Hili ni kwa watalamu wa Ving'amuzi na Satelite Dishes, ufafanuzi tafadhali!

Wakuu kuna vitu vinanichanganya sana, naombeni ufafanuzi kidogo kabla sijaingia mkenge. Kuna receivers ambazo ni MPGE4 compatible na MPGE2 ambayo ndiyo mimi natumia(Mediacom 930+). Tatizo ninaloona ni kwamba ina uwezo mdogo sana kwenye kutapata channels hasa fta. Kuna mtu aliniambia kwamba kuna fta channels nyingi ambazo ningeweza kutapa ikiwa receiver yangu ingekuwa na uwezo wa MPGE4. Hapo hapo kuna jamaa yangu alitoka Finland na receiver ambayo ni MPGE4 lkn mpaka sasa mafundi wetu wameshindwa kuinstall, imekaa tu ndani kama pambo.

Ombi langu nahitaji kujua yafuatayo:

1. Je, ni kweli kwamba MPGE4 na MPGE2 zina tofauti, na kwa kiasi gani?
2. Je, ikiwa MPGE4 inaweza kushika fta channel, maximum hapa kwetu naweza kupata ngapi?
3. Je, hiyo MPGE4 nayo itatumia satelites hizi tunazotumia kwenye MPGE2?
4. Nasikia kuna baadhi ya receivers zina uwezo wa kufungua scrambled channels,je hiyo inawezekana?

Mtanikosoa kama nitakuwa nimekosea vitu kadhaa hapo juu kwani mimi sio mtalamu wa mambo haya.

Nawasilisha....

Huyo rafiki yako yupo anapatikana wapi na majibu ya mafundi baada ya kushindikana yalikuwa yapi?
 
Je Unaweza kupata Citizen tv bila kupoteza Aljazeera,Emmanuel,CTL,NOOLYWOOD na MUVI TV?? Anayepata tafadhali nijuze nini cha kufanya. Kwenye Ku Citizen inasumbua sana,SIGNAL YAKE HAITULII, wakt mwingine ipo 54 ambayo ni bora,lkn wakt mwingne inashuka na kuwa 50-48 which isn't stable at all.
 
Je Unaweza kupata Citizen tv bila kupoteza Aljazeera,Emmanuel,CTL,NOOLYWOOD na MUVI TV?? Anayepata tafadhali nijuze nini cha kufanya. Kwenye Ku Citizen inasumbua sana,SIGNAL YAKE HAITULII, wakt mwingine ipo 54 ambayo ni bora,lkn wakt mwingne inashuka na kuwa 50-48 which isn't stable at all.

jaribu kuinua dish lako kama sm 1 au 1.5 wakati unaangalia signal ya chanel za bongo hasa star tv isishuke sana.
 
kuifuata deg 62 hata hiyo citizen iko intelsat 902 @ 62e ukifuata sana unapata Qtv na NTV kama una mpeg4

mimi kifurush cha EmmanuelTV, MuviTV kipo sawa ila cha EWTN, CtL, Nollywood Zinakatakata sana tatizo nini wakat ni LNB moja hiohio, nitatue vp hapo?
futi 6 dish
 
mimi kifurush cha EmmanuelTV, MuviTV kipo sawa ila cha EWTN, CtL, Nollywood Zinakatakata sana tatizo nini wakat ni LNB moja hiohio, nitatue vp hapo?
futi 6 dish

nolly ndio hazisumbui jaribu kuzungusha lnb yako (lnb Skew)
 
me natumia receiver ya strong MPGE-4, ninapata channels kibao sana.....ila ni kweli mara nyingine inasumbua kupata signal mpaka umpate fundi mtaalam sana
 
Wakuu sema bongo yetu net ya kusua sua sana, kama mngekuwa mnaweza au hamtumii package kwa ajili ya internet i mean ni unlimited then kuna box linaitwa Maxx100 na unaweka na dish lako nje sio kubwa sana la kati tu linatosha, then hilo box una connect kwenye net , basi hutoenda enda baa tena kupigizana kelele na mtu, kama EPL wanacheza timu sita kwa siku then zote unazipata unachagua, ila lazima box liwe connected kwenye internet maana saa zingine key zinakuwa blocked then lenyewe box kupitia ile net yako zina ji un block huna haja ya kwenda kwenye internet na kuangalia key...ninalo hilo box kwa miaka 3 sasa silipiii na wala sijawahi kusumbuka nalo hata kidogo na hata kukiwa na champions mipira yote napata, so napendekeza kama wadau mnaweza.


Gharama za box na dish lake zikoje? Gharama za internet nazo zikoje compared na gharama za malipo ya kawaida?
 
Back
Top Bottom