Historia ya CCM Njombe kufutika kabla ya 2014

Historia ya CCM Njombe kufutika kabla ya 2014

Mheshimiwa Lutondwe, heshima mbele!! Tunazo taarifa za kutosha za namna Mheshimiwa Nyimbo anavyotumia mali, muda na nguvu zake zote kukijenga CHADEMA kupitia mikutano ya wazi, nyumba za ibada na kupita nyumba kwa nyumba. Napenda kukubaliana na wewe kwa kumwita huyu bwana ni Kamanda. I wish uongozi wa CHADEMA taifa ungeielewa kazi nzuri inayofanya bwana Nyimbo kule Njombe.

Nataka nigeukie kwako Lutondwe, unatuhakikishiaje kwamba hivi sasa una mapenzi na CHADEMA na si ubunge? Kutoka na na historia yako, unaonekana kuwa ni mtu wa kutanga tanga unayeutaka ubunge kwa gharama yoyote bila kujali aina ya utumishi unaotaka kuutoa kwa wananchi wa Njombe hasa Njombe Kaskazini. Kumbuka tangu wakati huo ulipoanza na NCCR Mageuzi, baadaye CHADEMA, baadaye CCM na baadaye CHADEMA tena. Nataka kukuaminisha kwamba mwaka 2010, wananchi walikuwa tayari kuchagua upinzani, lakini hawakuwa na imani na wewe Lutondwe kutokana na kukosa msimamo. Na ni vema ukubali kwamba Njombe kaskazini mwaka jana ilikosa mwakilishi kutoka chama cha upinzani kwa ajili yako.

Bwana Lutondwe, ni vema ufike mahali fulani ukakubali kuwa mtumishi wa watu katika nafasi yoyote ambayo Mungu amekupa na si kuuangalia ubunge pekee. Jitoe kwa nguvu zote kama ambavyo Nyimbo anafanya sasa kuhakikisha unajenga kwanza chama (huo ni utumishi wenye heshima sana) kabla ya kufikiria huo ubunge ambao utakuwa ni matunda ya kazi nzuri mliyoifanya kwenye grassroot level.
 
huna imani kwanini? maana wana njombe wana mwamini ,sasa wewe unayeishi dsm humwamini kwa lipi?
:heh:
Kama wangemwamini wangemchagua 2010. Pale message waliyoituma wananchi kwa chadema na kwa Lutondwe ni kwamba hata CCM wangeweka jiwe lishindane na Nyagawa, bado wananchi wangechagua jiwe. Kura chache alizopata mwaka jana Nyagawa zilitoka kwa wananchi ambao wamekata tamaa na CCM na wako tayari kwa lolote lile ilimradi isiwe CCM. Mimi nilikuwa kwenye huo uchaguzi, na wananchi walikuwa wanasema wazi kabisa kwamba Lutondwe haaminiki.
 
baadaye sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa......Njombe ni CCM 100%...Nyimbo alikuwa mbunge kwa miaka 10 bila kuleta maendeleo yoyote zaidi ya matusi na dharau kwa utajiri wa KIFISADI na madawa ya kulevya .Leo hii anawadanganya wananjombe anataka kuleta maendeleo? maendeleo yapi aliyoshindwa kufanya enzi za UBUNGE? huyu hana utofauti na Jambazi kuvaa joho na biblia mkononi ili apate mwanya wakuhujumu uchumi.....NJOMBE haidanganyiki tena,labda NYIMBO asiwepo kwenye CHAMA hicho.
You are not serious man. Sidhani kama Nyimbo analinganishwa na mbunge mwingine yeyote aliyewahi kuongoza Njombe katika suala zima la utendaji. Utamlinganisha Nyimbo na Makweta, Makinda, Kaduma, Yono, au Ngunangwa? Sijamwona mbunge wa Njombe ambaye yuko serious kama Nyimbo.
 
Huyu jamaa aliwahi kumdondosha Makweta kwenye uchaguzi halafu jamaa wakampa hela akakubali kushindwa while ameshinda. Imani inabakia kwenye kujenga chama ila kugombea ubunge imani na Lutondwe imetoweka kabisa. Big up nyimbo, mkoa mpya chama kipya na itikadi mpya. Viva CDM

umehadithiwa ama una uhakika?kama kitu hukijui kwa nini usikae kimya? uchaguzi gani ambao lutondwe alimshinda makweta? UNAFIKI MBAYAAAAAAAAA.huyu ndo katibu wetu wa wilaya ya njombe cdm na ndo kaimu katibu wa cdm wa mkoa mpya wa njombe kama humtaki andamana,
 
Kama wangemwamini wangemchagua 2010. Pale message waliyoituma wananchi kwa chadema na kwa Lutondwe ni kwamba hata CCM wangeweka jiwe lishindane na Nyagawa, bado wananchi wangechagua jiwe. Kura chache alizopata mwaka jana Nyagawa zilitoka kwa wananchi ambao wamekata tamaa na CCM na wako tayari kwa lolote lile ilimradi isiwe CCM. Mimi nilikuwa kwenye huo uchaguzi, na wananchi walikuwa wanasema wazi kabisa kwamba Lutondwe haaminiki.
acheni unafiki wenu,mbona hadi dakika za mwisho hamkujitokeza kugombea kama nyie mnafaa? mlitaka cdm njombe kaskazini ikose kabisa mtu wa kusimama kama walivyofanya njombe kusini? kwa nini msimpongeze kwa yale mazuri anayoyafanya hadi sasa kwenye chama nyie mmeng,ang,ania mambo ya 2010 ambayo hayawezi kusaidia kitu chochote,shughuli za chama zenyewe hamfanyi mmekaznia umbea bila kuwajibika kwenye chama,mnadhani cdm itajijenga bila kujitoa muda,fedha na raslimali zingine?tuulizeni tunaofanya naye kazi za chama kama hatufai ama vipi
 
Daaah katika watu ninaowapitisa kipapinduzi Thomas Nyimbo hakosekani. Niliwahi tembelea katika ngome yake nikiwa ktika shughuli zangu za kikazi nikaambiwa ili tatizo liweze kutatuliwa kwa haraka jimboni hapo ni mpaka limfikie Kamanda Nyimbo nafurahi kusikia bado anapambana
 
Tuache malumbano wakuu,tutizame namna stahiki ya kujenga chama na si kwa kuoneshana vidole machoni,wanacdm ni watu makini,wasio na woga na ukweli ni kwamba kazi inayofanyika na viongozi wa cdm mkoa mpya wa njombe,kuanzia ngazi ya shina wanastahili pongezi za dhati,ujenzi wa chama kisicho na rasilimali si jambo jepesi ila makamanda wanajitoa kwa hali na mali ili kujenga chama,wanapambana katka mazingira magum ili kufikia malengo na kwa kweli nawapongeza sana kwa moyo wao wa kizalendo.mzee nyimbo kama mlezi wa chama mkoa mpya anafanya hata zaidi ya kawaida na kiukweli sioni sababu kwa watu kubeza kazi yake kwa chama.viva cdm na kwa nguvu ya umma tutavuka vihunzi vyote.
 
Kamanda mkuu wa jeshi la CHADEMA mkoa mpya wa Njombe akishirikiana na kamanda Nyagawa(Lutondwe).Amedhamiria kuhakikisha ifikapo 2014 jina la CCM linabaki historia katika mkoa mpya wa Njombe.Kamanda huyo ambaye anafanya kazi ya kueneza chama usiku na mchana katika mkoa mpya wa Njombe tayari amefungua zaidi ya matawi 180 ndani ya mwaka mmoja na anatarajia kuendelea kufungua matawa katika kata zote za mkoa huo.Jumamosi na jumapili ya tarehe 14.4.2012 na 15.4.2012 ataongoza kikosi cha maangamizi katika tarafa ya Lupembe,eneo ambalo linaongozwa na mbunge aliyeandika historia ya kuingia bungeni kwa elimu ya K.K.K.
Mikutano ya mwishoni mwa wiki itaanza katika kijiji cha Madeke mpakani na Morogoro,Mfiriga na Igombola.Siku ya jumapili ya tarehe 15 atakuwa Lupembe barazani na Matembwe.
Kwa kuwa ni wakati mwafaka wa kuleta mabadiliko katika nchi yetu,mheshimiwa Nyimbo anawaomba wazalendo wote duniani kute kujitokeza ili kuleta ukombozi wa kweli na uhuru wa kweli.

Kazi kama hii inatakiwa kufanywa nchi nzima. Tahadhari hayo matawi yasiwe vingenge vya wahuni ambao, na wavivu vijijini wakafanya chama makini CDM kuonekana ni chama la kihuni
 
kiukweli kazi inayofanywa na MH.NYIMBO NA lutondwe si ya kubeza,cdm mkoa wa njombe kwa sasa ina nguvu sana tofauti na miaka ya nyuma .ukiangalia wote wanaobeza si makamanda wa cdm lazima watakuwa wanatumika na ccm ili kuibomoa nguvu ya cdm ambayo imekuwa tishio kwa ccm mara tu baada ya uchaguzi,tazama tulikuwa hatuna tawi hata moja majimbo yote matatu ya wilaya ya njombe lkn sasa tuna matawi zaidi ya 200 wilaya nzima ,sasa mlitaka hawa makamnda wakae kimya ndo mngefurahi.mshindwe na mlegee
 
Bongo hakuna siasa za siri labda zile za CCM tu. Sheria na taratibu zinavitaka vyama vya siasa vikifanya mikutano ya wazi vitoe taarifa kwa uongozi wa eneo husika. Mikutano ya hadhara haina siri maana ni zama za kuwaamsha wananchi na kuwaonyesha kwamba pia kuna vyama vingine vina exist.

Strategy za siri haziwezi kufanya kazi kwa chama ambacho hakina mtandao, wanaoendesha strategy za siri mara nyingi huwatumia mabalozi na wanachama wake kwa kuendesha mikutano ya ndani. Huko Njombe CHADEMA haina wanachama wengi wa kufanya mikutano ya ndani, ndio kwanza wanafanya kazi ya ku-recruit wanachama, kufungua matawi na kusimika viongozi wa maeneo husika.

umesomeka.
 
Big up sana tulipamwinga ndiwandza nayune ya ndiwima ihibalula mlungu gumwinga nditange padebe hukaya. Im happy for the Gud news PeopleZzzzzzzzzzzzzzzzzzz ..........
 
Back
Top Bottom