Historia ya Mapinduzi unapoieleza chukua tahadhari kidogo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,916
30,259
HISTORIA YA MAPINDUZI UNAPOIELEZA CHUKUA NA TAHADHARI KIDOGO

Ukiwa mwandishi watu wengi wanakujua bila wewe hata kukutana nao hata siku moja.

Siku moja nilikuwa Dubai kitongoji cha Rashidiyya na ikasadifu kuwa siku hiyo ni siku ya kusoma kisa cha Isra na Miraji.

Aliyekuwa anasoma alikuwa Dr. Ahmed bin Sumeit akitokea Muscat, Omani ambae mimi nilifahamiana nae kwa mara ya kwanza Kampala kwenye mkutano uliowakutanisha Waislam kutoka sehemu tofauti za dunia.

Rashidiyya hii ndiyo sehemu ambayo Wazanzibari wengi walipokelewa na wakapatiwa hifadhi baada ya kukimbia Zanzibar baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1964.

Hapa Rashidiyya kwa sababu hii kuna jamii kubwa sana ya Wazanzibari.

Nikaja kukutananae tena Johannesburgna Lamu kwenye Maulid ikawa sasa ni watu tunaofahamiana vizuri.

Ahmed bin Sumeit ni mwalimu wa ''micro biology'' Chuo Kikuu Cha Sultan Qaboos na vile vile ni sheikh na anatoa darsa nyingi za mafunzo ya Kiislam Oman.

Sasa aliponiona pale msikitini baada ya shughuli ile akanifuata nilipokuwa nimekaa kusalimiana na hapa ndipo na watu wengine wakaanza kama vile kuniangalia na kujua kuwa mingozi mwao kuna mgeni katoka Tanzania ikawa sasa, ''Wewe si Mohamed Said?'' nk. nk.

Baada ya kula chakula pale msikitini akatokea kijana mmoja akanikaribisha ofisini kwake pale msikitini akanambia angependa kunitembeza kwenye msikiti mzima anionyeshe wanayofanya pale.

Hivi ndivyo tulivyojuana ikapelekea kunieleza kisa kilichomtokea baba yake wakati wa mapinduzi.

Anasema yeye alikuwa mtoto mdogo labda wa miaka mitano.

Siku ya mapinduzi asubuhi yake nyumba yao ilivamiwa na katika hao wavamizi alikuwa jirani yao familia zao zikijuana vyema.

Baba yake alitolewa nje ya nyumba na kupigwa risasi yeye akiona kwa macho yake.

Baada ya baba yake kupigwa ile risasi alianguka chini na yule jirani yake akamfuata pale chini na kumpiga teke.

Nilimpa pole kisha sote wawili tukawa kimya mimi nimeinama nimeimisha kichwa changu na yeye pia kainamisha chake kwa huzuni bila shaka kwa kurejesha ile picha ya kumbukumbu ya marehemu baba yake.

Kwa kuuvunja ule ukimya nikamuuliza alikuja lini Dubai na kama huwa anakwenda Zanzibar.

Akaniambia kuwa anakwenda Zanzibar na katika moja ya safari zake alikutana na yule mtu aliyempiga teke marehemu baba yake.

Huyu bwana amepooza upande mmoja anatembea kwa kuburuza mguu akicha vumbi likimfuata nyuma.

Nashukuru kuwa leo nimepata nafasi ya kukieleza kisa hiki cha mtoto aliyedhulumiwa roho ya baba yake na Allah akawaweka wote wawili dhalim na yule aliyedhulumiwa na kuwakutanisha hapa hapa duniani.

Amekuja bint mtangazaji wa East Africa Radio Mackriner Siyovelwa kutaka tufanye mahojiano na mimi kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.

Kipindi ambacho In Shaa Allah watakirusha leo siku ya sherehe ya kumbukumbu ya mapinduzi.

Katika mengi ambayo nimeeleza nimesema kuwa historia ya mapinduzi inataka mtu unapoihadithia uchukue tahadhari sana na uchunge ulimi wako mno ili kuweka staha kwa wale ndugu zetu waliopoteza wapendwa wao kwani kuna mengi yaliyopitika ya kusikitisha.

Picha ya kwanza mahojiano na East African Radio kuhusu mapinduzi na ya pili kulia ni Dr. Ahmed bin Sumeit na Mwandishi, Lamu.
KUKU.jpg
 
Waliua watu wasiopungua 20,000. halafu bado wamejibandika utukufu wa waliyoyafanya.

Mwisho wa CCM unakaribia
 
Back
Top Bottom