Historia inasema CIA walikuwa wakiondoa viongozi madikteta na waliweka viongozi wa kidemokrasia, zama hizi wanashindwa wapi?!

Unawazungumzia CIA waliopigwa na Russia kwenye uchaguzi wao au wapi hao??
 
Project yao ilikuwa ni kuufuta mfumo wa ki-dictator wa kicomunist, na kuweka mfumo wa kidemocrasia ya kibepari, nami naungana nao mfumo wa kijamaa ni wa ki-dictator na unachochea umasikini

Mkuu unaisema nchi yetu?
 
Uzi wako ni wa uongo 100% mkuu.CIA wanaondoa viongozi wanaotawala kwa maslahi ya watu wao na kushirikiana na wale ambao wanashirikiana nao katika uporaji wa rasimali za watu wao.Kama wangekuwa wanajali democrasia kamwe wasingeshirikiana na Saudi Arabia wala Bahrain.Wamarekani wanachojali ni pesa,utu and the so called democracy is nothing to them.Ni danganya toto tu mkuu.
Asante, kwa ukweli wako. Hivyo yeyote anayeshirikiana na hizo nchi ulizotaja hajali utu wala demokrasia?!
 
Kanuni Moja ya muhimu Sana Kwenye ubepari ni kwamba bepari huwa Hatoi hata Shilingi kumi ambayo hajui itarudi vipi.
Ukiona ametengeneza mgogoro halafu ameanza kuusolve ujue kuna maslahi yake.
Tazama yanayoendelea Israel na Saudis utaelewa kwamba masuala ya demokrasia ni hoja za kitoto Kabisa.
Hata uwe dikteta Vipi Kama unalinda maslahi yao dhidi ya maslahi ya nchi yako wewe ni rafiki yao.
Wao wana maslahi ya kudumu Hawana urafiki Wa kudumu.
Kiongozi wa nchi anayeingia mikataba ya hovyo na makampuni yao Huyo ni bora kabisa hata wananchi mgaragazwe vipi haina Shida Ila viongozi wanaotaka kuendeleza nchi zao na kuukataa ukoloni mamboleo uliowekwa mbadala ya ukoloni wakishamba wazamani watapata Tabu Sana.
JK alipata tuzo nyingi na kusifiwa kwasababu Moja tu aliwaacha wale watakavyo na aliishi kwa misaada yao akinyenyekea daima.
Huyu wasasa JPM atapata Tabu sana kwasababu Anahoja ya kujitegemea na kujitegemea sio lelemama Lazima ukusanye kodi na wananchi wahenyeke na huku inajulikana uvivu Wa Waafrika achilia Mbali kipaji cha majungu na umbea.
Tukiachwa ipo siku tutaendelea na tutasumbua Latima hao CIA watatuwekea speed gavana.
 
Lakini maslahi yao kuondoa utawala wa mtu na kuweka uongozi wa wengi ni faida kwa wananchi kuliko labda hata maslahi yao kisiasa au kiuchumi, nchi hizi za kiafrika watawala wamezidi kuonea raia wengi wenye nchi wakilinda maslahi yao wachache, binafsi ningeomba CIA wasaidie kuondoa watawala wachache na wasaidie kusimika viongozi wa wengi kwa maslahi ya nchi zetu hizi.
We jamaa una kichwa kigumu sana, CIA ipo kwa ajili ya marekani hata wakimuweka huyo unayesema kiongozi wa wengi kama baadae ataenda tofauti nao nasi watamtoa tu! Yaan hawajali raisi awe dikteta au mwanademokrasia, wanachojali maslahi yao na marekani! Yaani uende nao sawa
 
Mnisaidie tafakuri hii, zama hizi hawa CIA, wanashindwa wapi, vipi na kwanini wamekuwa tofauti na huko miaka ya nyuma, tulisoma jinsi walivyokuwa wakiondoa makandokando nchi zetu hizi, juzi juzi walifanikiwa Iraq, na hata Libya, lakini Syria wanaelekea kukwama, huku kusini mwa jangwa la sahara ni kama hawajishughulishi kabisa, au hivi vilio vyetu havisikiki au havijawafikia au vimepuuzwa.

Kwanini wasifundishe vijana wa nchi hizi mbinu za kutekeleza hazima hizo wenyewe bila wao kushiriki ikiwa hawataki kuhusika au kuhusishwa.

Nchi zetu hizi sio priority zao, kwanini wamekuwa wakikosoa bila kutoa solution, binafsi ningependa hata watoe mafunzo yale kwa wazawa kuliko kuangalia mambo kwa mbali bila kusaidia kutatua.

Waliua madikteta nini kimewasibu, hadi kutokutekeleza haya tena?!
Mkuu unataka kumlenga
Ngoja uone matusi ya Buku 7 FC
 
Nani alikuwambia CIA wanataka viongozi waliochaguliwa kidemokrasia ?
1. Mobutu CIA project baada ya kumuua Patrick Lumumba
2. Sadam hussein CIA PROJECT
3. Fidel Marcos CIA Project
4. Charles Taylor CIA Project
5. Shah wa Iran CIA Project
6. Mwaka 1973 CIA walimuua Rais Allende wa Chile aliyechaguliwa kidemokrasia na kumweka dikteta Pinochet
Hao ni.baadhi tu
Sina cha kuongeza. Nilikuwa nimepanga kumpa elimu kama hii lakini umemaliza. CIA wapo kwa maslahi ya Marekani sio kwa maslahi ya watu wa Taifa lingine lolote. Labda kidogo UK kutokana na urafiki wa muda mrefu na historia yenyewe kwamba wengi wao wanatokea UK. mleta uzi go and re-do your assigment.
 
CIA gani hao waliweka viongozi wa kidemokrasia?? Hivi unajua raisi wa USA aliwahi kuomba msamaha kwa kilichotokea kwa Guetamala? Sina hakika kama unaijua Guetamala
2016 Obama aliomba radhi kwa walichokifanya Libya, na wanajutia kwa uamuzi ule wa kumuondoa Gadaffi
Karibu

Kumuondoa Ghadafi kumekuwa ni kilio Kwa ulaya sababu ya mzigo wa kuhudumia wakimbizi. Matumizi ya nguvu hayajawahi leta utumbuzi.Unamuondoa kiongozi madarakani kisa nchi haikaliki unaanza kuingia gharama kuhudumia wakimbizi tena.
 
Kumbe watu wa aina mpo?!.
Yaani tuletewe vibaraka?!.
Wazalendo wa kweli wa taifa hili, tutakubali?.

P
Hatutaki vibaraka. Tumeshawashinda 2015; Ndio ulikuwa mwaka wa ushindi. Our minds have been opened now. We will be be implanting our leaders especially presidents. Tutapandikiza wenyewe, sio kusubiri kupandikiziwa.
 
Uko sahihi, je kinachoendelea sasa hivi ndani ya box la kura kwenye nchi yetu unaweza kusema viongozi wanapatikana kidemokrasia?
Demokrasia ni swala la kipropaganda. Maswala halisi ya nchi sio propaganda. Demokrasia ni mchezo wa danganya toto. Ililetwa kutufunika macho ili ipatikane gap ya kupangiwa viongozi. Mataifa makini huandaa na kupanga vongozi wao kwa ndani kabisa. Kinachosemwa mkuu sicho kinachotokea au kufanyika katika hali halisi.
 
Kuna mtu nimemjibu hapo juu, kama huna sababu ya kugombana na hawa watu ni bora ukajikalia kimya na kuendelea kuongoza kwa hekima na busara kuliko kupiga mayoye na kuleta athari kwa jamii yako..

Mchina juzi hapa kajaribu kunyanyua mdomo fimbo aliyochapwa nayo naona kaanza kwenda kwa hekima na busara maana amesahau Taiwan na Hongkong ni fimbo rahisi ya kumchapia..
Ushauri wako ni mzuri.
 
Lakini demokrasia zetu hizi sijui nikueleze vipi, yani hata tume kumtangaza mtu kwa shinikizo la kisiasa na uoga kupoteza vyeo vyao kwasababu wanao wateua ndio hutakiwa kuwatangaza, na watawala kutumia majeshi ya ulinzi kana zana zao binafsi za kujitwalia maharaja, wakitumia majeshi kutesa au kupoteza wapinzani wao sisi huku tunaita hiyo nayo demokrasia.

Mao wa China ndie msingi wa mfumo wa udikteta Africa wao walicopy na kupaste,vyombo vya dola kulinda maslai ya mtawala badala ya kulinda maslai ya taifa.Furaha ya dikteta yeyeto ni kutawala masikini wanaitwa wanyonge kama lugha ya kuwa pamba.Adui MKubwa wa dikteta ni Msomi na tajiri sababu hawataki mawazo mbadala,mawazo yao ndio Sheria, ni heri umkosoe Mungu huko Salama Kwa dikteta lzm uliwe kichwa Kwa risasi,kutekwa, kuteswa, kuuwawa, kubambikiwa kesi za uhaini,uhujumu uchumi na wapambe wa dikteta watumikao kama loudspeaker na kondomu wakienda kinyume kupinga maagizo ukiona cha mtema kuni.Wote ni mateka wa hiari,dikteta ashiki bunduki Maana ni dhaifu ila mdomo wake ndio bunduki akisema wasaliti wanafanywaje jibu upatikana.Mao wa China na Kim wa north Korea uabudiwa kama mungu.China ndie mfadhili mkuu na rafiki wa Madikteta yote Africa Kwa mabadilishano ya fedha na utajiri wa Africa. Vyombo vyote vya dola viko Kulinda maslai ya watawala na magenge yao vikitumika kuwashugulikia wapinzani usiku na mchana.
Hivo ni sahihi Kwa jumuiya za kimataifa kuyafurusha Madikteta ili kuepusha gharama za kuhudumia wakimbizi na kukoa pesa zitumike kwenye masuala mengine.Wawezacho Madikteta ni kuzalisha wakimbizi na sio kuhudumia wakimbizi. Sababu ya utapiamlo wa malezi bora utotoni toka Kwa masingo mother au wazazi wasio na maadili ndipo upatikana zao LA udikteta ambapo mtoto ugeuka laana Kwa anaowaongoza na si Baraka. Furaha yake ni kuwaumiza wengine vilio vya wengi ni burudani sawa na sauti nzuri masikioni mwa Madikteta.
 
Demokrasia ni swala la kipropaganda. Maswala halisi ya nchi sio propaganda. Demokrasia ni mchezo wa danganya toto. Ililetwa kutufunika macho ili ipatikane gap ya kupangiwa viongozi. Mataifa makini huandaa na kupanga vongozi wao kwa ndani kabisa. Kinachosemwa mkuu sicho kinachotokea au kufanyika katika hali halisi.

Mbona demokrasia ulaya imefanya matokeo Mazuri
 
Mbona demokrasia ulaya imefanya matokeo Mazuri
Nchi gani Ulaya kuna demokrasia tunayohubiriwa Africa? UK, Belgium, Netherlands, Luxembourg na Spain ni Falme hizo. Ujerumani hakuna term limits kwa Chancellor wala kwa Rais, Naongelea Ulaya Magharibi wa sababu ndio wadau wakubwa na wahubiri wa haya mamabo.
 
Unadhani walibya walifikiria kuwa matokeo yatakuwa hivi ilivyo sasa ila wakaona bora iwe hivyo kuliko utawala wa Gadaffi? Maana kinachoendelea sasa Libya kila mtu anakiona na ndiyo maana kinazungumziwa ila sijajua kama walibya wanaona ni bora hali ya sasa kuliko Gadaffi.
 
Mnisaidie tafakuri hii, zama hizi hawa CIA, wanashindwa wapi, vipi na kwanini wamekuwa tofauti na huko miaka ya nyuma, tulisoma jinsi walivyokuwa wakiondoa makandokando nchi zetu hizi, juzi juzi walifanikiwa Iraq, na hata Libya, lakini Syria wanaelekea kukwama, huku kusini mwa jangwa la sahara ni kama hawajishughulishi kabisa, au hivi vilio vyetu havisikiki au havijawafikia au vimepuuzwa.

Kwanini wasifundishe vijana wa nchi hizi mbinu za kutekeleza hazima hizo wenyewe bila wao kushiriki ikiwa hawataki kuhusika au kuhusishwa.

Nchi zetu hizi sio priority zao, kwanini wamekuwa wakikosoa bila kutoa solution, binafsi ningependa hata watoe mafunzo yale kwa wazawa kuliko kuangalia mambo kwa mbali bila kusaidia kutatua.

Waliua madikteta nini kimewasibu, hadi kutokutekeleza haya tena?!
Achana na mawazo hayo....Zama ni hizi hizi,, tena ni Zama mbaya.....usituletee balaaaaa....piga vita..Vita ya Tatu ya Dunia... Kinyago cha Chifu Burigi Chato ni laana.
 
CIA gani hao waliweka viongozi wa kidemokrasia?? Hivi unajua raisi wa USA aliwahi kuomba msamaha kwa kilichotokea kwa Guetamala? Sina hakika kama unaijua Guetamala
2016 Obama aliomba radhi kwa walichokifanya Libya, na wanajutia kwa uamuzi ule wa kumuondoa Gadaffi
Karibu
Huyo haijui CIA naona anajisemea tu. CIA ndio ilikuwa inakumbatia madikiteta Africa hii. Anamfahamu Mobutu? Anamfahamu Bokasa? Anamfahamu Amin? Anamfahamu Savimbi (japo hakuwa Rais lakini alitumika kumwaga damu).
Trump anajutia Marekani kumwondoa Saddam, anasema wakati wa Saddam kulikuwa na amani kuliko hali ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom