Historia fupi ya ugonjwa kisukari

MalcolM XII

JF-Expert Member
Mar 19, 2019
5,236
14,206
Fun fact kuhusu historia ya kisukari ni kwamba madaktari wa mwanzo kabisa waliweza kumtambua mgonjwa mwenye kisukari kwa kuonja mkojo wake!

IMG_0691.jpg

Kisukari ni moja kati ya magonjwa ya kwanza kabisa kutambuliwa na kuandikwa kwenye maandishi miaka ya 250BC huko Misri ikielezea tatizo la “kukojoa sana”.

Wataalamu wa magonjwa tiba wa kihindi kwenye miaka hiyo walielezea tatizo hili kuwa ni “mkojo wa asali’’ kwa sababu mkojo aina hii uliwavutia sana sungusungu.

Kwa lugha ya kigeni huitwa DIABETES MELLITUS, huku neno “diabetes” likimaanisha ‘kupitisha’ (to pass through) na “mellitus” likimaanisha ‘asali/sukari’ (honeyed or sweet).

Miaka ya 1745, mtaalamu wa mambo ya afya bwana Johann Peter Frank alitofautisha kisukari hiki na kile cha diabetes insipidus ambacho nacho kinahusiana na kukojoa sana lakini mkojo huwa hauna sukari.

Baadae katika miaka ya 1889, ikaja kugundulika kazi ya kongosho kwenye kuzalisha homoni ya insulini ambayo upungufu wake unapelekea tatizo hilo.

Wanasayansi Joseph Van Mering na Oskar Minkowski walimchukua mbwa na kumfanyia upasuaji mdogo kisha wakamtoa kongosho.
Baadae akaanza kuonyesha dalili nyingi za kisukari na alikufa siku chache baadae.

Ugunduzi wa tiba ya kisukari kwa kipindi hicho ulikuwa na changamoto nyingi sana. Wanasayansi walitumia insulini ya Farasi na Nguruwe ili kuwatibu wagonjwa wa kisukari jambo lilipelekea wengi kupata madhara ikiwemo mzio(allergy) n.k

Maendeleo ya utandawazi na teknolojia ya sayansi yamepelekea faida kubwa ikiwemo ugunduzi wa teknolojia ya Genetic engineering (Recombinant Gene Technology) ambayo imewawezesha wanasayansi kutengeneza insulini sawa na ile ya binadamu kutoka kwa viumbe wadogo (micro organisms) wakiwepo bakteria na fangasi.

Yaani inachukuliwa sample ya gene ya binadamu inayotengeneza insulini, inapandikizwa kwenye seli ya bakteria ambao wanaweza kuzalisha taarifa zao kwa haraka na mwisho kuivuna insulini mpya na ya kutosha ambayo iko sawa kabisa na ile ya binadamu.

IMG_0690.jpg
 
Fan fact kuhusu historia ya kisukari ni kwamba madaktari wa mwanzo kabisa waliweza kumtambua mgonjwa mwenye kisukari kwa kuonja mkojo wake!

View attachment 1690839

View attachment 1690825
Shukran kwa elimu.
 
Ma Dr wa zamani walishindwa kutumia ile ya kukojoa chini kisha kuangalia sisimizi?
 
Wataalamu wa zamani waliweka sana misingi kwa wataalamu wa sasa. Imagine maDr wa sasa ndo watibu kwa kuonja mkoja wa mgonjwa na magonjwa yalivyo mengi sasa hivi.

Kwa hii korona tiba nyingi zingesimama
 
Ma Dr wa zamani walishindwa kutumia ile ya kukojoa chini kisha kuangalia sisimizi?
Ndo elimu iliyokua miaka hiyo. Hata sasa ukiangalia taaluma za zaman unaweza ukadhan kama hawakufikiria vizuri ila ndo walioweka msingi wa taaluma ya sasa.

Eg vijijini walijenga nyumba ukiziangalia kwa sasa ni kama za ajabu lakini ndo base ya wataalam wa nyumba za sasa
 
Mkuu avatar zetu zinafanana,
Nje ya maada

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom