Tusiwalaumu viongozi wa dini,nao wanalinda maslahi yao na miradi yao.Walioongea Ikulu ndio hali halisi ya Dini na Siasa

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Watu wametweta,wamekasirika na wengine wamefura kwa maneno mazitomazito kwa kauli za viongozi wa dini walipoalikwa Ikulu.Mategemeo ya wengi,nadhani wale wasiokubaliana na hali ya utawala huu,na hasa waumini wa viongozi wa dini na huduma za kiroho,walidhani kuna mambo viongozi wao walipaswa kumfikishia Mh.Rais uso kwa uso.

Pengine wale "waumini rasharasha" wameanza kunung'unika,wanasononeka kwa taharuki,wanajiuliza,kama hawa tuliowategemea watusemee,mbona wanatukatisha tamaa na kutokuwa upande wetu?Inastua...

Ukiangalia mijadala katika mitandao mbalimbali,utaona wengi walidhani zile nyaraka za kitume zilizotolewa na viongozi wa kidini pale ndio ulikuwa muda muafaka wa kuziwasilisha na kusema mawazo yao na ya waumini wao.Baraza la Maaskofu Katoliki lilikuwa na ujumbe wake wa Kwaresma,alikuwepo Monsignore Nyaisonga,KKKT waliotishiwa kufutwa katika ramani ya makanisa Tanzania baada ya ukosoaji,nao walikuwepo.

Shura ya Maimamu nadhani walikuwepo,maana wale BAKWATA tunaambiwa si chombo kinachodhaniwa kuwakilisha mawazo ya Waislamu wote,wapo wasiokubaliana nao.Yule Gwajima aliyetuambia miezi kadhaa iliyopita kuwa Gavana wa Dsm ni bomu,naye alikuwepo.Huyu kila Jumapili alihubiri na kuongoza maombi ya kupata nafasi ya kumuona Rais ili amwambie jinsi Gavana wa Bandari ya Salama alivyo bomu katika utawala huu.

Kwa kweli,wengi wa walioongea,wameongea juu ya shida zao na changamoto ya miradi yao inayowaingizia fedha,na si shida na matamanio ya waumini wao.Kile kilio kuwa watu wanapotea na kukutwa kwenye viroba,haijasikika tena.Hakuna aliyeuliza changamoto za chaguzi ndogo,vurugu na ukiukwaji mkubwa wa kanuni na sheria katika chaguzi,na namna ambavyo serikali imejiandaa kuyazuia hayo katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2010.

Kilio cha watu kupotea bila jitihada za serikali kuonekana kuwajibika kuwatafuta,kupotea kwa Ben Saanane na Azzory Gwanda,kushambuliwa kwa mbunge wa upinzani mpaka leo watesi wake hawajakamatwa wala tu kuhisiwa.Haya yalikuwa na maswali ambayo yalipaswa walau kusikika katika mkutano ule.

Waumini wengi,pengine wengi zaidi wasio waumini,walidhani ule ndio muda muhimu wa yale maudhui ya nyaraka za Kichungaji zilizotolewa na viongozi wa dini,pale ndio ilikuwa mahali pake.Ni ajabu kuwa,katika mihadhara na mawaidha misikitini,Masheikh wengi wamekuwa wakiongelea juu ya kukamatwa,kuwekwa rumande na kuteswa kwa masheikh wa jumuiya ya Uamsho.

Kila mtu anajua,kina Sheikh Mselemu wapo ndani,bila hukumu kufikiwa tamati,mara kadhaa wamelalamika kufanyiwa ukatiri,kama kulawitiwa na kuteswa pasipo nafasi ya kujitetea.Nilidhani,na nadhani wengi pia walidhani,Masheikh wale,wakiongozwa na Sheikh mkuu wa Dar es Salaam,bila kuingilia Uhuru wa Mahakama,wangeiuliza serikali inayowashikilia,imefikia wapi??

Bahati mbaya au nzuri,wengi walipopata nafasi,waliuliza juu ya miradi yao,mmoja anaulizia leseni yake TCRA,anasema TV yake haifanyi biashara,lakini anasahau kuwa king'amuzi cha kuangalia TV yake anakiuza na kinamuingizia asilimia za mapato.Anatangaza huduma inayomuingizia kipato,hakuna jina la kumpa zaidi ya mjasiliamali.

Shule,hospital na vyuo vya elimu ya juu,zaidi ya kutoa huduma za kijamii katika jumuiya zetu,lakini pi ni biashara.Hizi zinaigiza pesa,zinaandikiwa "proposals" za kuombea pesa nje ya nchi,na sehemu ya pesa haingii katika miradi.Ni sehemu ya "vitega uchumi" katika baadhi ya taasisi za dini.

Pale kulikuwa na viongozi wa dini na viongozi wa Huduma za Kiroho,na ilibaki kidogo waparuane,pale mmoja alipoomba kuwepo na utaratibu wa kusajili huduma za kiroho zinazoibuka kama uyoga,mwingine akaona huduma yake inaguswa,akawa mkali.

Historia ni mwalimu mzuri,hata huko nyuma dunia iliwahi kuona,pale ambapo siasa na dini vinapatana,hata katika ushirika ulio na gharama katika maisha ya waumini,dini hupiga magoti na kukaa kimya.Sina mang'amuzi makubwa sana ya urafiki wa mashaka kati ya viongozi wa dini na siasa katika ulimwengu wa Kiilslamu,lakini walau nina nafasi ya kujadili ushirika wa aina hii katika uliwengu wa magharibi.Tunaweza kukumbushana kwa faida ya mjadala kwa mada fulani niliyokwisha kuibandika hapa siku kadhaa zilizopita.

Katika maandishi ya kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed",wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia,Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake.Maana kwa wakati ule,kanisa lilikuwa na "kontroo "ya maisha ya kiroho na serikali ilikuwa na "kontroo" ya maisha ya kisiasa.

Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya basi kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.

Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume,ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa.Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.

Pili alimua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya "bomani" na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.

Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za clubs zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.

Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing" ni "Public Crime"...Yaani mwananchi ukiwa mtaani unabushana,mtu akikwambia sema haki ya Mungu...Ukisema tu "Haki ya Mungu ntayafunga majizi yote,msema kweli ni mpenzi wa Mungu".Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu.Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile ya "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako"(Kwa hiyo amri hiyo ingekuwa enzi hizi,kuna mtu angekuwa jela zamaniii)

Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo wa 1920's kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.

Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.Ndoano hii ikanasa vizuri kwa kanisa.Hawakupepesuka wala kutikisika.

Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa in "Full Control of the Catholic Church".Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.

Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akaamuru kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.

Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa,na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani;japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.

Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Railway
station".Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa "kukontrol" Elimu?Mussolini alihitaji elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza "dini" kwa watoto.

Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio "rasharasha" waliona ni kama "rushwa" kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya serikali ya kifashisti ya Mussolin yalifanikiwa.Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.

Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini.Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema hewalaaa,huu ni utawala mzuri tu,maana umerudisha heshima ya Papa katika nchi ya Italia.

Mara kadhaa,Mussolin alitumia muda wake kukutana na viongozi wa dini na mara baada ya kikao,magazeti yalichapisha picha ya Mussolin na viongozi wa dini wakigonga glass zenye mvinyo mweupe.Hii ilijenga picha kuwa "All is well with us".

Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna "ufashisti",lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ni magumu,pesa imepotea na uchumi umenyambulika na kutikisika.Hii ni kauli ya yoyote aliye huru kufikiri bila hisia za itikadi.

Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa viwanda kama tunavyoambiwa,lakini haiwezi kuwa sababu ya kutokusema ukweli kuwa "HALI NI NGUMU",na tunapaswa kuhoji ili serikali tuliyoipa dhakana ituambie kwanini na lini tutavuka hapa.Kusema na kuuliza swali hili,haimaanishi hatukubaliani na Rais aliye madarakani,ila tunatumia haki yetu kumuhoji yeye tuliyempa dhamana ya kutuongoza.

Kama hali hii ni kwa sababu mianya yote ya wapiga dili imefunikwa basi na tuseme,na sio kusema kinyume chake.Kuwa baba wa kiroho na kuongea kinyume cha yale waumini wako ambao ni sehemu ya wananchi wa Tanzania wanalalamika,ni kuwa upande wa pili badala ya ule wa waumini wako.

Ndio maana wale wanafunzi wa historia ya kale,wanaweza kustuka.Kwamba kauli hizi za viongozi wa dini,walipopata nafasi kuwasilisha mawazo ya waumini wao,mbona wameishia kuongelea "miradi" yao tu??.Na hapa nadhani niseme hasaa,viongozi wa dini ambao wako "institutionalised",si hizi huduma za kiroho za kina barafu ambapo leo akiwa ziara USA au akifariki,kanisa nalo linaweza kufariki.

