Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,720
- 1,639
Mababu weusi wa kale huko misri walikuwa wanaamini kuwa Maisha na watu walikuwa na mwanzo, kivipi!!?
Elimu ya mababu hao inasema hapo mwanzo kulikuwa na maji yaliyokuwa yamejaa Dunia Nzima pamoja na Giza Zito,
Siku moja kikazuka kama kisiwa kidogo katika yale maji, na juu ya kisiwa hicho alisimama Atum/ Adam/ Temu/ Atom / Mungu/Mtu wa kwanza
Atum alikohoa na kwenye hayo makohozi alitoka mwanaume aliyeitwa "SHU"
Atum alitema mate likiwa ni tendo lake la pili akamtema mwanamke "TEFNUT"
Atum akapita kila kona ya Ulimwengu na kuumalizia katika uumbaji, maana yalikuwa ni maji tu yaliyokuwa yamezunguka kila kona ya Dunia. Wanyama na kila kitu juu ya uso wa nchi vikafwanya kwa miujiza yake.
Siku Moja Atum aliwapoteza Shu na Tefnut, kitu kilichofanya awatafute kila mahali bila mafanikio!,
Atum alituma Jicho lake la kulia lizunguke kila kona na kila mahali ulimwenguni kuwatafuta wanawe,
Mwisho Jicho lake hilo liliweza kuona watoto zake, hivyo Atum alipata furaha kuu, alilia machozi ya furaha huku akielea huku na huko katika Ulimwengu.
Machozi yale yalipokuwa yakianguka chini na kugusa ulimwengu yalikuwa yakiumba watu katika rangi na hali tofauti.
Shu na Tefnut (hawa tunaweza kuwaita kama ndo uzao wa kwanza wa watawala wa kibinadamu) walizaa watoto wawili yaani GEB na NUT hao walipendana sana wao wakazaa watoto wanne, Seth, (Mungu wa maovu) Nephtys, Osiris (Mungu wa chini ya Dunia) na Isis (Malkia).
Baada ya watoto wale kuzaliwa shu alimrusha juu ya anga NUT ili aende juu angani akasimamie kila kitu juu ya anga la Dunia na GEB akalazwa chini katika Ardhi ili asimamie uso wote wa Dunia.
Osiris alimuoa Isis na kwa Muda huo Osiris akiwa ni mtawala wa Dunia yote, huku Seth akiwa kamuoa Nephtys miaka mingi ilienda lakini mambo hayakuwa shwari sana, Seth alikuwa na wivu mkuu kuwa kwanini Osiris kaka yake atawale Ulimwengu! Alikuza wivu wake siku hadi siku mpaka siku fulani alimfuata Osiris na kumuua na kumgawanya gawanya vipande, kisha kuvitupa huku na kule ili kufunga asiweze kuamshwa tena kama kipande chochote kitakosekana!
Hatimaye roho ya osiris ilishuka Chini ya Ulimwengu na ikaenda kutawala huko.
Huku Duniani hatimaye Seth akawa mfalme wa ulimwengu, huku mke wa Osiris akihangaika, na kulia kila siku, ila siku moja Isis alipata Mimba ya ajabu bila mwanaume, ikiwa ni roho ya osiris kuiweka mimba hiyo Tumboni mwa Isis,
Hatimaye Isis akaja kujifungua mtoto wa wa kuume aliyeitwa Horus/ Heru.
Horus alipokua mtu mzima akaja kusimuliwa jinsi babayake Osiris alivyouawa, na baba mgodo wake Seth, hivyo naye akapanga kisasi cha kuja kulipiza kisasi kwa Seth.
Hatimaje siku ya siku Seth na Horus walikutana na kilichofuata ilikuwa ni vita ya masaa kadhaa, Horus alipoteza jicho lake Moja ila mwisho wa siku alimuua Seth.
Na hatimaye Horus (mtoto) akawa mfalme wa Dunia na Osiris baba ake akiwa ni mfalme wa chini ya ulimwengu.