Historia ya machinjio ya Kawe (cows way)

wakukurupuka1

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
525
1,182
Kati ya mwaka 1947 mpaka 1975 wakoloni waingereza walikuwa ni wamiliki wa kiwanda kilichokuwa kinaitwa TANGANYIKA PACKERS LTD (TPL) kiliajiri wafanyakazi zaidi ya 1200 na walikuwa wanafanya kazi kwa shift na walichukuliwa kwa mabasi ya kazini.

Mpaka mwaka 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kuingia serikalini kufuatia sera za ujamaa, kiwanda kilikuwa kikubwa sana, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje ya nchi mpaka kwa malikia wa Uingereza.

Neno KAWE maana yake ni COWS WAY yaani njia za ng'ombe, Serikali ilivyokichukua tu kwanza walinyimwa leseni ya kusafirisha nje (walinyimwa cheti kilichokuwa kinaitwa PHYTOSANITARY CERTIFICATE cheti cha kuthibitisha ubora wa vyakula vya package).

Hivyo soko la ndani likawa gumu kikawa kinasambaza nyama zake kwenye mabucha ya Dsm na badae kija kufa mwaka 1993! Pana mbunge mmoja wa Kawe alikinunua kwa Bei ya chini sana nae akashindwa kukiendesha hatimae akaanza kuuza mashine na baadhi ya vipuri kama chuma chakavu na mwishoe kikafa kabisa!

IMG_8972.jpg
 
Kati ya mwaka 1947 mpaka 1975 wakoloni waingereza walikuwa ni wamiliki wa kiwanda kilichokuwa kinaitwa TANGANYIKA PACKERS LTD (TPL) kiliajiri wafanyakazi zaidi ya 1200 na walikuwa wanafanya kazi kwa shift na walichukuliwa kwa mabasi ya kazini, mpaka mwaka 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kuingia serikalini kufuatia sera za ujamaa.

Kiwanda kilikuwa kikubwa sana, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje ya nchi mpaka kwa malikia wa Uingereza, Neno KAWE maana yake ni COW WAY yaani njia za ng'ombe, Serikali ilivyokichukua tu kwanza walinyimwa leseni ya kusafirisha nje (walinyimwa cheti kilichokuwa kinaitwa PHYTOSANITARY CERTIFICATE cheti cha kuthibitisha ubora wa vyakula vya package)
hivyo soko la ndani likawa gumu kikawa kinasambaza nyama zake kwenye mabucha ya Dsm na badae kija kufa mwaka 1993!
Pana mbunge mmoja wa kawe alikinunua kwa Bei ya chini sana nae akashindwa kukiendesha hatimae akaanza kuuza mashine na baadhi ya vipuri kama chuma chakavu na mwishoe kikafa kabisa!

Baada ya kufa kabisa familia nyingi za Kawe zilikosa ajira na kuanza kuhangaika huku na kule

Maono ya mamlaka yameonelea ni heri kuyapangisha majengo husika kwa manabii na mitume ili wawaombee wakazi wa Kawe na Watanganyika wengine wapate ajira kwa njia za miujiza huku wakilipia huduma hiyo kwa njia ya sadaka nk
FB_IMG_1692755231773.jpg
 
Tamaa nyingi, mbele kiza. Walitegemea kuuza nyama huko ughaibuni wakasahau kuwa hawana nembo yao wenyewe kwenye vile vikopo vyao na pia vyeti vya kuthibitisha ubora wa Nyama hiyo.
 
mbunge mmoja wa Kawe alikinunua kwa Bei ya chini sana

Inasikitisha sana, historia hii iwe funzo.

Haiwezekana Tanzania ina mifugo mingi katika Afrika halafu nyama inaoza bucha pia wafugaji kukosa soko la uhakika kwa maamuzi mabaya kisa uzalendo wa kijamaa.


Wenzetu kama nchi ya Brazil n.k wanaendelea kuuza nyama ya vikopo duniani kote sisi imebaki simulizi.
 
Back
Top Bottom