Historia inasema CIA walikuwa wakiondoa viongozi madikteta na waliweka viongozi wa kidemokrasia, zama hizi wanashindwa wapi?!

Mfalme ni kama nembo ya taifa na si Mtendaji ni sawa na sisi tuwe na baba wa taifa.Hizo nchi zinaongwa na katiba haziongozwi na mawazo ya MTU mmoja ( udikteta).
 
Kwa taarifa ni bora kinachoendelea kuliko alichokuwa akiwafanyia. Usitake kutishia watu.
Wengi walimjua Gaddafi Kwa nje,sawa na nje wamjuavo jiwe Kwa nje.Gaddafi alimsaidia IDD amin, alikuwa mfadhili wa kundi La kigaidi La seleka na watuarag.Aliiendesha Libya Kwa mkono wa chuma sawa na kumchapa mtoto kisha unampa pipi na chocolate anyamaze.
 

U
Umenena vyema ni hadi pale tu maslai yao yatakapokuwa mashakani.KAGAME na M7 kudumu kwao mda mrefu si kwamba wako vizuri kwenye intelligence au wanawadhibiti wapinzani, ni Kwa sababu wanajua kula na kipofu wanacheza kote Lkn hawagusi maslai ya mabeberu awachezei sharubu za beberu wanapora Congo wanamuuzia beberu,beberu anawapa silaha, misaada na pesa za kujiimarisha.Hapo beberu ajali kuumia kwako thus anaalikwa mikutano ya kimataifa. Sasa naona students yeye anaingia kichwa kichwa kuchezea sharubu za beberu,beberu wana njia nyingi sana za kuwatoa wasiowataka na kila jamii ina njia zake nchi zenye nafuu kiuchumi kutumia njia za vikwazo hakuleti ticha ya haraka, njia sahihi ni kukuundia vikosi vidogovidogo na kuvipa silaha tumeona Libya,Iraq, Syria, Yemen, nk vikizidiwa nguvu wanaingia kupitia UN Kwa gia ya kuwalinda RAIA hapo utapigwa no free fly zone yaani anga yako inafungwa kifuatacho ni kipigo cha mbwa koko ardhini na angani,ukijifanya nebukadineza lzm wachomoe betri Salama ukimbilie uhamishoni.Wao watajilipa kupitia Mali ulizonazo kama ni mafuta gesi au madini yaani kuondolewa kwani madarakani utakugharamia mwenye we.Kwa nchi masikini zenye maslai makubwa kwao utawekewa vikwazo ili maisha yawe magumu maisha yakiwa magumu wananchi wako wataungana kuimba wimbo mmoja na vyombo vya dola hawa askari wa chini Maana dukani mwaenda wote wa juu ni wanufaika wa udikteta, wanalinda maslai ya dikteta,ila hali huwa ni wafata upepo wanapima nguvu ya wananchi ikiwa kubwa wakuu wa vyombo vya ulinzi huwa wanamgeuka dikteta anabaki mwenyewe aamini macho yake tumeona Libya, Egypt, sudani,Zimbabwe, nk wakuu wa vyombo vya ulinzi ni wafata na wapima upepo wanapima joto ili wasitengwe na jumuiya za kimataifa.
Hivo CIA wakati mwingine hawahitaji kutumia nguvu kumfurusha dikteta.
 
Hivyo siyo kwamba walifanya kusaidia kuweka demokrasia, kuondoa vigenge vya watawala wachache na kusaidia kusimikia viongozi wa wengi?! Maana nchi zetu hizi zimebadirisha kabisa maana ya neno demokrasia, wamejikinga nyuma ya majeshi badala kuwekwa na wananchi.
 
Ushauri kwako, kajielimishe zaidi kuhusu hili. Wamarekani kupitia hao CIA kamwe, hawafanyi “regime changes” kukusaidia wewe bali kujisaidia wao. Sasa wewe baki hapo ukisubiri.
Hivyo unasema watawala hawa wa nchi zetu wanatimiza masharti ya wamarekani na CIA, na wanapokandamiza na kunyima demokrasia wananchi wake haiwasumbui wamarekani na hata CIA kwasababu interest zao wanazitekeleza.
 
Usipende kutamani ubeberu ukijiinua Africa ndugu,tengeneza tafakuri za watu weusi na bara letu,achana na makaburu hayo

Black man redemption
Watawala hawa wamenifanya nitamani ubeberu, maana beberu wanatoa haki. Hawa watawala weusi wameumiza wananchi wao muda mrefu sasa, mahakama za watawala, majeshi ya watawala, fedha za watawala, miradi ya nchi ya watawala. Hawa wananchi wao wamebaki na nini?!
 
Kuna mchangiaji jaelezea hili vizuri sana, usipoelewa jiote humu jf. Nisawa na mwanafunzi kuhudhuria lecture na haelewi chochote, bora kubaki nyumbani.
 
Sisi wala viazi na kuku tumeshadhibitiwa na majeshi yetu wenyewe, maana yamegeuka kuwa kampuni za ulinzi wa watawala hivyokukosa namna ya kufurukuta, mahakama zao na hutenda kwa maslahi yao maana judges huteuliwa na wao, hulipwa na wao sisi hatuna uwezo kujitetea ndio tunaomba hao handsome CIA waje wasaidie kutuondolea hawa watawala na watusaidie kutuwekea viongozi tutakao wachagua, maana ilivyo sasa hatuchagui bali watawala huteua na kupitisha wawatakao wao kutekeleza maslahi yao.
Hawa wanawake wapo wengi huyo handsome akichukua nitachukua mwingine, kama panya wanasumbua ndani na handsome anaweza kusaidia kuwatoa chumbani mimi tipwatipwa sioni shida kabisa kumruhusu aingie huko chumbani hata akihakia huko mimi nita tafuta palipo salama bila panya.
 
Ina maana mpaka sasa hujui azma ya unafiki wa wazungu? Umeishia darasa la ngapi mkuu
Bahati mbaya sikufundishwa unafiki huo huusemao wewe uajua vitabu vyetu walitunga wazungu nikasoma shule za kuzungu na walimu wazungu.
Nimekuta nonewa na weusi watawala na magenge yao wakati hao wazungu walinipenda walinipa elimu nzuri na bure.
 
Ungetumia lugha ya SADC wasomaji wa ukanda huu waelewe pia, hatujui umeunga mkono hoja au rumspringa. Ila tumekupigia makofi maana ndio utamaduni huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…