Historia ya Kihima Ujiji na asili ya Waha

Historia ya Kihima Ujiji na asili ya Waha

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
2,101
Reaction score
3,866
HISTORIA YA KIGOMA UJIJI NA ASILI YA KABILA LA WAHA

Wakati miji mingine ikipata majina kutokana na ujio wa wageni, kuna baadhi ya miji ilipata majina yake kutokana na Waafrika wenyewe. Na kutaja majina kutokana na wenyeji kulitegemea sana watu, hasa wale waliokuwa maarufu kwenye jami. Na ile miji iliyopata majina kutokana na wageni, sababu ilikuwa ni kujiwekea sifa kwa mataifa hayo na wakati mwingine mitazamo tu ya wageni hao ilisababisha mji fulani kupata jina.

Kihistoria miji hii ilipata majina kutokana na watu maarufu waliopata kuishi na kujiwekea historia katikia miji hiyo.

Ifahamike tu kwamba kabla ya mji wa Kigoma kuitwa Kigoma palikuwa panaitwa "Lusambo Gwa Nyange" na Ujiji palikuwa panaitwa "Ubujiji.

Inaelezwa kuwa eneo la Ujiji kulikuwa na watu waliojiita WAJIJI (kabila) ambapo eneo hilo la Wajiji waha walikuwa wanapaita "Ubujiji" kulingana na lugha ya kikabila.

Na wengi walikuwa wanapenda kwenda Ubujiji na kujikuta wakijazana kwenye mji huo. Na hata waarabu walipofika hapo Na kwa kuwa wakati huo Waarabu hawakuwa na nguvu sana hawakutaka kubadilisha jina hilo na badala yake waliamua kuendeleza mji huo wa Wajiji na jina hilo.

Na hata mpaka ukoloni ukianzishwa bado eneo hilo lilikuwa na jina hilo, isipokuwa kukawa na mabadiliko katika kiothografia na matamshi ya neno Ubujiji.

Na hapo ndipo tukapata jina "Ujiji.
Na hata kwenye maandiko ya wakati huo ulitambulisha mji huo kama Ujiji.

Kwa upande wa jina la Kigoma pia mambo yalikuwa hivyo, sema kwa upande wa Kigoma, mji ulipata kukua kutokana na ujio wa (Wagoma) katika mji wa BUGOYE.
Ikumbukwe kuwa Kabla ya kuitwa Kigoma palikuwa panaitwa BUGOYE, Wagoma ni moja ya kabila la kimanyema waliokuja tanganyika Miaka ya 700 Na sultani wao wagoma alikuwa akiitwa (Sultan Simba) na Eneo walilofikia Wagoma ni eneo la SHEDE - BANGWE
Na mara baada ya Wagoma hao kuishi hapo kwa Muda mrefu Na kuanza kuujenga mji (Mjini) ndipo wageni (wakoloni) waliupa mji huo jina kutoka kuwa BUGOYE na kuwa KIGOMA kwakuwa hao watu walioishi hapo walijita "Sisi ni wagoma" Na ile sehemu aliyokuwa akikaa bwana Bugoye palifahamika kwa jina la Ibugoye ambapo kwa sasa ndio pale (Mwanga) Lakini Kiuhalisia Wagoma walifikia Maeneo ya BANGWE.

Na kwa kuwa ardhi ya Ujiji ilikuwa yenye rutuba, Wagoma walipenda kulima maeneo ya Ujiji. Kwa hiyo mji wa Kigoma na Ujiji ni miji ambayo ilijipatia historia ya pekee barani Afrika, kwani miji hiyo imepata majina yenye asili yake hapa hapa Afrika.

Ikumbukwe kwamba wagoma ni Kabila La wamanyema... Kwasababu Wamanyema ni Mkusanyiko wa makabila zaidi ya 18 yaliyoungana na kuwa kitu kimoja.

Pia wamanyema walipofika Eneo hilo Kuna ambao walipata majina katika miji kama Katonga, Kabwe, Mkabogo au Kabogo hao wote walikuwa ni wamanyema wenye asili ya DRC (Lakini ikumbukwe kwamba Wamanyema Kiasili kabisa ni watu kutoka SUDAN (koo zao zilikwenda zinahama hama mpaka DRC na Tanganyika, DRC ilikuwa ni njia lakini si asili yao)

Pia Waha Inasemekana walijikita sana kwenye Kilimo na ndio chanzo cha wao kuishi mbali na eneo hilo la BUGOYE (Kigoma na ujiji) Ispokuwa Waha walifahamiana na Wamanyema kutokana na ujio wa wamanyema eneo hilo. Lakini kiuhalisia Waha walijikita kwenye kilimo na Wagoma walijikita kwenye Uvuvi na ndio maana makazi yao yalikuwa mbali mbali.

.................
Asili ya kabila la Waha.

Historia ya waha ilianzia katika kijiji kiitwacho "Buha" kilichopo "Heru" hapo ndipo waha walipofikia baada ya kutoka maeneo ya "Burundi, Rwanda na Kongo" Asili ya Waha ni watu kutoka Burundi, Rwanda na Kongo, kama ilivyo kwa wamanyema asili yao ni Sudan na Kongo.

