Hili suala la Benki kuweka wazi taarifa za fedha za mtu kwenye sakata la Mwanza limekaaje?

Nenda Marekani au nchi yoyote ya EU utoe fedha kiasi cha Shilingi (equivalent) milioni 300 halafu uje utuambie jinsi MOVIE ilivyoenda.
Mkuu hapo ni kwamba kama huyo mwenye akaunti hakutoa maelezo ya kutosha basi haruhusiwi kutoa hiyo pesa basi.. lkn kumruhusu afu unawapigia polisi hapo wamekosea tena sana.. Crdb bank

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama walivyosema baadhi ya wengine kwamba tatizo labda ni jina la mtoa taarifa kujulikana. Ila kuhusu benki kuripoti muamala kama huo kwa vyombo husika ipo sahihi kabisa.
Nchi yetu pia ina sheria zinazohusu utakatishaji wa fedha.
Ni wajibu wa benki kutoa taarifa wakitilia shaka muamala wowote ule, iwe kutoa ama kupokea pesa. Yaani ukienda kufanya muamala ambao upo nje ya kawaida yako na benki ikatilia shaka basi inatakiwa kutoa taarifa ya muamala huo, kinyume chake ni kosa.
Kama fedha hizo zingetoka na kwenda kufadhili ugaidi au uhalifu mwingine tungelalamika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hamna mkuu,benki nyingi duniani zinatoa taarifa za mteja kwa vyombo vya usalama inapobidi labda

kwani ukusikia hizo hela zilikuwa zinaenda wapi mkuu

Labda ninavyoelewa kwa kifupi tu...

Kulingana na sheria ya Utakatishaji fedha... (AMLA) ni kweli Benki Wana nafasi yao ya kuripoti muamala wowote Wenye shaka katika akaunti ya mteja na kutoa taarifa kwa ngazi ya juu ndani ya Benki husika.

Lakini pia sheria za fedha na Benki Kuu kiwango cha fedha kikizidi kiasi fulani lazima uwe na mlinzi msindikizaji ambaye ameidhinishwa mfano Jeshi la Polisi, Security Group, G4S nk.

Kosa ambalo kimsingi naliona hapa, kama mtoa tips alitaka usalama wa mteja wake basi alihatarisha Sana maisha ya mteja.. kwa mazingira ya usalama wa baadhi ya askari wetu.
 
Kama walivyosema baadhi ya wengine kwamba tatizo labda ni jina la mtoa taarifa kujulikana. Ila kuhusu benki kuripoti muamala kama huo kwa vyombo husika ipo sahihi kabisa.
Nchi yetu pia ina sheria zinazohusu utakatishaji wa fedha.
Ni wajibu wa benki kutoa taarifa wakitilia shaka muamala wowote ule, iwe kutoa ama kupokea pesa. Yaani ukienda kufanya muamala ambao upo nje ya kawaida yako na benki ikatilia shaka basi inatakiwa kutoa taarifa ya muamala huo, kinyume chake ni kosa.
Kama fedha hizo zingetoka na kwenda kufadhili ugaidi au uhalifu mwingine tungelalamika?

Sent using Jamii Forums mobile app
But utoaji wa taarifa ya suspecious transaction mboa unatumia form maalum na lazima ufike kwa immediate supervisor kwa maamuzi lakini hilo jambo mbona kama limechukua muda mfupi..
 
Hela si za kwake, wakati anazileta mpka kuwa nyingi mbona hawakumtilia shaka na kureport au kumkataza. Kutoa dio imekuwa shidah na amesema anaenda kununua nini.
Hata angetaka kuhonga bado alikuwa na haki
 
Aisee, MI bado sijaelewa..
Yaani walitilia shaka muamala, it's ok jibu hapa Ni wasingempa mpaka watakapojiridhisha... Sasa, swala la wao kumpa 300M then kumpigia mkuu Wa mkoa kwamba kuna jamaa kavuta mzigo wa maana hapa.. Hapo ndio pale napopata mashaka sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kwanini RC na sio Mkuu wa polisi?? Kuna kanamna hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtu anapoenda kununua madini,haendi na sh laki moja,na jamaa aliulizwa akasema anakwenda kununua madini na hiyo ndo taarifa,bank wanaweza kuwa walitimiza utaratibu tu wa kutoa taarifa kuwa mtu fulani katoa bank kiasi fulani,then hawa jamaa wakaitumia taarifa kuwatarget hao kama kwamba wamehalifu
 
Bank teller naye aunganishwe,kwa nini aruhusu fedha hiyo kutoka ata kama alitahadharisha..Somebody is Spy in that Branch..Hapo ndio utafahamu kwa nini watu wengine wanajenga Ngome..
Mara nyingi kama si zote managers wa bank kubwa kubwa huwa nao ni Chain ya system tu, Credibility hakuna kabisa sasa hawa wana expect kufanya zaidi biashara ile hali wanashindwa kumlinda mteja, Haya toeni taarifa kwa siri inapobidi na haina haja ya ku expose kama walivyofanya kwanza wasingekubali hata kuwa quoted na hao Politicians RC na RPC
 
Bank nyingi za bongo ovyo sana ndo maana mimi siweki ela zaidi ya milioni 10 kwenye account moja maana najua shida yake.Ata hivyo hao jamaa nao haziwatoshi wamewezaje kusafirisha mzigo wote huo wa pesa na madini wakati hali ya nchi ilivyo wanaiona.au bado kuna watu vichwa vyao viko gizani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom