Norshad
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,224
- 12,622
Habari wandugu,
Nielekee katika swali langu kama linavyojieleza hapo juu,
Kumekuwa na mtukio mengi ya watu kufikwa na mauti wakiwa katika nyumba za wageni, hasa wale wanaofika pale kama wapenzi, vifo hivi mara nyingi vinahusisha zaidi wanaume kuliko wanawake, napenda kufahamu ni nini kinachosababisha hali hii iongezeke mara dufu miaka ya hivi karibuni?
Nitatoa mfano ambapo jana wakati narudi nyumbani nilipita jirani na nyumba moja ya wageni ambapo kulikuwa na tafrani kubwa huku mwanamke akiwa mtupu kama utupu mnavyoujua, yule mrembo alikuwa akiwaka kwamba yule mwanaume aliyeingia naye katika hicho chumba walimokuwepo alikuwa hataki kutumia kinga, na yeye hawezi fanya mapenzi bila kinga hawajuani wamekutana juu juu tu, hivyo akawa analalama kwamba jamaa alitaka kumuingilia kinguvu, ukimsikiliza jamaa sasa ambaye naye alikuwa na taulo tu. Yeye asema yule ni malaya amemchukua kwa dhumuni la kwenda kusuuza nafsi yake.
Shida iliyotokea kule ndani ni kwamba yule mwanamke alikuwa amemuwekea madawa katika chuchu na kinywaji ili jamaa akizima yule mwanamama amuibie asepe na atakachoweza kubeba.
Sasa ile ni trick ya mwanamke mjazia nzi ili aonekane yeye jamaa ndio ana makosa lakini ni kwamba yule malaya ndio alitaka muibia na kwa kuwa ni tabia, ama mozoea ama ndio kazi yake hakuona taabu kutoka nje uchi na kumjazia nzi jamaa, sasa kwa mantiki hii inawezekana vifo vingi vinavyowakuta wazinzi huko katika nyumba za wageni vinatokana na matumizi ya madawa kama haya ya kusizishana ili mwengine atimize lengo lake.
Imefikia stage mtu akiingia na mwanamke gest, alafu ikatokea mwanamke ametangulia kutoka kabla ya aliyeingia nae, husimamishwa mapokezi na kurudishwa mpaka katika chumba walichokuwemo ili kuhakikisha usalama upo wa kutosha.
Je kuna sababu zingine ambazo zinaweza kusababisha kifo ama vifo hasa kwa wanaume huko ktk nyumba za wageni zaidi ya hii ya kuwekewa madawa ama yeye mwenyewe kwa hiyari yake kuchanganya madawa ili aonekane shababi.
Nawasilisha