Historia ya Lema kabla ya kuwa mbunge

LENGISHO

Senior Member
Sep 15, 2017
169
245
1135636
62590770_853909188315847_8628533852870451973_n.jpg


Niligombea Ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2005 ,pamoja na biashara nyingine mbali mbali pia nilikuwa nafanya biashara ya dala dala.

Kwani nini leo nimeikumbuka hii picha ?Wakati huu Mimi na Neema(Mke wangu)tulikuwa na biashara ya duka la reja reja (Mini Supermarket),iliyoitwa Billionare.

Katika uchaguzi wa Mwaka 2005 niligombea Ubunge kupitia TLP. Nilifanya kampeni iliyo nijenga sana IMANI katika kuamini jambo,kuna wakati pesa za kufanya kampeni zilikuwa ni taabu sana,Mimi na Neema tuliamua kuwa yeye atakuwa anafunga biashara kabla ya saa tatu usiku,Hasan alikuwa dereva wetu ambaye kwa sasa ni marehemu tulimwambia awe analeta gari saa mapema kabla ya saa mbili na robo usiku.

Wakati huu mimi nilikuwa nachukua gari naanza kufanya route za Njiro vs Mjini huku Mke wangu akiwa anakusanya nauli,nilikuwa navaa kofia na abiria akitaka kushuka navua kofia najitambulisha,lakini namuomba asidai chenji aniachie inasaidie kampeni.

Abiria wengi walikuwa wanacheka na kufurahi na wengine kulipa zaidi ili kusaidia mkakati huu wa kuchanga fedha za kampeni,ulifanikiwa kwa kiasi kidogo lakini ulisaidia safari ya ndoto yangu.

Tulikuwa tunafikiria njia nyingi sana za kuhakisha kwamba hatukwami katika ndoto yetu, japo sio rahisi kueleza kila kitu leo,lakini mwaka huo nilishindwa Ubunge kwa mbinu chafu,sikukata tamaa baada ya hapo nilianza maandalizi kuelekea 2010.

Mwaka 2010 nilishinda Ubunge kwa mara ya kwanza na hata sasa bado ni Mbunge.

Hii stori leo itaishia hapa,lakini itoshe kusema kuwa ni kweli mambo yanaweza kuwa sio rahisi lakini elewa kuwa YANAWEZEKANA.

Nina fikiria katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani nitakuwa natoa simulizi vipande vipande kama hivi ili kuwatia moyo watu wanaotaka kuingia kwenye mapambano ili waone kuwa wanachohitaji zaidi ni Imani na Tumaini katika kushinda mapambano.
 
Kuna Jamaa aliniambia umefika nchi nyingi Takatifu ikiwamo Israel na unamtumaini Mungu Sana!
 
Tuwekee na ile picha uliyokuwa unafuga rasta huku ukiwa unafanya zile shughuli za siri.
Historia huwa inaandikwa kwa kuamua kipi kiwepo kipi kisiwepo Historia haimaanishi uelezee kama vile Unafanya kitubio.
Ndio maana Historia haitumbii Nyerere alikuwa na mke kabla ya Maria
 
Sasa Lema kaweka story yake wewe unaanza kumuomba aweke unayotaka. Weka yako na wewe unayoipenda likely huna cha kuijenga hadhira ya Lema
 
Labda anajisafisha.huyu yuko mbioni,kuelekea ccm,sema kamati kuu ilmkataa tangu mwanzo.anatapatapa
 
Back
Top Bottom