hisa za CRDB vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hisa za CRDB vipi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Malila, May 3, 2009.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Nimeona tangazo la kuuzwa hisa za crdb. Kilichonishitua ni bei ya hisa hizo. Nakumbuka hisa za crdb mwanzoni ziliuzwa bei kubwa (sikumbuki bei lakini ilikuwa zaidi ya 1000/ hivi) lakini hii bei ya leo ( Tsh 150/ kwa hisa moja) inaacha maswali mengi kichwani. Kwa wanaojua nini kinaendelea nyuma ya pazia tujulisheni mapema.
   
 2. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Usijali mkubwa huu ndio mkabala wa DECI.

  Naona wamegundua kwamba watanzania wanahela sana hasa dau likiwa dogo.
   
 3. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Fall in share value (price) simply means poor performance of the company or poor rating of the company by shareholders or prospective shareholders. Is important to take not when share value is going down.
   
 4. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani tuwe makini with our recent obssesion with these IPO's...tuwe makini..kuna watu wanasafisha hela sana kutumia hizi vitu...pigeni due dilligence ya crdb before buying anything!!
   
 5. Offish

  Offish Senior Member

  #5
  May 3, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Also take note that CRDB Bank has been hit by ongoing global downturn, as most of its money borrowed by traders in cotton and similar crops could not be paid back as a result of the crisis biting the crops at the world market.
   
 6. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  nasikia kwenye pamba jamaa walitumbukiza zaidi ya 50bn! pagumu hapo.
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Halafu nauliza: ni kwa nini benki kubwa hivi Tz hawana tawi Visiwani? NBC na NMB yapo matawi Pemba na Unguja!

  Hivi watafungua tawi lini Visiwani?
   
 8. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu......Good Question....!!!!
   
 9. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  The thing is, most Tanzanians are naive
   
 10. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  How is the trend like (kupanda na kushuka bei za hisa)?
  Nasikia za NMB zimeanza kushuka. Anyone to confirm this?
   
 11. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  stimulus package ya mkuluu inawalipaa....

  sio mbaya wakifaidi ile 1.7trln..
   
 12. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Unajua kabla mtu hujanunua hisa unatakiwa uongee na mshauri, akuambie maana ya uwekezaji na wakati unanunua hisa unatakiwa uchague makampuni ambayo ynatoa faida kubwa na yanafanya vizuri.

  Wakati wa IPO wa tu wengi walikimbilia kununua kwa hiyo bei lakini waliioomba walikuwa wengi kuliko idadi ya hisa kwa hiyo wakati wa kugawa kila mwanahisa alipata hisa 500ya ulichoomba, baada ya hapo kila mtu kwenye hela yake iliyobaki alipata 35%.

  Kuna aliyeuliza mbona mara ya kwanza ziliuzwa bei kubwa ni hivi, mwanzo waliuziana mashareholder wakubwa kwa bei ya shilingi 600, kwenye IPo walizigawa zile hisa zikawa ndogondogo ili ziwe nyingi ndo wakaziuza kwa sh.150 kwenye Primary Market,
  zilivyoingia sokoni wakaanza na bei ya 200, lakini imeshuka sana mpaka jana ilikuwa 187 sh. kuna oversupply , purchase hamna mpaka jana kwenye trade kuna hisa 22milioni. na wanunuzi haman.
   
 13. M

  Mshika Moja Member

  #13
  Jul 23, 2009
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hisa za NMB zimeshuka hadi kufikia Shs 730 per share. Wakati wanaingia kwenye listing zilianza na bei ya shs 1,200 kwa muda mfupi sana, na tangu hapo zimekuwa zikishuka mpaka hapo kwenye shs 730 !, Hii si habari nzuri sana kwa wadau walionunua hisa kwa wingi hapo NMB, hasa waliokopa ili wawekeze.
   
 14. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Majority do not know when to buy or when not to buy. When to sell and when not.
  80% wanaweza kupanic wakaamua kuuza, halafu baada ya muda bei ikapanda.

  Donald na Kiyosaki wanasema this is not investing but gambling. :)
  They (Donald and Kiyosaki) invest on things they have control over. Pia kwenye security, kwamba huwezi kupata hasara kubwa.
  Mwenye hisa asilimia 51% huyo atakuwa na control.
   
 15. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  zimshuka kwa sababu ya over supply, halafu CRDB waliharakisha sana kuingia sokoni wangetakiwa wawape wenzao muda kwanza wenyewe wangeingia sokoni mwaka kesho.

  Hisa ni nzuri kwa wenye long term plana ambao wanasubiri dividend, lakini kwa wawekezaji wadogo wenye lengo la kuuza na kupata faida wanajazana sokoni ndo wanasababisha soko linashuka. Leo NMB ni 700 inazidi kushuka
   
 16. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kufulia unafikiri ni kwa watu binafsi, hata mabenki yanafulia. Kabla ya kununua lazima ufanye consultation na watu wa uchumi wakuimbishe la sivyo unaingia mkenge bila kujua. Mimi zilinipita hizo hisa sikuwa na hela. Interest nazo ikafa mpaka sasa hivi sina mzuka nazo wasiniingize mjni bure.

  Asante kwa aliyetoa mada, imetusaidia sana.
   
 17. a

  agika JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yes Carol u r right, watu wananunua bila kufanya consultation, kama hizi za CRDB hata mimi niliziacha zipite, coz nilifanya marketing intelligence mtu akanishika sikio akanambia hapo hapafai mama nikarusha kaubawa kangu, ila nilifaidika na zile za NMB coz mie ni short time investor nanunua niuze kwa faida mama watoto waende shule.
   
 18. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  NINAVYOELEWA NI KUWA CRDB WALIUZA SHARE ZAO ZOTE. KWA HIYO HIZI SHARES ZAO ZA SASA HIVI NI SHARE MPYA AMBAZO ZIMETENGENEZWA/KUCHANGANYWA (DILUTED SHARES)

  mchanganyon wa shares (dilution of shares), itakuwa wametoa shares mpya ili kukusanya mtaji wa kuendeshea nakufidia hasara waliyopata, kwa mantiki hiyo shares zitakuwa zimechanganywa na watu wenye shares zao tokea mwanzo zitashuka bei

  mfano CRDB WANA TOTAL SHARE 10M, ALAFU WAMEAMUA KUTENGENEZA SHARE MPYA 5M ILI KUKUSANYA SHILINGI SH 20M KWA AJILI YA UENDESHAJI.
  KAMA ULIKUWA UNAMILIKI 1% YA SHARES (SHARES 100,000) ITAKUBIDI ULIPE TENA SH 2M (1% OF SH 20M) ILI UENDELEE KUMILIKI 1% YA SHARES (SHARES 150,000). KWA HIYO KAMA USIPOTOA HIYO SH 2M, SHARES ZAKO ZITAKUWA ZIMECHANGANYIKA NA HAUTAKUWA UNAMILIKI 1% TENA KAMA ILVYOKUWA AWALI.
  KWA AJILI WAMETOA SHARES ZINGINE ILI KUPATA HELA KWA HIYO SASA HIVI CRDB INA SHARES 15M BADALA YA 10M KWA HIYO SHARES ZAO INABIDI ZISHUKE

  NOTE
  MWANZO TOTAL SHARES 10M , 1% YAKE NI SHARES 100,000
  BAADA YA SHARE MPYA TOTAL SHARES (5+10= 15M), KWA HIYO 1% YAKE NI 150,000. KWA HIYO LAZIMA WASHUSHE BEI YA SHARE KULINGANA NA MTAJI
   
Loading...