Mkuu, hisa ili ikuletee faida au hasara, inategemea na mwenendo wa kibiashara wa kampuni unayonunua hisa. Biashara ikienda vizuri na kwa mafanikio, wanahisa mnagawana faida lakini biashara ikienda vibaya kama ya TOL na mkawa mnapata hasara, wanahisa mnagawana hasara. Hivyo ni biashara ya kubahatisha na ndiyo maana wengi huangalia mwenendo na ustawi wa kampuni kabla ya kuamua kununua hisa.