Historia inasema CIA walikuwa wakiondoa viongozi madikteta na waliweka viongozi wa kidemokrasia, zama hizi wanashindwa wapi?!

Demokrasia ni swala la kipropaganda. Maswala halisi ya nchi sio propaganda. Demokrasia ni mchezo wa danganya toto. Ililetwa kutufunika macho ili ipatikane gap ya kupangiwa viongozi. Mataifa makini huandaa na kupanga vongozi wao kwa ndani kabisa. Kinachosemwa mkuu sicho kinachotokea au kufanyika katika hali halisi.

Unaelewa unachokisema au umelewa madaraka hivyo unaogopa kuyapoteza?
 
Unadhani walibya walifikiria kuwa matokeo yatakuwa hivi ilivyo sasa ila wakaona bora iwe hivyo kuliko utawala wa Gadaffi? Maana kinachoendelea sasa Libya kila mtu anakiona na ndiyo maana kinazungumziwa ila sijajua kama walibya wanaona ni bora hali ya sasa kuliko Gadaffi.

Kwa taarifa ni bora kinachoendelea kuliko alichokuwa akiwafanyia. Usitake kutishia watu.
 
Mnisaidie tafakuri hii, zama hizi hawa CIA, wanashindwa wapi, vipi na kwanini wamekuwa tofauti na huko miaka ya nyuma, tulisoma jinsi walivyokuwa wakiondoa makandokando nchi zetu hizi, juzi juzi walifanikiwa Iraq, na hata Libya, lakini Syria wanaelekea kukwama, huku kusini mwa jangwa la sahara ni kama hawajishughulishi kabisa, au hivi vilio vyetu havisikiki au havijawafikia au vimepuuzwa.

Kwanini wasifundishe vijana wa nchi hizi mbinu za kutekeleza hazima hizo wenyewe bila wao kushiriki ikiwa hawataki kuhusika au kuhusishwa.

Nchi zetu hizi sio priority zao, kwanini wamekuwa wakikosoa bila kutoa solution, binafsi ningependa hata watoe mafunzo yale kwa wazawa kuliko kuangalia mambo kwa mbali bila kusaidia kutatua.

Waliua madikteta nini kimewasibu, hadi kutokutekeleza haya tena?!

Interest za marekani ndio kipaumbele cha kwanza popote duniani... Cha kwanza anachoangalia ni atatumia nini kwenye nini na atapata nini..... Kama haimlipi kivile atapotezea na kuishia kutoa matamko tuu
 
Kwa taarifa ni bora kinachoendelea kuliko alichokuwa akiwafanyia. Usitake kutishia watu.
Nimetisha watu kvp tena? Mie nimeeleza kuwa kinachoendelea sasa kipo wazi kila mtu anaona jinsi gani hali ilivyo mbaya na ndiyo mana watu wanajadili,sasa wewe unaesona utawala wa Gadaffi ndio kulikuwa na hali mbaya kuliko hali tunayoiona sasa basi ungeelezea huo utawala wa Gadaffi ulikuaje ili tupime na hali iliyo sasa.
 
Kaa kimya huna ujualo, kuliko hao wananchi kuishi chini ya utawala wa kikandamizaji, ni bora waanze upya.
 
Watu weupe wana kitu flani hivi cha utofauti. Wakipewa mtaa waishi hata kama watajenga nyumba za mbao lile eneo lazima litakuwa na kautofauti flani na maeneo mengine kimazingira.

Yaani tukibadilishana tukapewa nchi zao na wao tukawapa za kwetu baada ya miaka kadhaa Africa inakuwa nyingine kabisa na huko ulaya hutaamini tutakachokifanya.

Ila ndivyo tulivyo watuache tu wasituingilie. Kama Kuna kiongozi anatuumiza na hatuwezi kujitetea wenyewe tuachwe tu.
 
Zile ni Propaganda za Clinton sidhani kama CIA walitaka mtu kama Clinton sababu kuu ni Clinton angeanzisha vita na Urusi sababu ya beef lao na Clinton. America needed more power on all aspects ndo maana Trump akatokeza( unaweza kuta Trump ni mtu wao?
Unawazungumzia CIA waliopigwa na Russia kwenye uchaguzi wao au wapi hao??
 
Usipende kutamani ubeberu ukijiinua Africa ndugu,tengeneza tafakuri za watu weusi na bara letu,achana na makaburu hayo

Black man redemption
Mnisaidie tafakuri hii, zama hizi hawa CIA, wanashindwa wapi, vipi na kwanini wamekuwa tofauti na huko miaka ya nyuma, tulisoma jinsi walivyokuwa wakiondoa makandokando nchi zetu hizi, juzi juzi walifanikiwa Iraq, na hata Libya, lakini Syria wanaelekea kukwama, huku kusini mwa jangwa la sahara ni kama hawajishughulishi kabisa, au hivi vilio vyetu havisikiki au havijawafikia au vimepuuzwa.

Kwanini wasifundishe vijana wa nchi hizi mbinu za kutekeleza hazima hizo wenyewe bila wao kushiriki ikiwa hawataki kuhusika au kuhusishwa.

Nchi zetu hizi sio priority zao, kwanini wamekuwa wakikosoa bila kutoa solution, binafsi ningependa hata watoe mafunzo yale kwa wazawa kuliko kuangalia mambo kwa mbali bila kusaidia kutatua.

Waliua madikteta nini kimewasibu, hadi kutokutekeleza haya tena?!
 
Write your reply...Hao CIA hawajamuona huyu Dictator wetu mbobezi, mwizi kibaka! eti anajiita mzalendo, anakuwaje mzalendo wakati ni mkimbizi?
 
Duh watusaidie maana haya magenge ya wachache kujitwalia rasilimali za wengi yanatuumiza.
Ushauri kwako, kajielimishe zaidi kuhusu hili. Wamarekani kupitia hao CIA kamwe, hawafanyi “regime changes” kukusaidia wewe bali kujisaidia wao. Sasa wewe baki hapo ukisubiri.
 
Kwanini wasifundishe vijana wa nchi hizi mbinu za kutekeleza hazima hizo wenyewe bila wao kushiriki ikiwa hawataki kuhusika au kuhusishwa.

Nchi zetu hizi sio priority zao, kwanini wamekuwa wakikosoa bila kutoa solution, binafsi ningependa hata watoe mafunzo yale kwa wazawa kuliko kuangalia mambo kwa mbali bila kusaidia kutatua.

Waliua madikteta nini kimewasibu, hadi kutokutekeleza haya tena?!
Hebu kuwa mkweli. US ilikuwa inafanya hivyo kwa nchi ambazo zina maslahi nazo na wamekuwa nwanaweka vibaraka wao. Mfano mzuri ni Angola ambapo walikuwa wanamsaidia sana bwana Savimbi. Kama walivyofanya Iran kwa kumpindua waziri mkuu Mohamed Mosadegh[alitaifisha visima vya mafuta]. Mifano ipo mingi sana.
 
CIA gani hao waliweka viongozi wa kidemokrasia?? Hivi unajua raisi wa USA aliwahi kuomba msamaha kwa kilichotokea kwa Guetamala? Sina hakika kama unaijua Guetamala
2016 Obama aliomba radhi kwa walichokifanya Libya, na wanajutia kwa uamuzi ule wa kumuondoa Gadaffi
Karibu
Afadhali umeweka sawa ,dogo ana miaka 17 analeta story ya kiduanzi
 
Huu ulaji wa kuku mataahira na viazi vya kukaanga ndio huzalisha vijana wenye mawazo haya

Hivi wewe kweli unawaza mabeberu wakusaidie mambo ya ndani ya nchi yako?

Hii ni sawa na kumuita jirani hendisam aende chumbani kwa mkeo akamsaidie kutoa panya huku wewe tipwatipwa ukitetema nje kwa woga what a shame!!!
 
Hii ni dhana ya kawaida kwa watu wenye unyonge wa akili. Kwamba ‘Subiri kaka mkubwa aje ndio utauona moto.’
Ukweli ni kuwa kama tunaona kuna uovu fulani tunatakiwa kukomaa wenyewe kuuondoa. Hao ‘wakubwa’ mleta mada anaowalilia wenyewe walifanya hivyo hivyo. Wamarekani waliukataa ukoloni wa mama yao mwingereza, Warusi waliukataa na kuuondosha utawala wa Czar na baadae ukomunisti, na wachina pia walikataa na kujitoa kutoka makucha ya wajapani. Na wala hamna cha ajabu C I A kujali maslahi ya Marekani mpaka kuingilia mambo ya nchi nyingine. Huo ndio ubeberu wenyewe na ieleweke kuwa ubeberu ni aina ya maendeleo ya kiuchumi na sio hizi hadithi za wanasiasa huko vijijini au propaganda uchwara hapa jukwaani. Na wala tusifikiri kwamba hawaoni au hawajali mambo yanayoendelea huku kwetu ambayo wengine wanayaona sio sahihi wakati wengine wanaona ndio tumefika, kutegemeana na tofauti za itikadi, viwango vya elimu, uzoefu, ukomavu katika demokrasia
n. k. Ni kwamba tu watafanya kitu kama wakiona maslahi yao yanaathiriwa kupita kiwango fulani cha uvumilivu na sio kabla ya hapo. Na ukiwa na dikteta mwerevu hatavuka hicho kiwango chao cha uvumilivu hivyo atacheza nao mpaka basi huku wale wanaompinga wakiugumia maumivu ya moyo na hata mwili.
Lakini pia wakati mwingine wanaweza fanya kitu kwa ajili ya unafiki tu ili kuuonesha ulimwengu kuwa wanasimamia kile wanachojinadi kuwa wanakiamini, hasa kama kuna taharuki na kelele nyingi mahali, kama ilivyo Palestina kwa mfano.
Cha msingi ni kuwa chanzo kikuu cha uovu ni dhana ya baadhi ya binadamu kudhani kwamba wanaweza kujua, kuhodhi na kutekeleza mazuri yote kwa ajili ya watu wengine au taifa lote(the greater good) na hivyo kuwasukumilia pembeni wote wenye mawazo tofauti.
Hatupaswi kama nchi kufika mahali ambapo inabidi kubembeleza huruma ya watu wengine ndio tukae sawa.
Tutatue matatizo yetu sisi wenyewe. When big brother come he will come to rape and kill and not to help. And even if they bring some relief it will prabably be very marginal and only for a selfish few. Let us heed the lessons of history.
 
Back
Top Bottom