoweri Museveni alielekea White House ambako alifanya kikao cha faragha na Rais Bill Clinton pamoja na National Security Adviser aliyeitwa Anthony Lake. Rekodi za kuhusu walichoongea hazipo mpaka leo hij ikimaanisha kwamba bado ziko sealed, lakini kwa mfululizo huu wa matukio nilioeleza unaweza kukisia ni nini kiliongelewa.



Nikirejea tutaunganisha nukta za mfululizo wa matukio haya na kufanya hitimisho langu la kudunguliwa kwa ndege ya Rais Juvenal Habyarimana…. stay here.




Habibu B. Anga alias 'The Bold' - 0718 096 811
To Infinity and Beyond


Pls: WhatsApp, Follow and subscribe
am waiting.....!!!
 
Hizo hata sauzi zipo, this is Africa
Im glad you know that , so what the he'll was this mentally retarded whore who goes by the name Jestkilla was bragging about. ? .............The vast portion of África is still a filthy & stinking shithole , and what we need is putting aside our ethnic differences , having a sense of one identity as Africans and struggling together to make Our countries great ................Tribal hatred won't get us anywhere .......
 
Mkuu gadaffi alikuwa mzalendo zaidi ya kagame ila udikteta wake ma kukandamiza wakosoaji huku akiwanyima uhuru wananchi kulifanya apinduliwe na vijana wa kijiweni tu......

Kagame hata kma kafanya maendeleo kwani anashindwa kuandaa mrithi ambaye ana uwezo kama wake wa kuipeleka Rwanda mbele?? Je akifariki ghafla si ndio mambo ya nchi kuingia vitani sababu ya ombwe la uongozi

Ni vyema apishe awaachie hata wahutu muhula mmoja ili tension za ukabila ziishe na baada ya hapo watutsi watawale milele ila kitendo cha kagame kuitawala Rwanda tokea miaka ya 90 mpaka 2034 sidhani kama wahutu watakubali itapelekea vita nyingine huko mbeleni
Maisha ya Libya before Gadafi, Libya with Gadafi, Libya after Gaddafi... changanua hapo... acha habari za kumezeshwa... shirikisha ubongo wako ambao ninaamn uko vzur tu
 
Maisha ya Libya before Gadafi, Libya with Gadafi, Libya after Gaddafi... changanua hapo... acha habari za kumezeshwa... shirikisha ubongo wako ambao ninaamn uko vzur tu
Kwahiyo ina maana unashabikia kagame kutawala hadi 2034??

Nachosema ni kwamba maendeleo hayana faida kama hakuna AMANI..... Nchi ambayo ina tension ya kikabila kama Rwanda amani inatakiwa iwe priority kuliko mabarabara na majumba hivyo basi badala ya kagame kufocus kwenye maendeleo pekee afocus pia kwenye kuunda umoja wa kitaifa

Ndio natolea mfano gadaffi aliinvest kwenye maendeleo ya kiuchumi ila alisahau maendeleo ya kijamii hivyo kusababisha nchi kuingia vitani..... Leo kagame anaonekana shujaa ila udikteta na ukabila utasababisha Rwanda iishie kama libya

Muda utaongea
 
Tatizo lako mtoa nyuzi umekuwa na bias ,na unataka kutujengea mazingira kuwa Kagame alikuwa kiongozi bora...umeshaonyesha kuegemea upande mmoja kuanzia story yenyewe,picha etc kumbe ujui kuwa watu wengi wanainformation ya Rwanda kabla ya vita na baada ya mauaji etc.
Umeamua kuonyesha maaba yako wazi wazi kwa PK sasa hii inatilia shaka usahihi ya unayotaka kutuhaminisha.
 
Im glad you know that , so what the he'll was this mentally retarded whore who goes by the name Jestkilla was bragging about. ? .............The vast portion of África is still a filthy & stinking shithole , and what we need is putting aside our ethnic differences , having a sense of one identity as Africans and struggling together to make Our countries great ................Tribal hatred won't get us anywhere .......
Well said, hata hao watusi waliojipa u first class citizen ukweli ni kwamba wanawahitaji wahutu ili kujenga nchi yao so hakuna binadamu anaeweza kuishi peke yake, everybody needs someone especially neighbors so superiority ni kitu cha kupuuzwa! Naamini kufikia 2040 tribalism itakuwa inakaribia kuisha kabisa huko chigali
 
Kwahiyo ina maana unashabikia kagame kutawala hadi 2034??

Nachosema ni kwamba maendeleo hayana faida kama hakuna AMANI..... Nchi ambayo ina tension ya kikabila kama Rwanda amani inatakiwa iwe priority kuliko mabarabara na majumba hivyo basi badala ya kagame kufocus kwenye maendeleo pekee afocus pia kwenye kuunda umoja wa kitaifa

Ndio natolea mfano gadaffi aliinvest kwenye maendeleo ya kiuchumi ila alisahau maendeleo ya kijamii hivyo kusababisha nchi kuingia vitani..... Leo kagame anaonekana shujaa ila udikteta na ukabila utasababisha Rwanda iishie kama libya

Muda utaongea
Hata miaka 100 kama akiwa hai akae tu, viongoz aina ya Kagame wanatokeaga mara moja moja

Kwamba Gadafi alisahau maendelea ya kijamii? Libya ya wapi unazungumzia? Rwanda hakuna amani?

Mfano mzuri ni China, sababu ya kumfanya Xi Jinping atawale maisha yake yote unaijua? watu wa vile wanatokea mara moja moja, angalia yule mwanamama pale ujeruman
 
Back
Top Bottom