Historia ya kina Zanzibar

Ndy nini kilifanya wapemba waikatae ASP? kwani chama kilichoratibu mapinduzi ni chama gani? Maana najuwa tangu enzi za sultani Pemba walikuwa na vyama vyao vya harakati na unguja walikuwa na vyama vyao ,,nini kilipelekea kujiita wazi wazi Pemba peoples part..na afro Shiraz part?
 
Ukiangalia hivyo vyama kwa ujumla kirefu chake ni mashaka matupu....
ZPPP
ASP ...nadhani chuki zao zilianzia tangu huko nyuma,,na wala sio CCM mkuu..
 

kwa miaka hiyo Unguja ilizoeleka kuitwa Zanzibar japo kua haikuwa lugha sahihi lakini jamii ya wakati huo ilizoea hivo, kwa maana ile zanzibar and Pemba people party ilimaanisha Unguja na Pemba.
 
kwa miaka hiyo Unguja ilizoeleka kuitwa Zanzibar japo kua haikuwa lugha sahihi lakini jamii ya wakati huo ilizoea hivo, kwa maana ile zanzibar and Pemba people party ilimaanisha Unguja na Pemba.
Na hiyo afro shizar part ni watu gani? Nina maana hao afro Shiraz ndy walikuwa watu wa asili gani? Tukilijuwa hilo ndy tutajuwa mzizi wa chuki zao..
 
Ukiangalia hivyo vyama kwa ujumla kirefu chake ni mashaka matupu....
ZPPP
ASP ...nadhani chuki zao zilianzia tangu huko nyuma,,na wala sio CCM mkuu..

ASP kilianzishwa kwa misingi ya kibaguzi, na hata sera zake ndizo zilivyokuwa, na ndio mana wanaharakati wengi walikiacha njiani chama na wakajiunga na vyama vengine. kama si yale mapinduzi ASP ingejifia miaka michache tu mbeleni.
 
Na hiyo afro shizar part ni watu gani? Nina maana hao afro Shiraz ndy walikuwa watu wa asili gani? Tukilijuwa hilo ndy tutajuwa mzizi wa chuki zao..

Afro shirazi kilikua ni muunganiko wa wabara kwa kupitia umoja wao African Association ambao walikua kama ni tawi la TAA na watu wenye asili ya shirazi kwa ku[pitia umoja wao wa Shirazi Association. na ndio mana nikakwambia ASP kilitokana na mizizi ya kibaguzi
 
OK...nadhani ndy chuki zilianzia humo... Shukran Mkuu kwa taarifa
 
SOMA HAPA CHINI NA PICHA YA IQBAL MBUNIVU










Jamvi La Utubusara

April 18, 2016 ·
...

Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina zuri la Tanzania. Vijana wengi pengine hata wazee hawamjui wala kusoma historia yake kwani haifahamiki.
Mwandishi mmoja wa Redio Safari ya Mtwara Alphonce Tonny Kapelah alipata bahati ya kuonana ana kwa ana na kuzungumza na Mohammed Iqbal Dar akajieleza:
Swali: Uliingiaje katika shindano la kubuni jina la nchi?
Jibu: Siku moja nilikuwa maktaba nikijisoma Gazeti la Tanganyika Standard ambalo siku hizi linaitwa Daily News, mikaona tangazo lililosema: “Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana. Kwa hiyo wananchi wote mnaombwa kushiriki kwenye shindano la kupendekeza jina moja litakalozitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.”
Swali: Baada ya kuona tangazo hilo ukafanyaje?
Jibu: Niliamua kuingia kwenye shindano hilo.

Swali: Ulianzaanzaje kubuni jina linalofaa?
Jibu: Nilichukua karatasi nikaandika kwanza Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na imani ya dini yangu. Baada ya hapo nikaandika jina la Tanganyika kisha nikaandika Zanzibar halafu nikaandika jina langu la Iqbal halafu nikaandika jina la Jumuiya yangu ya kidini ya Ahmadiya. Baada ya hapo nikamrudia tena Mwenyezi Mungu, nikamuomba anisaidie ili nipate jina zuri kutoka katika majina hayo niliyokuwa nimeandika. Baada ya hapo nilichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar nikachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha anikaunganisha nikapata jina TANZAN.
Swali: Mbona halijakamilika?
Jibu: Nami niligundua kuwa halijakamilika hivyo nikachukua herufi ya kwanza ya jina langu ambayo ni herufi I katika jina langu la Iqbal kisha nikachukua herufi ya kwanza A ya jina la dini yangu yaani Ahmadiya. Niliandika jina la awali la TANZAN nikaunga na herufi hizo likawa TANZANIA nikaona ni jina kamili tena zuri.

Swali: Ulipopata jina hilo la Tanzania ulifanyeje?
Jibu: Kabla ya kulipeleka kunakohusika serikalini nilifanya utafiti mdogo na kugundua kuwa nchi nyingi za Afrika majina yao yanaishia na IA kwa mfano EthiopIA, ZambIA, NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA. Baada ya utafiti huo nikapendekeza na kuamua kwamba jina TANZANIA ndilo litumike kuwakilisha nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar. Kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka katika majina manne ambayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.
Swali: Ikawaje?
Jibu: Baada ya kujiridhisha kuwa jina hilo linafaa nikalituma kwenye kamati ya kuratibu shindano. Baada ya muda mwingi kupita baba yangu Dk. Dar alipokea barua nzito kutoka iliyokuwa Wizara ya Habari na Utalii ilisomeka kama ifuatavyo:
“Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar….ili iitwe Tanzania.
“Nafurahi kukuarifu kuwa mshirikiane zawadi ya sh.200 iliyoahidiwa na leo nakuletea cheki ya sh.12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh. 200.
Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiri jina la jamhuri yetu.”
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.
Swali: Kwani washiriki mlikuwa wangapi?
Jibu: Tulikuwa watu 16 lakini mimi nikaibuka mshindi lakini alijitokeza mtu mmoja, Yusufal Pir Mohammed aliyedai naye alishinda, hata hivyo, alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya uthibitisho na kupongezwa kama nilivyoandikiwa mimi na serikali, sasa nikapewa cheki ya shilingi 200 na zawadi ya ngao. Nilileta mabadiliko makubwa sana ya jina jipya. Ninachosikitika ni kuwa mchango wangu bado Watanzania hawauthamini lakini mimi naipenda Tanzania na najivunia kuwa Mtanzania ila naamini kuwa siku moja ukweli utajulikana.
Swali: Hivi sasa unaishi wapi?
Jibu: Kwa sasa naishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko nilipata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK, Dar es Salaam House, 18 Turnhouse Road.
Swali: Unaweza kutueleza historia yako kifupi?
Jibu: Mimi Mohamed Igibal Dar ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi, nilizaliwa mkoani Tanga mwaka 1944. Baba yangu alikuwa daktari wa binadamu mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dk. Tadar na alihamia Tanganyika kutoka India mwaka 1930. Nilipata elimu ya msingi mkoani Morogoro katika Shule ya Msingi H.H Agha Khan, kwa sasa ni shule ya serikali.
Baadaye nilijiunga na Shule ya Mzumbe nikasoma kidato cha kwanza mpaka cha sita.
 

Attachments

  • JAMAA[1].jpg
    32.3 KB · Views: 1
Na hii ikoje mkuu kihistoria,watu wa Pemba na unguja kuna chuki Fulani ya ndani ya nafasi zao? hebu nipe history yao mkuu, kabla ya ukoloni na baada ya kuja sultani.
Chuki zipo kote hata..mrima..na ubaguzi juu..
 
Kikubwa wapemba wengi wanawachukulia waunguja kama wasaliti, hii ni kutokana na yale mapinduzi ambayo yaligharimu damu za ndugu zao wengi.
Mapinduzi yalifanyika Unguja...walikufa wapemba wepi...
 
Hii paragraph yako ya mwisho umetulisha matangu pori. Kavipitie tena vyanzo vyako vya habari Bibie
 
Hakuna kitu hapa jina Tanzania lilibuniwa na Ikbar mwanafunzi wa Mzumbe kwa wakati huo kati ya October na Nov.1964.
 
Sultan Jamshid aliponzwa na woga wake na utoto maana vyama vyote vikimtambua kama mkuu wa nchi.Hakutakiwa kukimbia.
 
Alitake safe option mkuu, watu waliuliwa karibu 20,000 angesalimika yeye?
Wasingemgusa na Uingereza walikuwa washirika wake hadi leo anaishi Portsmouth akijulikana ,his majesty sultan of Zanzibar.Woga na utoto vilimponza,mkuu
 
Wasingemgusa na Uingereza walikuwa washirika wake hadi leo anaishi Portsmouth akijulikana ,his majesty sultan of Zanzibar.Woga na utoto vilimponza,mkuu

Mkuu inaoneknwa bado hujakagua vizuri nyaraka zinazohusiana na mapinduzi ya Zanzibar. Sultan hakukurupuka kukimbia aliondoka baada kuamuriwa afanye hivyo na serekali ya kingereza na Nyerere ndie aliemuhifadhi baada ya kuondoka Zanzibar kwa amri ya Serekeli ya Uingereza.

Yale mapinduzi hayakumlenga yeye lakini lazima yangelimuathiri na ndio mana alitolewa kafara. Usultan ulikua ni mtiifu kwa serekali ya Uingereza lakini vyama vilivyokua vikiongoza serekali ZNP/ZPPP havikua na mafahamiano mazuri na serekali ya Uingereza.
 
Labda tukiangalia angle ya ASP ,ingekuwaje kama Uhuru wa 9/12/1963,ungelikabidhiwa kwake,ingekuwaje upande wa sultan.Maana vyama vyote vikimtambua kama mkuu wa nchi ya Zanzibar.
 
Labda tukiangalia angle ya ASP ,ingekuwaje kama Uhuru wa 9/12/1963,ungelikabidhiwa kwake,ingekuwaje upande wa sultan.Maana vyama vyote vikimtambua kama mkuu wa nchi ya Zanzibar.

Wametawala nchi kwa miaka 20 bila ya uwepo katiba
Wametawala kwa miaka 20 bila ya kuwepo baraza la kutunga sheria.
Walifuta vyama vingi.
Waliua watu wasiopungua 20,000 katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya mapinduzi.
Waliungnaisha nchi na Tanganyika bila ya kufuata taratibu zinazotakilikana.

Haya yote wasingeliweza kuyafanya kama wangepata serekali kwa njia za uchaguzi

hawa watu hawakuwa watu wakawaida, CHIZI ALIPEWA RUNGU unauelewa huo msemo? Hawakuwa wanasiasa bali walikua ni wahuni tu yani Karume na kundi lake la wahani, hao wanasiasa wa ASP wenyewe wengi waliishia vifungoni na wengine kuuliwa. (Hanga, Sadalla, Twala, Mdungi Ussi, Ringo, Othman Sharif, Msigwa na wengineo)

Na kwa kukuridhisha tu ndani ya usiku ule ule wa mapinduzi group kubwa la wapiganji wa ASP walitaka kwenda kumvamia mfalme wamuuue, Mapambano yalikua makubwa sana kati yao na Polisi mpaka Polisi walipofanikiwa kumuondosha Mfalme.
 
Nikupongeze kwa kuwa shahidi wa mengi nikiyoyasoma kuhusu Zanzibar.Naomba kujua mengi zaidi hasa kumhusu Babake Abdalah Majura,gereza la kwa Mandera aka kwa baMkwe.Huwa nina hisia kwamba waingereza walikuwa na mpango na Nyerere kuhusu Zanzibar maana haiwezekani wasiweke mkataba wa kiulinzi na Zanzibar baada ya kuikabidhi Uhuru wake.Hivi ,the gang of 14 walipatikanaje?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…