kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,793
- 5,042
Nina rafiki yangu kila mwanamke anayenisumbua kwake anampata kirahisi sana. Mara ya kwanza nilipata mwanamke karibu na nyumbani kwake pale. Mwanamke huyo alinipenda, siku ambayo nilimkutanisha na jamaa yangu, huyo mwanamke akaanza kuomba sijui namba ya simu, mimi nikaona labda ushemeji. Baada ya siku kadha, nikasikia wanatoka. Nilipaniki sana ila mwisho nilipotezea.
Kuna mwanamke mwingine ambaye tulikuwa tunasoma naye, mwanamke huyo nilimtongoza, alinisumbua sana ila mwisho alikuja kukubali. Kuna siku nilikuwa naongea naye, huyo jamaa yangu akapita hapo. Mwanamke alikuwa kama amepagawa, akawa ananiuliza kama yule ni rafiki yangu, nikamwambia ndiyo, baada ya siku kadhaa nikasikia wanatoka tena!
Nilimfuata jamaa kwa hasira, ila alinipa mwishowe nilikubali matokeo tu. Kuna mwanamke mwingine nilikuwa kwenye harakati za kutaka kumtongoza, jamaa akasema yeye tayari ameshaongea na amesha kubali, nikabaki na shangaa sasa.
Ila huyu wa mwisho nasema na liwalo na liwe, sikubali tena kuwa kinyonge. Kuna mwanamke tunafanya naye kazi, sasa mwanamke huyo kwasasa nina miezi mitatu namfukuzia, bado mtoto wa kike ajatoa jibu kamili.
Ila juzi yeye jamaa alikuwa amenifata kazini kwetu. Kwa bahati mbaya akakutana na mwanamke anatoka ndani ya kazi, mimi nilikuwa bado nipo ndani. Jamaa alivyomuona mwanamke huyo akamuomba namba zake za simu na tayari ameshapewa.
Ila mimi nina miezi mitatu sina namba yake, najaribu kuomba lakini mtoto wa kike anakataa. Yeye amepewa kirahisi sana. Sijamwambia kama yule ni mwanamke ambaye mimi namfukuzia, ila yeye ndiyo ameniambia kuwa pale kazini kwetu kuna mwanamke tayari yupo kwenye anga zake, alikutana naye kazini kwetu pale.
Na ninavyojua atakuwa ni yeye tu, hakuna mwingine. Pamoja na kubisha najua ni lazima jamaa atatafuna tu. Mimi kinachonipa msongo wa mawazo ni kujiuliza jamaa yeye ana damu ya namna gani mpaka apendwe na wanawake wote wanaonisumbua?
Kimuonekano mimi mzuri kuliko yeye, sasa sijui shida nini hasa!