Hima hima tujitokeze kwa wingi kujiandikisha

Hima hima tujitokeze kwa wingi kujiandikisha

MLAMBAMWIKO

Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
13
Reaction score
1
Ndugu zangu nawasihi tujitokeze kwa wingi kwenye zoezi linaloendelea la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Tusiishie kuwa kizazi cha walalamikaji tu, kumbuka kuwa kura yako moja ni muhimu mno kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.

Ni lazima pia kuwahamasisha wengine katika zoezi hilo muhimu. Kuna kundi la watu waliokata tamaa na ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura, hawa wasiachwe nyuma bali waendelee kuelimishwa juu ya umuhimu wa kura yao katika maamuzi ya kupata viongozi bora.

ASIBAKI HATA MTU MMOJA MWENYE SIFA YA KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA KUACHA KUTUMIA HAKI YAKE HIYO YA MSINGI.
 
Tatizo siyo wananchi kutojitokeza, tatizo ni tume haina vyombo vya kutosha kuandikisha watanzania wote kwa muda uliobaki.
 
Serikali nayo inaamasisha watu wajiandikishe....haki yao ya msingi...na baadae hawatoi haki hiyo ili watu wajiandikishe kwa wakati. Unajua tume iko mikoa gani na zoezi linaendeleaje? umeshajiadikisha wewe? Kagera na wilaya zake tunasubili....lini watafika hatijui....wakifika office hazifungwi usiku mchana...vifaa havitoki kama watu on cues hawajaandikishwa.
 
hata watu wakijitokeza kwa wingi tume baada muda inawakimbia wapiga kura kwa kisingizio kuwa muda wa kujiandikisha wa siku saba umeisha. hayo yamejitokeza kwenye mikoa yote ambako tume inaandikisha wapiga kura.
 
Unahakika na ulichoandika? UKAWA walikubaliana na hali hiyo maeneo husika? Kama ni kweli wasitegemee ushindi...maana wananchi watakuwa wamegawanywa...waliojiandikisha na wasio....walio watakuwa ccm....na majina mengi ya halufu ya upinzani yatatatolewa. Ni vyema ukawa kulijua hilo....
 
Tujiandikishe kwa wingi ndugu zangu, hiyo ndiyo tiketi pekee ya kuing'oa ccm madarakani.
 
Unahakika na ulichoandika? UKAWA walikubaliana na hali hiyo maeneo husika? Kama ni kweli wasitegemee ushindi...maana wananchi watakuwa wamegawanywa...waliojiandikisha na wasio....walio watakuwa ccm....na majina mengi ya halufu ya upinzani yatatatolewa. Ni vyema ukawa kulijua hilo....

mkuu huo ni ukweli fuatilia tu maeneo yote ambayo tume wamefanya uandikishaji lazima utakuta hayo malalamiko.
 
kwa sasa najua zoezi la kuandikisha linaendela Mtwara, mimi bado sijajiandikisha ila mara waandikishaji watakapofika nitahakikisha najiandikisha. pamoja na changamoto zote tusiache kujiandikisha.
 
ni kweli ndugu lakini pamoja na changamoto hiyo, hakikisha unajiandikisha, ni kukomaa hadi mwisho.
 
hapo ndio watu wanapaswa kukomaa, muda kuisha sio kosa la wananchi bali vifaa vibovu na utaratibu mbovu, tusikubali tuvuliwe haki yetu ya kupiga kura
 
Back
Top Bottom