Inafahamika kuwa waha au kabila la "Ha" ni moja ya kabila kutoka Wabantu wa mashariki. Wabantu hawa walipata kufika maeneo hayo hata kabla ya miaka ya 600 yaani kabla ya wamanyema.

Na ifahamike kuwa asilimia kubwa ya makabila mengi yaliyopo hapa Afrika yalipata majina kulingana na wageni walivyoelewa au walivyoona.
Na kuna makabila yalipata majina kutokana na namna wanavyopigana, yapo makabila yaliopata majina namna wanavyopiga makelele na wengine walipewa majina kulingana na lugha yao au matamshi yao. Kwa upande wa kabila la Waha ambao wengi tunafahamu kuwa wanapatikana katika mkoa wa Kigoma.

Ukweli ni kwamba kabila hili ni miongoni mwa kabila ambalo lina historia kubwa sana tangu walipofika katika ardhi hiyo na pia ni kablia lenye umaarufu mkubwa hapa nchini..

Kipindi watu hawa wanafika maeneo ya Afrika mashariki hawakujulikana kama kabila la (Ha) na hawakuja wakiwa na kundi moja. Bali walikuja kwa mtindo wa Koo au ukoo. Na kila ukoo ulikuwa na jina lake.

Ukoo au koo zilizokuwa hapo zilipata kumiliki ardhi. Na cha msingi ni kwamba watu hao walifanikiwa kuitwa majina ya maeneo waliyokaa kutokana na mazingira yake. Kwa mfano kuna ukoo uliokaa sehemu zenye u"ngo (Bayungu) walijiita "Wayungu" na wale waliokaa sehemu za mwinuko (Heru) walijiita "Wanyaheru." Lakini mpaka kufikia miaka ya 1800, koo hizo ziliungana na kuishi sehemu na kutawaliwa na chifu mmoja.

Na hapo ndipo watu hao walianza kupata jina moja lililowatambulisha kwa wageni.

Sasa kwa nini watu hao waliitwa Waha?

Hii ndiyo mitazamo iliyosimulia asili ya neno "Waha au Ha"

1- Wapo waliodai kuwa asili ya neno Waha au Ha ni pale Wakoloni walipofika katika ardhi ya BUGOYE na kuwauliza watu hao kuwa “ ninyi ni wakina nani” na ndipo watu hao walipojibu “tur; Abhaha” wakimaanisha “ sisi ni watu wa hapa hapa. Na hapo wakoloni hao walikalili kuwa Waha kwa kuchukua neno “ha”,,,, Kiuhalisia waha na wamanyema ni Watu wamoja tangu enzi na enzi walipendana na kuthaminiana.

2-Wapo wanaodai kuwa wakolomi walipokuja na kukuta ufalme wa Buha umekuwa na ulikuwa na watu wengi, walimuuliza mfalme wao kuwa “hawa ni wakina nani” na ndio mfalme wa Buha alipojibu kuwa “N’abhaha” akimaanisha kuwa “ hawa ni wenyeji wa hapa hapa” na hapo wakoloni hao walipata neno“Ha” na walipoandika waliaandika hivyo.

Maelezo haya yalitolewa kwa mujibu wa watu walikuwa wamekutwa katika ardhi ya Buha. Kwa upande mwingine, historia inafafanua kuwa, Watusi walikuwa watawala wa kabila la Waha.

Na kuna mahususiano makubwa sana kati ya Watusi na Waha. Na hivyo hata neno Waha bado lilionekana kuhusiana na Watusi.

"Kwa Watusi neno Abaha lina maana ya mtu yeyote “anaowapa ardhi” na kwa Watusi aliyekuwa akitoa ardhi alifahamika kwa jina la Mteko. Na mteko alikuwa akitoa ardhi kwa Watusi, walifahamika kwa jina moja la Uwaha.

Na waliolima shamba moja na Mteko walijiita “Abhaha” na hata kuna baadhi ya Watusi hujiita “ Waha” na ndio maana hata walivyotawala walijiita hivyo.

Wamanyema na Waha Ndio wenyeji wa kigoma. Uwenyeji huu tunauzungumza ni miaka ya zamani sana hata kabla ya kuanza kwa ukoloni hawa watu tayari walikuwa wakiishi pamoja... na walikuwa wakipendana na kuthaminiana na kuna vitu Waha waliwafundisha wamanyema na pia kuna vitu wamanyema waliwafundisha waha na wote hawa waliipigania Tanganyika Kutoka mikononi mwa serekali ya kikoloni. Kwa mfano "Iddi_Faiz ni mmanyema ambae hatuwezi kumsahau kwasababu yeye ndie aliyekuwa muweka hazina wa chama cha TANU "

-Hata kuligawa bara la Afrika Scramble For Africa ilikuwa bado kabisa wamanyema na waha walikuwa wakiishi pamoja .. na Ikumbukwe uhuru wa nchi hii hatuwezi kumsahau "Mwami Thereza Ntare" malkia wetu wa Kiha na chifu mwanamke wa kasulu ambae aliipigania nchi hii kutoka mikononi mwa wakoloni na likawa Taifa huru.

" Heshima imfikie Kila mwana Kigoma Popote Alipo"

#Share ili wengine pia wajifunze.


©Mhe. Stellah Manyanya
 
Back
Top Bottom