Hisa za precision air

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,739
744
Habari za mchana wana JF, wadau kuna hisa za hili kampuni zinauzwa hisa moja ni Tsh 475 na wanaanza kuuza kuazia hisa 200. Nina mpango wa kununua hisa 200: naomba elimu hapa wanauchumi faida ninazoweza kupata kama mwanahisa na risk zake. Sijawahi miliki hizi hisa na moja ya masharti ni kuwa mwombaji anatakiwa kupata ushauri wa wataalam kuhusu ushiriki wao na wala kampuni haitahusika, sasa naomba ushauri ili nisije ingia mkenge ingawa risk kwenye ni mojawapo ya challenge naomba msaada zaidi. Naamini wachumi mtanisaidia. Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu, hisa ili ikuletee faida au hasara, inategemea na mwenendo wa kibiashara wa kampuni unayonunua hisa. Biashara ikienda vizuri na kwa mafanikio, wanahisa mnagawana faida lakini biashara ikienda vibaya kama ya TOL na mkawa mnapata hasara, wanahisa mnagawana hasara. Hivyo ni biashara ya kubahatisha na ndiyo maana wengi huangalia mwenendo na ustawi wa kampuni kabla ya kuamua kununua hisa.
 
Kwa haya makampuni yetu tunavyoyajua kila mwaka wanatoa financial statement zao zina loss kila mara kukwepa corporate tax sijui hapo minority shareholder kama wewe utapata wapi pesa yako.
 
Zingekuwa za Air Tanzania Ningenunua -- watu wameuwa shirika letu, wamelipamba hili limekuwa kama national airline, then sisi watanzania tunashangilia kwenda kununua hisa.

Aisee hela ninazo ila SINUNUI - naenzi na nakumbuka THE WINGS OF KILIMANJARO --- nasikia uchunguu...
 
Kwa haya makampuni yetu tunavyoyajua kila mwaka wanatoa financial statement zao zina loss kila mara kukwepa corporate tax sijui hapo minority shareholder kama wewe utapata wapi pesa yako.

Hapo kwenye ujanja ujanja wa makampuni yetu kukwepa kodi, sijui wanahisa waambiwa ukweli au wanaonyeshwa zile takwimu za TRA.
 
Zingekuwa za Air Tanzania Ningenunua -- watu wameuwa shirika letu, wamelipamba hili limekuwa kama national airline, then sisi watanzania tunashangilia kwenda kununua hisa.

Aisee hela ninazo ila SINUNUI - naenzi na nakumbuka THE WINGS OF KILIMANJARO --- nasikia uchunguu...

Yaani Mkuu FUSO umenikumbusha mbali, nimesononeka hadi basi. Uroho wa mali wa hawa wazee wetu ndo unaiua nchi yetu!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom