Ukweli ni kwamba wanawake wakijifungua watoto kadhaa hubadilika sana. Na kama hajiangalii akajiachia tu anaweza kuchakaa mapema sana. Sasa kama ulimpendea wembamba wa tumbo, sijui ngozi laini ndiyo utajijua. Na wakati mwingine hata misambwanda hupotea. Yaani mkeo aliyekuwa na msambwanda wa kutingishika sasa kazaa watoto wawili kajiachia kenenepa jumla kama vile kavaa ovaroli hata msambwanda huwezi kuuona tena. Hata akipita unamwangalia kwa jicho la kuibia unajisemea kimoyomoyo dah hapa nilipiga chini kuchagua.
Kama mdau alivyosema hapo juu, mwanaume una wajibu pia wa kuhakikisha kuwa mapenzi hayafi. Hakikisha mkeo anavaa vizuri. Anajipamba. Manukato uyapendayo. Kama unene wake unakukera fanyeni mazoezi pamoja. Mitoko(dates) angalau kwa mwezi mara mbili. Sehemu nzuri tulivu ambako mtakaa tu na kutathmini penzi lenu kwa ujumla. No hard talk. No ishu za watoto. No ishu za pesa. Just simple light talk. Mkumbushe kuwa bado unampenda na kama kuna kitu unakimisi mwambie. Open communication. Na wewe muulize kama kuna kitu anataka uwe unafanya ili kumsisimua. Yaweza kuwa ni kumsaidia jikoni akiwa anapika. Au kutandika kitanda pamoja kama mlivyokuwa mnafanya zamani. Au hata kumpaka mafuta na kumkanda kidogo akitoka kukoga au akitaka kulala. Wakati mwingine utakumbushwa kuwa mume wangu siku hizi wala huniambii kama unanipenda. Vitu vidogo ulivyokuwa unafanya zamani na sasa huvifanyi tena. Vizawadi vile vidogo vya kichokozi ulivyokuwa umemzoesha...
Mapenzi ni hisia na hisia, japo ni suala la kikemikali na homoni, saikolojia pia ina nafasi kubwa sana. Na mara nyingi ni vitu vidogo dogo tu...na jambo la muhimu sana ni kusali pamoja kama wote ni waumini. Hakuna jambo linaloleta amani ya kweli kwa wapendanao kama kupiga magoti mbele ya Mungu mkilia pamoja na kumkabidhi Mungu mapungufu yenu na kumuomba awasamehe ili nanyi msameheane na kuanza upya. Pure spiritual and emotional karthasis kwa wapendanao...
Tunachokosea sisi wanaume ni ile kuona hisia zimepungua na badala ya kutafuta suluhisho tunaamua kukata njia ya mkato kutafuta mchepuko ambao utakuwa unatufanyia yale ambayo tungependa wake zetu ndiyo watufanyie. Mapenzi nyumbani hakuna na watu mnaishi tu ali mradi mpo. Frustrations, tension na stress kibao hasira nje nje mwishowe hata maana ya ndoa inakosekana.
Wanandoa Mungu na Awasaidie

