Historia ya kaburi la Iringa lililogoma kuhama

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
297
306
Kaburi la Mzee Martin Kiyeyeu aliyefariki mwaka 1974, kama linavyoonekana katika picha kando ya barabara ya Iringa-Mbeya

Uliwahi kusikia maajabu ya Kaburi hili la mtu maarufu katika fani ya waganga wa jadi Almaarufu Kiyeyeu?

Kaburi la Kiyeyeu, lipo Njiapanda ya Mlolo pembezoni kabisa mwa barabara iendayo Mkoani Mbeya ukitokea Iringa lipo upande wako wa kulia, katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Hili ni kaburi alilozikwa mtu mmoja aliyekuwa Mganga maarufu wa jadi katika ukanda mzima wa maeneo ya mkoa huo, ambaye alifariki dunia miaka ya nyuma kidogo lakini hadi leo hii kaburi hilo ukiliona ni kama limejengwa jana.

Ukiangalia kwa makini picha hii utaweza kuona jinsi nyaya za umeme wa Tanesco zilivyokwepa kaburi la Martin Kiyeyeu

Baada ya kufariki dunia mganga huyu, alizikwa kwa kufuata taratibu na mira za Machifu ambapo alizikwa kwa kusindikizwa na mtu aliye hai, aliyejitolea kwa ajili ya kuzikwa naye akiwa hai ili kumsindikiza, ambapo inadaiwa mtu huyo aliketi na kumpakata mganga huyo aliyezikwa huku akiwa amekaa.

Kaburi hilo limekuwa liwashangaza watu waliowengi na hata ndugu wa marehemu huyo kutokana na kuwa na maajabu na miujiza isiyoisha kana kwamba mtu huyo amezikwa mahala hapo jana.

Moja kati ya maajabu makubwa yaliyowahi kutokea mahala lilipo kaburi hilo ni wakati Shirika la umeme lilipokuwa katika zoezi la kuweka Nguzo za umeme pembezoni mwa barabara hiyo na kutokana na kaburi hilo kuwa karibu kabisa na barabara kubwa. Ndipo ilipoamuliwa kuweka nguzo hizo na kupitisha nyaya za umeme kiubishi.

Lakini baada ya kumaliza zoezi hilo walishangazwa kwa kuona kuwa eneo la juu ya kaburi hilo hapakuwa ukipita umeme hali ya kuwa ulipoanzia hadi kabla na baada ya kaburi hilo umeme umejaa tele, ila eneo la juu ya kaburi hilo tu hakuna umeme.

Jambo hilo liliwafanya Tanesco kukubali matokeo na kuamua kuchukua uamuzi wa busara kwa kuhamishia baadhi ya nguzo hizo upande wa pili wa barabara ili kukwepa eneo hilo, hivyo nyaya hizo zikavuka barabara kabla ya kufikia kaburi hilo.

Baada ya kulivuka kaburi hili, na baada ya kufanya hivyo ummeme huo uliwaka na hadi hii leo unaendelea kuwaka, hivyo Serikali japo haiamini uchawi lakini hapa iliamini uchawi upo.

Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling’oa.

Hata hivyo kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake baada ya mila na matambiko kufanyika.

IMG_20190713_183720_001.JPG
 
Huyo aliyempakata wakati wa kuzikwa amegeuka ni "mzimu" Ndiye anayeleta mauzauza yote hayo. Wamisri na Wajerumani walipotaka kufukia dhahabu na vito vya thamani walikuwa wanaweka watu hai hapo mali zinafukiwa halafu watu hao wakafukiwa na hizo mali wakiwa hai au wameuawa wakiambiwa "chunga hapa tutakuja baadaye" ndipo wanapigwa risasi. Ukijaribu kwenda kufukua hizo mali uzichukue utakutana na mambo ya ajabu. Hapa Tanzania kuna sehemu kama hizo na japo zinajulikana zilipo, hizo mali haziwezi kutolewa kirahisi. Maeneo ya Tanga kuna vitu kama hivyo. Mali zilifukiwa na Wajerumani (ambao wengine wao ni wachawi kupindukia) wakati wanatawala Tanzania
 
Sibishi ila ishu kama hizi nimekuwa nikisikia tu kama story toka utotoni natamani siku moja nishuhudie ili nijiridhishe.
 
Huyo aliyempakata wakati wa kuzikwa amegeuka ni "mzimu" Ndiye anayeleta mauzauza yote hayo. Wamisri na Wajerumani walipotaka kufukia dhahabu na vito vya thamani walikuwa wanaweka watu hai hapo mali zinafukiwa halafu watu hao wakafukiwa na hizo mali wakiwa hai au wameuawa wakiambiwa "chunga hapa tutakuja baadaye" ndipo wanapigwa risasi. Ukijaribu kwenda kufukua hizo mali uzichukue utakutana na mambo ya ajabu. Hapa Tanzania kuna sehemu kama hizo na japo zinajulikana zilipo, hizo mali haziwezi kutolewa kirahisi. Maeneo ya Tanga kuna vitu kama hivyo. Mali zilifukiwa na Wajerumani (ambao wengine wao ni wachawi kupindukia) wakati wanatawala Tanzania
kuna story niliwahi kuzisikia kuhusu wakoloni especially wajerumani na baadhi ya wamisionari.

inasemekana wakati walipokuwa wanazambaza ustaarabu na desturi zao kwa mababu zetu, walihakikisha wana document masuala yote yaliyohusu mila, matambiko, uchawi na dawa za mitishamba za waafrika na kwenda kufanyia tafiti huko kwao.

sio tu kwamba wazungu waliondoka na raw materials bali pia hata uchawi wa kiafrika waliondoka nao na wanautumia sana katika tafiti zao za kisayansi huko kwao huku sisi wakitumbia ni mila potofu zilizopitwa na wakati.
 
Huyo aliyempakata wakati wa kuzikwa amegeuka ni "mzimu" Ndiye anayeleta mauzauza yote hayo. Wamisri na Wajerumani walipotaka kufukia dhahabu na vito vya thamani walikuwa wanaweka watu hai hapo mali zinafukiwa halafu watu hao wakafukiwa na hizo mali wakiwa hai au wameuawa wakiambiwa "chunga hapa tutakuja baadaye" ndipo wanapigwa risasi. Ukijaribu kwenda kufukua hizo mali uzichukue utakutana na mambo ya ajabu. Hapa Tanzania kuna sehemu kama hizo na japo zinajulikana zilipo, hizo mali haziwezi kutolewa kirahisi. Maeneo ya Tanga kuna vitu kama hivyo. Mali zilifukiwa na Wajerumani (ambao wengine wao ni wachawi kupindukia) wakati wanatawala Tanzania

Mkuu hebu niambie au taja ni mahali gani huko Tanga wajerumani hadi leo wamezika hizo mali, I am serious.

Hatuwezi kulia umaskini ilhali kuna mali iliyozikwa/ iliyolala ardhini bure bure tu!!??. Tafadhali weka wazi ili sisi tusioogopa twende kuchukua hizo mali.
Sisi tunamuogopa Mungu tu katika suala hilo.
 
Back
Top Bottom