Nyumba Aliyolala Baba wa Taifa Kigoma Ujiji wakati wa Kupigania Uhuru wa Tanganyika 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,839
30,168
NYUMBA YA OMARI SELEMANI KAGOBE NA MNARA WA NYERERE KIGOMA UJIJI

Mbele ya nyumba ya marehemu Omari Selemani Kagobe umejengwa mnara unaojulikana kama Mnara wa Nyerere.

Mnara huu ni kumbukumbu yake Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere safari yake ya kwanza kufika Kigoma wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika safari hii Mwalimu Julius Nyerere alifikia nyumbani kwa Omari Selemani Kagobe.

Bahati mbaya mzalendo Omari Selemani Kagobe na wapigania uhuru wenzake hawafahamiki na historia hii haijapewa umuhimu unaostahili halikadhalika kumbukumbuku hii ya nyumba na mnara wake.

Ni suala la muda tu nyumba itatoweka na mnara sawia.

Kitakachobaki ni simulizi kuwa hapo ilikuwapo nyumba ya Omari Selemani Kagobe nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

1684472623670.png
 
Namfahamu mtoto wa mzee Omari, akiitwa Seleman Kagobe. Alikuwa idara ya uhasibu wizara ya mambo ya ndani miaka ya nyuma.

Ni miaka mingi tumepotezana, sijui kwasasa yuko wapi.
 
Back
Top Bottom