Historia fupi ya deni la Stirling Civil Engineering Ltd

Historia fupi ya deni la Stirling Civil Engineering Ltd

Alafu utamsikia analaumu waliotuibia kwenye madini kupitia mikataba tuliosaini wenyewe kuwa eti wanatuacha sisi masikini wao wanatajirika anasahau maamuzi yake nayo yanatuletea umasikini pia.
 
Ukifuatilia muhtasari wa hii hadithi ya Bilioni 90 (87) unachukia sana....

Tulipovunja mkataba wa kandarasi yao ya ujenzi wa barabara ya Wazo Hill hadi Bagamoyo (kibabe), Stirling Civil Engineering Ltd, wakatupeleka mahakamani.>>>> (TUKASEMA HATUTISHWI)

Tarehe 10 Desemba, 2009 - Mahakama ya Usuluhishi ya Paris ikaamuru tuwalipe fidia ya hasara tuliyowasababishia kwa kiburi chetu, ya dola za Marekani milioni 25 (Takribani Shilingi Bilioni 40 wakati huo) >>>> TUKAGOMA!

Serikali yetu ikakata Rufaa, tarehe 10 Juni 2010 hukumu ya rufaa ikasomwa, tukapigwa chini. Tukaamuriwa kuilipa kampuni hiyo fedha hizo vinginevyo kila mwaka mmoja utakaohesabiwa tutalipa na riba ya asilimia 8. >>>>TUKADHARAU!

Kutokana na ucheleweshaji wa malipo, deni hilo limeongezeka hadi dola za Marekani milioni 38.7 kufikia tarehe 30 Juni, 2017. Hii ni sawa na takribani shilingi Bilioni 90 za Tanzania. >>>> TUKAENDELEA KUGOMA!

Mwezi Julai 2017, kampuni inayotudai imekamata ndege yetu, 'Bombadier Dash Q400' - sharti la kurudishiwa ndege yetu (isipigwe mnada) ni sisi kulipa hizo shilingi bilioni 90. >>>> NDIYO TUMEKUMBUKA KUWAPIGIA MAGOTI!

[Tayari Waziri Mahiga amewaomba Stirling Construction tuwalipe Bilioni 30 (kama advance payment) waachie ndege yetu wakati mazungumzo mengine ya namna ya kumalizia deni lililobaki yakiendelea. Halafu kuna watu bila aibu wanasema Lissu ndiye sababu ya ndege yetu kukamatwa. Hivi Lissu anahusikaje hapa?]

Ninajiuliza hivi akili zetu tumemgawia mwekezaji gani?

Yani tunakwenda kuwalipa watu Bilioni 90, za bure [kwa uzembe wa mtu mmoja aliyevunja mkataba kwa kukurupuka.!]

Bilioni 90 ni sawa na Magari 3,000 ya Wagonjwa (Ambulances) na yangeliweza kugawiwa kila kata ya Tanzania.

Bilioni 90 ni sawa na matrekta 1,500 ya kisasa na tungeliweza kuyagawa kwa nusu ya kata za Tanzania na kwa miaka mitano idadi ya Makumi Elfu ya wakulima wangefaidika.

Bilioni 90 ni pesa nyingi sana, mno! Lakini zinakwenda kupotea hivi hivi, na wanaoohusika na kiburi kilichopelekea hasara hii siyo tu kwamba wamekataa kujiuzulu au kuomba radhi! Bali wanatumia nguvu kubwa zaidi kutaka umma uamini kuwa wao ni "watakatifu" na "hawafanyi makosa makubwa kama haya."

Tungekuwa na watu wenye utu wangelitoka hadharani, wangekiri makosa yao, wakajiuzulu na kuomba wasishtakiwe. Kinyume chake, waliotutia hasara hii ndo wako mstari wa mbele kuwatisha waliofichua KASHFA hii.
Mkuu sijaelewa, hao Sterling ndio waliotengeneza ndege pia? Vipi wazuie? Ufafanuzi wa kibiashara mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sijaelewa, hao Sterling ndio waliotengeneza ndege pia? Vipi wazuie? Ufafanuzi wa kibiashara mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ufahamu wangu mdogo ni hivi., sterling ni kampuni la ujenzi la wadai wetu, wakaenda kutafuta kampuni nyingine inayokamata mali za wadaiwa sugu, na hiyo kampuni ikaenda kuikamata bombardie yetu! Sijui kama nimeeleweka!
 
Kwa ili suala sijui tatizo ni wanasheria wanaotumiwa na serikali au viongozi wenyewe wa serikali, kwa mwanasheria makini hawezi kushauri serikali kuvunja mkataba ambao anajua kufanya hivyo kuingiza nchi kwenye hasara kubwa. Kama serikali walipata ushauri kutoka kwa wanasheria kwa nn hawakufanya maamuzi sahihi? walivunja huo mkataba kwa faida ya nani? Kama kwa faida ya nchi mbona Leo tunadaiwa hizo fedha zote? Kitu kinachoumiza viongozi hawaumizwi na chochote kuhusiana na malipo ya hizo fedha wanaoumia ni raia wa kawaida kwa sababu ndio wanaokamuliwa kodi kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu apoo hiyo historia hainaa mashiko ya ainaa yoyotee tupige mdomo tuu anae mpinga Magufuri ni kibaraka wa wakoloni mamboleo ndiyo anayo yaleta lissu sasa ivii tafuta Mada nyingine haunaa takwimu za unacho semaaa

Sent using Jamii Forums mobile app

Embu shuka pointi zako basi tuone huo ukibaraka ukoje.
Mleta mada amekupa facts and figures!
 
Sababu za kuvunjwa kwa mkataba ni zipi?
Na tazamia jibu zaidi ya "kukurupuka"!
 
Historia mbona haionyeshi mkataba uliingiwa lini?
Historia haionyeshi mkataba ulivunjwa lini?
Historia haionyeshi thamani ya mkataba uliovunjwa lini...
Historia haionyeshi waliovunja mkataba ni kina nani...

Historia imerukia kwenye maamuzi ya Mahakama na Rufaa
Kwani anayetakiwa kujua. Kesi kwa undani ni mlalamikaji, mlalamikiwa na wanasheria wao!! Waulize hao ndio watakupa facts za kesi
 
Kwani anayetakiwa kujua. Kesi kwa undani ni mlalamikaji, mlalamikiwa na wanasheria wao!! Waulize hao ndio watakupa facts za kesi

Soma hoja iliyopo na uielewe, hili swali anatakiwa ajibu aliyeanzisha hoja maana chanzo cha deni ni baada ya mkataba husika kuvunjwa, historia ya mkataba inaanza baada ya kusainiwa ili utekelezaji uanze sasa kama unaelezea ili watanzania tujue inabidi tuanzie mwanzo kabisa
 
Hakuna kitu apoo hiyo historia hainaa mashiko ya ainaa yoyotee tupige mdomo tuu anae mpinga Magufuri ni kibaraka wa wakoloni mamboleo ndiyo anayo yaleta lissu sasa ivii tafuta Mada nyingine haunaa takwimu za unacho semaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1] [emoji1] [emoji1] .mjomba unaweza ukashindana na radio mpaka ikazima.si kwa utomaso huu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom