Elections 2010 Himizi Watu 5 Jumapili Kwenda Kupiga Kura

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
945
Ndugu zanguni Watanzania, nimekuwa nikifuatilia uchaguzi hapo nyumbani kwa karibu sana. Nimesoma nakala nyingi zinazo husu uchaguzi wa 2010. Sasa tukiwa tumefika kwenye dakika za lala salama ni wazi kabisa mabadiliko yako kwenye ncha zetu za vidole. Mwaka 2010 naufananisha na mwaka 1960 hapo Tanzania ambapo chachu ya kumfukuza mkoloni ilikuwa imepamba moto. Watanzania wengi walijiunga na Mwalimu kuhakikisha kwamba Mkoloni lazima anaondoka. Mwaka huu 2010 pia naufananisha na mwaka 1964 nchi Marekani, ambapo harakati za mageuzi ya siasa za kibaguzi zilipamba moto. Ni mwaka ambao uliazisha mchakato mpya wa kupinga mageuzi na miaka michache badae weusi walikuwa huru.

Ndugu yangu Mtanzania, hivyo basi lazima tufahamu kwamba 2010 sio tuu Dr Slaa Vs Mh. Jakaya Kikwete au CCM vs Chadema, bali 2010 ni present vs future. 2010 ni jiwe la msingi kwa Tanzania ya miaka mingi ijayo, 2010 ndio mwanzo wa safari ndefu ya kuelekea kwenye demokrasia na maendeleo. 2010 ni Mafisadi vs Wananchi. 2010 sio mwaka wa mchezo ndugu yangu, ni mwaka ambao Watanzania wenzetu wa karne zijazo watatujaji na kusema kwamba 2010 ndipo chachu za maendeleo zilipo anzia. Ndugu zanguani 2010 ni mwaka muhimu kuliko tunavyodhani.

Mtanzania mwenzangu, uwe Mkristo, Muislam au Mpagani. Uwe Mchaga, Mmakonde, Mmwera, Mkwere au Msambaa kama mimi ni lazima ukumbuke ya kwamba wote tunashare ADUI mmoja tuu nae ni UMASIKINI narudia nae ni Umasikini. Basi tuweke tofauti zetu nyuma tupigane na huyu adui. Njia ya kumshinda huyu aduni ni kwenye kupiga kura na kuchagua wale ambao watakao shirikiana na sisi kuandaa mbinu za kumpiga adui huyu. Jumapili kura yako itahakiki kwamba Tanzania sio ya kundi la watu fulani, Tanzania sio ya chama fulani, Tanzania sio mali wala hadhina ya kundi fulani, Bali Tanzania inawenyewe na wenyewe ni wananchi wa Tanzania.

Tukumbuke ya kwamba Jumapili sio tuu utakwenda kupiga kura, lakini jumapili utakwenda kuandika HISTORIA mpya kwenye UKURASA mpya. Histori hii itasomwa na vizazi vingi vijavyo, historia hii itasimama kwa karne na karne zijazo. Hivyo wakati tunasogea mwishoni kumbuka ya kwamba Jumapili sio siku tuu kama siku nyingine. Bali Jumapili ni siku ya Historia. Basi, ili hii Historia iwe yenye umuhimu kwa wote, jitahidi kuhimiza wenzio watano kwenda kupiga kura.

Tumia muda wa siku hizi mbili zijazo kuelimisha wenzio umuhimu wa siku ya Jumapili. Waeleze Watanzania wenzako kwamba Jumapili ndio mwisho wa Kuambiwa hakuna dawa ya Umasikini, Jumapili ndio mwisho wa kuambia Hakuna dawa ya Elimu, Jumapili ndio mwisho wa kusikia neno haiwezakani. Na Jumapili ndio hatua ya kwanza ya safari yetu ndefu kabisa ya Maendeleo na demokrasia ya KWELI. Hivyo ni MUHIMU kila Mtanzania akausika kwenye kupiga hatua hiyo.

Ndugu zanguni Watanzania, hakikisha unaelimisha wenzio siku hizi mbili kuhusu umuhimu wa kuhakiki kwamba majina yao yapo kwenye kituo husika. Na mwisho hakikisha siku hii unakwenda kuandika Historia na wenzio watano. Tengeneza timu ya watu watano ambao mtakwenda wote siku hiyo mapema kabisa kukata mzizi wa fitina. Kuwaambia kwamba 2010 ndio mwanzo, kurasa mpya.

Ukweli ni kwamba siku ya Jumapili ni bora kuliko sikukuu yoyote ile Tanzania, kwani siku hii ndio tunakwenda kusherekea mwanzo wa maendeleo kwa WOTE. Na sio maendeleo kwa watu wa Masaki au Raskazone au Kapilipoint au Uzunguni, bali ni maendelo kwa wote hata ndugu zako wa Kisiju, Mkata, Mvuti, Chanika mpaka Wawi.

Ndugu zanguni, Watanzania wenzenu wengi hatupo nyumbani nanyi, lakini tunatazama tukio hili kwa karibu sana, na tunahuzunika kwamba hatuta weka hatua zetu za mwanzo katika kurasa hii mpya kabisa ya maendeleo na demokrasia. Nafahamu kabisa tukio hili litakamilisha njozi za Watanzania wengi sana. Tukumbuke mwisho wa minong'ono ni Jumapili. Kumbuka kuchukua wenzio Watano kuelekea kwenye kituo cha kura, na kama una vijana wadogo waelimisha ya kwamba Jumapili tunakwenda kupanda mbegu mpya ya maendeleo kwa wao na vizazi vijavyo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Watanzania.
 
Back
Top Bottom