Kanisa libaki kuwa mali ya wanyonge,liachane na "urafiki" wa mashaka kama ule wa "Mussolini" na "Vatican" enzi hizo ya zama za giza za ufashisti Ulaya.
Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya ufashisti wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya Ugumu wa maisha na hali mbaya ya Uchumi kwa waumini wake.

Kutoa kauli za wogawoga za aina hii hadharani,na wakati mwingine mbele ya mimbari na katika altare takatifu,inatoa mashaka kwa waumini na wataamua kurudi na kupekua kurasa za kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed"

Tukizifunua kurasa hizi;Tutahitimisha kwa kusema "Viongozi wa dini wameongea lile walilojituma kuongea na sio walilotumwa kulitumikia kwa viapo na nadhiri".Tutawakumbusha kuwa kuutumikia mwili ni gharama zaidi ya kuitumikia roho.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body)

Tuitumikie Roho inayodumu milele,kuliko mwili unaooza na kuliwa na nyenyere.
 
Binafsi nimejiridhisha pasi na shaka kwamba hakuna mbinyo wowote wa haki za binadamu wala demokrasia nchini Kama ambavyo tumekuwa tukiaminishwa na wapinzani wa serikali yetu.

Hali hii ingekuwepo kwa fursa waliyopewa viongozi wetu wa kiroho lazima idadi ya nusu au hata kuzidi nusu ya wajumbe wangeelezea tatizo hilo kwani walishapa mchango wa awali toka kwa yule mchungaji Mangi ivo angetumika kama rejea ktk michango mingine.

Kwa ujumla walizungumzia matatizo ya huduma za kijamii kitu ambacho Mh. Rais anataka apewe muda zaidi aweze kuyatatua na asisumbuliwe na mikutano ya kukosoa ilhali ndio yupo ktk kipindi Cha utekelezaji.

Nimebaini wapinzani wa Rais wamegundua bila ya ku disturb utendaji wa serikali hii uchaguzi wa 2020 watakosa agenda madhubuti za kupatia kura hasahasa za ubunge ndio mana wanajaribu kufanya juhudi zote kutuaminisha kuwa hakuna demokrasia, na ukiukaji wa haki za binadamu vitu ambavyo viongozi wetu wa kiroho nafsi zao zimewasuta kusemea mambo yasiyokuwepo.

Nakumbuka tukiwa wadodo wakati fulani tulipokuwa tunawasumbua mama zetu hadi wanashindwa kufanyakazi zao kulima, kupika nk basi walikuwa wanatufinya kidogo unalia weee Kisha unalala na yeye anapata muda wa kuendelea na majukumu yake. Hili ndio naliona likitokea kwa wapinzani wa Magu. Kufinya kidogo yeye anapata fursa ya kuwafanyizia kazi Watanzania.

Aslam Aleykhum!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hamna viongozi wa dini Tanzania wala wa kiroho Kaka yangu, wote wapo kwajili ya matumbo yao na familia zao,
Ifikie wakati watanzania sadaka zetu tuwape masikini moja Kwa moja, sio lazima wawe masikini wale wapitao kuomba majiani,, ila haiitaji digrii kumjua masikini, tuachane na kutoa sadaka Kwenye Haya makanisa, maana sadaka zetu ndio zinawatajirisha hawa wachumia tumbo,
Mi binafsi nishaachaga kutoa Kwenye nyumba za ibada, Labda ukuta ukianguka ntachangia tena kiasi kidogo tu,

Hawa wachumia tumbo wanatajirika kwa hizi sadaka zetu, unadhani mtu Kama gwajima nn kimemtajirisha, ana ghorafa ukiambiwa ni lake unaweza usiamini
 
Siku zote, mara zote husoma nyaraka zako hadi mwisho hata ziwe ndefu kiasi gani....

Huu ndiyo ukweli halisi wa kilichotokea jana....

Haieleweki hakika tatizo lilikuwa ni nini....

Kwamba, labda mwaliko ulikuwa wa kushitukizwa hata wajitetee hawakujiandaa? Hawajui watu waumini wao wanaowaongoza wana shida/matatizo gani? Hawajui wajibu wa serikali kwa watu wao?

Au wao kwa kuwa wanapata sadaka mia mia, mia mbili na kuzitumia kununulia suti wanadhani waumini wao wanaziokota tu?

Viongozi wetu wa kiroho/dini hawaelewi kweli kuwa serikali ina wajibu wa kuhakikisha kuna utengamano ktk jamii ikiwa ni kiashiria namba moja cha watu kuwa na uchumi bora na kukuza kipato cha mtu mmoja moja?

Kiujumla, hawa baba zetu wa kiroho wanatuangusha na obviousily wana bei hawa, wananunulika hawa na wengi wanaingia taratibu ktk mtego huo!!
 
Binafsi nimejiridhisha pasi na shaka kwamba hakuna mbinyo wowote wa haki za binadamu wala demokrasia nchini Kama ambavyo tumekuwa tukiaminishwa na wapinzani wa serikali yetu.

Hali hii ingekuwepo kwa fursa waliyopewa viongozi wetu wa kiroho lazima idadi ya nusu au hata kuzidi nusu ya wajumbe wangeelezea tatizo hilo kwani walishapa mchango wa awali toka kwa yule mchungaji Mangi ivo angetumika kama rejea ktk michango mingine.

Kwa ujumla walizungumzia matatizo ya huduma za kijamii kitu ambacho Mh. Rais anataka apewe muda zaidi aweze kuyatatua na asisumbuliwe na mikutano ya kukosoa ilhali ndio yupo ktk kipindi Cha utekelezaji.

Nimebaini wapinzani wa Rais wamegundua bila ya ku disturb utendaji wa serikali hii uchaguzi wa 2020 watakosa agenda madhubuti za kupatia kura hasahasa za ubunge ndio mana wanajaribu kufanya juhudi zote kutuaminisha kuwa hakuna demokrasia, na ukiukaji wa haki za binadamu vitu ambavyo viongozi wetu wa kiroho nafsi zao zimewasuta kusemea mambo yasiyokuwepo.

Nakumbuka tukiwa wadodo wakati fulani tulipokuwa tunawasumbua mama zetu hadi wanashindwa kufanyakazi zao kulima, kupika nk basi walikuwa wanatufinya kidogo unalia weee Kisha unalala na yeye anapata muda wa kuendelea na majukumu yake. Hili ndio naliona likitokea kwa wapinzani wa Magu. Kufinya kidogo yeye anapata fursa ya kuwafanyizia kazi Watanzania.

Aslam Aleykhum!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi Sheikh,kwa muktadha wa mjadala.Na hii ndiyo sifa ya kujadiliana.Mnakubaliana na kutokukubaliana kwa staha.Asante
 
Hakuna viongozi walio tumwa na Mungu wakawa ka hawa. Hawa niviongozi wa Dino zao kwa maslahi ya hizo NGOs zao. Utaona sehemu kubwa walikuwa wanazungumzia hela na si ustawi wa watu wanao waongoza. Uhuru wa watu kwao ni kero kwani jinsi serikali ya siasa isivyo taka watu wawe guru ,hawa nao hawapendi waumini wao wawe guru pia. Kwani wakiwa huru hizo NGO zao zitakifa kwanza asilimia 90 ni waongo wababaishaji na wazandiki. Hizo Dini ni ajira kwao. Kwa ujumla ni wajasiriamali wa kutumia hizo Dini( NGO)
 
Umepigilia msumari.
 
KIlichotokea jana hakikutegemewa, zaidi ya kumsifia mfalme hakuna ambacho viongozi hawa wameweza kumwambia Mfalme maana badala ya wao kumshauri yeye ameawashauri namna ya kuendesha taasisi zao. Binafsi nilitegemea kuona zile nyaraka zikisomwa tena jana au kukabidhiwa kwake kama mawazo kutoka taasisi zao. FR. DR. Kitima sikuelewa alitumwa nini na TEC au yale yalikuwa mawazo yake binafsi na sio ule waraka wa TEC, Wapo ambao watasema ule ulikuwa ujumbe wa Noeli n.k. je tokea ujumbe ule utoke kuna jambo gani limebadilika? au yote sasa yamerekebishwa.
 
images%20(3).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imani ilisha geuzwa kuwa Biashara kitambo sana ,wanacho tuhusia Waumini sicho wanacho kisimamia kuanzia Rohoni mwao mpaka Akilini mwao.Binafsi nna wachukulia kama Wana Siasa wengine tu .
 
Watu wametweta,wamekasirika na wengine wamefura kwa maneno mazitomazito kwa kauli za viongozi wa dini walipoalikwa Ikulu.Mategemeo ya wengi,nadhani wale wasiokubaliana na hali ya utawala huu,na hasa waumini wa viongozi wa dini na huduma za kiroho,walidhani kuna mambo viongozi wao walipaswa kumfikishia Mh.Rais uso kwa uso.

Pengine wale "waumini rasharasha" wameanza kunung'unika,wanasononeka kwa taharuki,wanajiuliza,kama hawa tuliowategemea watusemee,mbona wanatukatisha tamaa na kutokuwa upande wetu?Inastua...

Ukiangalia mijadala katika mitandao mbalimbali,utaona wengi walidhani zile nyaraka za kitume zilizotolewa na viongozi wa kidini pale ndio ulikuwa muda muafaka wa kuziwasilisha na kusema mawazo yao na ya waumini wao.Baraza la Maaskofu Katoliki lilikuwa na ujumbe wake wa Kwaresma,alikuwepo Monsignore Nyaisonga,KKKT waliotishiwa kufutwa katika ramani ya makanisa Tanzania baada ya ukosoaji,nao walikuwepo.

Shura ya Maimamu nadhani walikuwepo,maana wale BAKWATA tunaambiwa si chombo kinachodhaniwa kuwakilisha mawazo ya Waislamu wote,wapo wasiokubaliana nao.Yule Gwajima aliyetuambia miezi kadhaa iliyopita kuwa Gavana wa Dsm ni bomu,naye alikuwepo.Huyu kila Jumapili alihubiri na kuongoza maombi ya kupata nafasi ya kumuona Rais ili amwambie jinsi Gavana wa Bandari ya Salama alivyo bomu katika utawala huu.

Kwa kweli,wengi wa walioongea,wameongea juu ya shida zao na changamoto ya miradi yao inayowaingizia fedha,na si shida na matamanio ya waumini wao.Kile kilio kuwa watu wanapotea na kukutwa kwenye viroba,haijasikika tena.Hakuna aliyeuliza changamoto za chaguzi ndogo,vurugu na ukiukwaji mkubwa wa kanuni na sheria katika chaguzi,na namna ambavyo serikali imejiandaa kuyazuia hayo katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2010.

Kilio cha watu kupotea bila jitihada za serikali kuonekana kuwajibika kuwatafuta,kupotea kwa Ben Saanane na Azzory Gwanda,kushambuliwa kwa mbunge wa upinzani mpaka leo watesi wake hawajakamatwa wala tu kuhisiwa.Haya yalikuwa na maswali ambayo yalipaswa walau kusikika katika mkutano ule.

Waumini wengi,pengine wengi zaidi wasio waumini,walidhani ule ndio muda muhimu wa yale maudhui ya nyaraka za Kichungaji zilizotolewa na viongozi wa dini,pale ndio ilikuwa mahali pake.Ni ajabu kuwa,katika mihadhara na mawaidha misikitini,Masheikh wengi wamekuwa wakiongelea juu ya kukamatwa,kuwekwa rumande na kuteswa kwa masheikh wa jumuiya ya Uamsho.

Kila mtu anajua,kina Sheikh Mselemu wapo ndani,bila hukumu kufikiwa tamati,mara kadhaa wamelalamika kufanyiwa ukatiri,kama kulawitiwa na kuteswa pasipo nafasi ya kujitetea.Nilidhani,na nadhani wengi pia walidhani,Masheikh wale,wakiongozwa na Sheikh mkuu wa Dar es Salaam,bila kuingilia Uhuru wa Mahakama,wangeiuliza serikali inayowashikilia,imefikia wapi??

Bahati mbaya au nzuri,wengi walipopata nafasi,waliuliza juu ya miradi yao,mmoja anaulizia leseni yake TCRA,anasema TV yake haifanyi biashara,lakini anasahau kuwa king'amuzi cha kuangalia TV yake anakiuza na kinamuingizia asilimia za mapato.Anatangaza huduma inayomuingizia kipato,hakuna jina la kumpa zaidi ya mjasiliamali.

Shule,hospital na vyuo vya elimu ya juu,zaidi ya kutoa huduma za kijamii katika jumuiya zetu,lakini pi ni biashara.Hizi zinaigiza pesa,zinaandikiwa "proposals" za kuombea pesa nje ya nchi,na sehemu ya pesa haingii katika miradi.Ni sehemu ya "vitega uchumi" katika baadhi ya taasisi za dini.

Pale kulikuwa na viongozi wa dini na viongozi wa Huduma za Kiroho,na ilibaki kidogo waparuane,pale mmoja alipoomba kuwepo na utaratibu wa kusajili huduma za kiroho zinazoibuka kama uyoga,mwingine akaona huduma yake inaguswa,akawa mkali.

Historia ni mwalimu mzuri,hata huko nyuma dunia iliwahi kuona,pale ambapo siasa na dini vinapatana,hata katika ushirika ulio na gharama katika maisha ya waumini,dini hupiga magoti na kukaa kimya.Sina mang'amuzi makubwa sana ya urafiki wa mashaka kati ya viongozi wa dini na siasa katika ulimwengu wa Kiilslamu,lakini walau nina nafasi ya kujadili ushirika wa aina hii katika uliwengu wa magharibi.Tunaweza kukumbushana kwa faida ya mjadala kwa mada fulani niliyokwisha kuibandika hapa siku kadhaa zilizopita.

Katika maandishi ya kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed",wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia,Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake.Maana kwa wakati ule,kanisa lilikuwa na "kontroo "ya maisha ya kiroho na serikali ilikuwa na "kontroo" ya maisha ya kisiasa.

Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya basi kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.

Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume,ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa.Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.

Pili alimua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya "bomani" na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.

Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za clubs zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.

Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing" ni "Public Crime"...Yaani mwananchi ukiwa mtaani unabushana,mtu akikwambia sema haki ya Mungu...Ukisema tu "Haki ya Mungu ntayafunga majizi yote,msema kweli ni mpenzi wa Mungu".Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu.Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile ya "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako"(Kwa hiyo amri hiyo ingekuwa enzi hizi,kuna mtu angekuwa jela zamaniii)

Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo wa 1920's kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.

Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.Ndoano hii ikanasa vizuri kwa kanisa.Hawakupepesuka wala kutikisika.

Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa in "Full Control of the Catholic Church".Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.

Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akaamuru kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.

Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa,na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani;japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.

Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Railway
station".Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa "kukontrol" Elimu?Mussolini alihitaji elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza "dini" kwa watoto.

Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio "rasharasha" waliona ni kama "rushwa" kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya serikali ya kifashisti ya Mussolin yalifanikiwa.Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.

Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini.Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema hewalaaa,huu ni utawala mzuri tu,maana umerudisha heshima ya Papa katika nchi ya Italia.

Mara kadhaa,Mussolin alitumia muda wake kukutana na viongozi wa dini na mara baada ya kikao,magazeti yalichapisha picha ya Mussolin na viongozi wa dini wakigonga glass zenye mvinyo mweupe.Hii ilijenga picha kuwa "All is well with us".

Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna "ufashisti",lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ni magumu,pesa imepotea na uchumi umenyambulika na kutikisika.Hii ni kauli ya yoyote aliye huru kufikiri bila hisia za itikadi.

Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa viwanda kama tunavyoambiwa,lakini haiwezi kuwa sababu ya kutokusema ukweli kuwa "HALI NI NGUMU",na tunapaswa kuhoji ili serikali tuliyoipa dhakana ituambie kwanini na lini tutavuka hapa.Kusema na kuuliza swali hili,haimaanishi hatukubaliani na Rais aliye madarakani,ila tunatumia haki yetu kumuhoji yeye tuliyempa dhamana ya kutuongoza.

Kama hali hii ni kwa sababu mianya yote ya wapiga dili imefunikwa basi na tuseme,na sio kusema kinyume chake.Kuwa baba wa kiroho na kuongea kinyume cha yale waumini wako ambao ni sehemu ya wananchi wa Tanzania wanalalamika,ni kuwa upande wa pili badala ya ule wa waumini wako.

Ndio maana wale wanafunzi wa historia ya kale,wanaweza kustuka.Kwamba kauli hizi za viongozi wa dini,walipopata nafasi kuwasilisha mawazo ya waumini wao,mbona wameishia kuongelea "miradi" yao tu??.Na hapa nadhani niseme hasaa,viongozi wa dini ambao wako "institutionalised",si hizi huduma za kiroho za kina barafu ambapo leo akiwa ziara USA au akifariki,kanisa nalo linaweza kufariki.

Kanisa libaki kuwa mali ya wanyonge,liachane na "urafiki" wa mashaka kama ule wa "Mussolini" na "Vatican" enzi hizo ya zama za giza za ufashisti Ulaya.
Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya ufashisti wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya Ugumu wa maisha na hali mbaya ya Uchumi kwa waumini wake.

Kutoa kauli za wogawoga za aina hii hadharani,na wakati mwingine mbele ya mimbari na katika altare takatifu,inatoa mashaka kwa waumini na wataamua kurudi na kupekua kurasa za kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed"

Tukizifunua kurasa hizi;Tutahitimisha kwa kusema "Viongozi wa dini wameongea lile walilojituma kuongea na sio walilotumwa kulitumikia kwa viapo na nadhiri".Tutawakumbusha kuwa kuutumikia mwili ni gharama zaidi ya kuitumikia roho.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body)

Tuitumikie Roho inayodumu milele,kuliko mwili unaooza na kuliwa na nyenyere.
ndio maana siku hizi huki kinachoitwa Sadaka na Zaka sitoi tena, yaani makofu badala ya kuwasrmea waumini wao wanataka.mambo yao tu yaende sawa.

Leo tar24 nimepigiwa simu na baba huk kijijini etii kanisa linafanya harambee tulichangie niemsikiliza kwa makini, kimoyo moyo nikasema sadaka na zaka zangu huenda kuwasomesha wadogo zangu na kusaidia ndugu zangu tu wenye shida.

Siko tayari kuwatolea pesa zangu hawa wahuni wanaojiita maaskofu.
 
Bora viongozi wa kikristo ila kwa waislam wallah tunavilaza huko juu hakuna mfano.

Kama kauli yangu itaniingiza jahanam sawa ila waislam tuko imara ila upupu uliyopo ngazi za kitaifa ni mtihani sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tukiongea kwa lugha ya jumla hakuna kiongizi wa kidini au wa kiroho awe wa Kiislam au Kikristo ambao katika mkutano na Mh. Rais waliongea matamanio ya wamini/waumini/kondoo au hadhira anayoihudumia katika mimbari ya nyumba zao za ibada!

Ukiachilia mmoja au wawili miongoni mwao waliojaribu japo kwa uoga na kupaka mafuta kuyasema yale wanaowaongoza wanatamani waseme mbe ya mkuu wa nchi, wengine wote hata wale tuliowazoea kuwaona kama wasemaji wazuri juzi hiyo hawakuyasema yale wafuasi wao walitamani wayaseme.

Si kwa mashekh wala maaskofi na wachungaji, wote wamejivika joho la WOGA na udhaifu kama wa muhimili aliousema CAG!

Hii inamaanisha kwamba mwananchi wa kawaida hana mtu wa kumsemea.

Viongozi wa kisiasa waliowazoea kuwasemea hasa wapinzani na wanaharakati wa mashirika yasio ya serikali wote wamefunga midomo yao!

Hakuna jasiri wa kumueleza mfalme ajifunge msuli vizuri maana amekaa utupu!...kila mtu anaangalia nafsi yake!

Viongozi wa dini wanaangali namna bora ya kujineemesha kimapato kupitia sadaka na misaada iliyopewa ruhusa na serikali, hakuna anayetaka kuiudhi serikali kwa kuiambia ukweli!

Je wananchi waende wapi?...je waende nje ya mipaka kwa mabeneru kuomba wawasemee matattizo yao?
 
Viongozi wa dini wameongea lile walilojituma kuongea na sio walilotumwa kulitumikia kwa viapo na nadhiri".Tutawakumbusha kuwa kuutumikia mwili ni gharama zaidi ya kuitumikia roho.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body)

Tuitumikie Roho inayodumu milele,kuliko mwili unaooza na kuliwa na nyenyere.
Asante kwa makala nzuri mkuu! Sasa tumetambua vyema misimamo ya viongozi wetu wa kiroho. Ila kuhusu hali tunayopitia ni Mungu atatuokoa (Mungu atafanya mlango wa kutokea pasipo na njia) tusichoke kuomba.
 
Back
Top Bottom