Hili ndio jipu sugu ambalo Magufuli hatoweza kulitumbua mpaka anamaliza muda wake

abuu muhammad

Senior Member
Jul 29, 2015
161
39
Misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini imekuwa ikiipotezea serikali mabilioni ya pesa. Taasisi za dini inatumia mwanya huu kufanya biashara. Kuna taasisi moja iliwahi kuagiza gari aina ya V8 kwa ajili ya mfanya biashara mmoja mkoani Tanga.

Kuzingatia hili serikali ya awamu ya 4 iliwahi kupeleka azimio la kufuta misamaha hii ya kodi wakati huo waziri wa fedha akiwa Mustafa Mkulo, taasisi za dini za kikristo wakiongozwa na Pengo walilipinga hili kwa nguvu zao zote hadi serikali ikasalimu amri.

Kwa mantiki hii taasisi hizi za kikristo zinanufaika sana na misamaha ya kodi na zinahusika sana na suala la kuikosesha mapato mengi serikali, hili ni jipu ambalo JPM hatoweza kamwe kulipasua kwani yy mwenyewe anaogopa hata kuliangalia na hata kulikaribia hatoweza. La kujiuliza ni nani atakaeweza kumwambia rais kuna jipu hili lahitaji kutumbuliwa? Ni waziri wa fedha?

Ni waziri mkuu? Je Magufuli mwenyewe hajui kuwa hili ni jipu? Au tatizo ni kuwa viongozi wake wa dini wananufaika?
 
Last edited by a moderator:
Misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini imekuwa ikiipotezea serikali mabilioni ya pesa. Taasisi za dini inatumia mwanya huu kufanya biashara. Kuna taasisi moja iliwahi kuagiza gari aina ya V8 kwa ajili ya mfanya biashara mmoja mkoani Tanga. Kuzingatia hili serikali ya awamu ya 4 iliwahi kupeleka azimio la kufuta misamaha hii ya kodi wakati huo waziri wa fedha akiwa Mustafa Mkulo, taasisi za dini za kikristo wakiongozwa na Pengo walilipinga hili kwa nguvu zao zote hadi serikali ikasalimu amri,
Kwa mantiki hii taasisi hizi za kikristo zinanufaika sana na misamaha ya kodi na zinahusika sana na suala la kuikosesha mapato mengi serikali, hili ni jipu ambalo JPM hatoweza kamwe kulipasua kwani yy mwenyewe anaogopa hata kuliangalia na hata kulikaribia hatoweza. La kujiuliza ni nani atakaeweza kumwambia rais kuna jipu hili lahitaji kutumbuliwa? Ni waziri wa fedha? Ni waziri mkuu? Je Magufuli mwenyewe hajui kuwa hili ni jipu? Au tatizo ni kuwa viongozi wake wa dini wananufaika?

Huo msamaha wa kodi ni kwa taasisi za dini zote au ni kwa dini za kikristo tu maana uzi wako inaonesha msamaha wa kodi unazihusu taasisi za dini ya kikristo tu
Au mleta uzi unachuki na dini tajwa?
 
Wewe unafikiri kwanini serikali inashindwa kuifuta hiyo misamaha ya kodi,au unafikiri ni kwa kuwa tu viongozi wa dini wanapiga kelele hizo unazosema?
 
Ban requeat sent to moderators.... this stupid religious biases can not be tolerated.... misamaha ya kodi ni kwa mashirika yte ya kidin siyo wakristo tu....

Please ban huu uzi melo, inviisible and etc
 
Misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini imekuwa ikiipotezea serikali mabilioni ya pesa. Taasisi za dini inatumia mwanya huu kufanya biashara. Kuna taasisi moja iliwahi kuagiza gari aina ya V8 kwa ajili ya mfanya biashara mmoja mkoani Tanga. Kuzingatia hili serikali ya awamu ya 4 iliwahi kupeleka azimio la kufuta misamaha hii ya kodi wakati huo waziri wa fedha akiwa Mustafa Mkulo, taasisi za dini za kikristo wakiongozwa na Pengo walilipinga hili kwa nguvu zao zote hadi serikali ikasalimu amri,
Kwa mantiki hii taasisi hizi za kikristo zinanufaika sana na misamaha ya kodi na zinahusika sana na suala la kuikosesha mapato mengi serikali, hili ni jipu ambalo JPM hatoweza kamwe kulipasua kwani yy mwenyewe anaogopa hata kuliangalia na hata kulikaribia hatoweza. La kujiuliza ni nani atakaeweza kumwambia rais kuna jipu hili lahitaji kutumbuliwa? Ni waziri wa fedha? Ni waziri mkuu? Je Magufuli mwenyewe hajui kuwa hili ni jipu? Au tatizo ni kuwa viongozi wake wa dini wananufaika?

Pamoja na kwamba umeonesha bias kwa dini za ki-Kristo, lakini naomba nikueleweshe tu kwamba taasisi hizi ni wadau wakubwa wa serikali kwenye swala zima la kutoa huduma za kijamii kama vile Elimu & Afya! Serikali itakapoweza kujizatiti kutoa huduma hizo kwa utoshelevu kwa walipa kodi wao, basi itakuwa pia na jeuri ya kubana misamaha husika ya kodi! Kwamba kuna ubadhirifu kwenye misamaha kwa baadhi ya taasisi ni jukumu la serikali kuthibitisha hilo na kuchukua hatua stahiki za kisheria! Unapokuwa na serikali dhaifu, basi mianya ya ubadhirifu nayo inakuwa mingi!
 
Huo msamaha wa kodi ni kwa taasisi za dini zote au ni kwa dini za kikristo tu maana uzi wako inaonesha msamaha wa kodi unazihusu taasisi za dini ya kikristo tu
Au mleta uzi unachuki na dini tajwa?
Ukiuliza hili watakiwa ueleze na ww kwani serikali ilipotaka kufuta hii misamaha ya kodi ililenga taasisi za kikristo pekee? Mbona wao ndio waliokuja juu na kutoa makaripio makali kwa serikali?
 
Pamoja na kwamba umeonesha bias kwa dini za ki-Kristo, lakini naomba nikueleweshe tu kwamba taasisi hizi ni wadau wakubwa wa serikali kwenye swala zima la kutoa huduma za kijamii kama vile Elimu & Afya! Serikali itakapoweza kujizatiti kutoa huduma hizo kwa utoshelevu kwa walipa kodi wao, basi itakuwa pia na jeuri ya kubana misamaha husika ya kodi! Kwamba kuna ubadhirifu kwenye misamaha kwa baadhi ya taasisi ni jukumu la serikali kuthibitisha hilo na kuchukua hatua stahiki za kisheria! Unapokuwa na serikali dhaifu, basi mianya ya ubadhirifu nayo inakuwa mingi!
Sijaonyesha bias ila kwenye taasisi za kikristo nilisema kuonyesha kuwa wao ndio ambao walikuja juu sana, jambo linaloeleweka kuwa taasisi za dini hata za kiislamu zinatumia huu mwanya,
 
Misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini imekuwa ikiipotezea serikali mabilioni ya pesa. Taasisi za dini inatumia mwanya huu kufanya biashara. Kuna taasisi moja iliwahi kuagiza gari aina ya V8 kwa ajili ya mfanya biashara mmoja mkoani Tanga. Kuzingatia hili serikali ya awamu ya 4 iliwahi kupeleka azimio la kufuta misamaha hii ya kodi wakati huo waziri wa fedha akiwa Mustafa Mkulo, taasisi za dini za kikristo wakiongozwa na Pengo walilipinga hili kwa nguvu zao zote hadi serikali ikasalimu amri,
Kwa mantiki hii taasisi hizi za kikristo zinanufaika sana na misamaha ya kodi na zinahusika sana na suala la kuikosesha mapato mengi serikali, hili ni jipu ambalo JPM hatoweza kamwe kulipasua kwani yy mwenyewe anaogopa hata kuliangalia na hata kulikaribia hatoweza. La kujiuliza ni nani atakaeweza kumwambia rais kuna jipu hili lahitaji kutumbuliwa? Ni waziri wa fedha? Ni waziri mkuu? Je Magufuli mwenyewe hajui kuwa hili ni jipu? Au tatizo ni kuwa viongozi wake wa dini wananufaika?

Tatizo unaandika kwa kubahatisha! Kama taasisi za dini zinasamehewa kodi kwa mujibu wa sheria na kwa kuisaidia serikali kutoa huduma za jamii, shida iko wapi?! Kwanza unatakiwa utambue walioweka hiyo sheria hawakuwa na mihemko kama wewe, ni watu werevu waliofanya tathmini kwa kushirikiana na serikali ndo wakafikia huo msimamo!

Kama kuna watu wanapenyeza bidhaa zao kupitia mgongo wa dini kama unavyosema kuhusu huko Tanga, hilo ni swala la ukiukwaji wa taratibu! Hapo sheria inatakiwa ichukue mkondo wake na hiyo taasisi iwajibishwe, lakin sio kusema kwa kuwa kuna taasisi ilikiuka taratibu ndo zote ziazibiwe kwa kosa la mmoja!

Wakwepa kodi ndani ya hii nchi wamelelewa na serikali yenyewe kupitia viongozi wetu! Hizo container 11,884 sijui kama kuna ngapi za taasisi za kidini!! Tatizo la hii nchi sio dini, ni CCM! Jipu kubwa kuliko yote ni CCM na mfumo wake, hili jipu ndo ambalo JPM hatoweza kulitumbua, maana kwanza tayari ameshasombwa na mfumo wenyewe, na tayari ameshageuka jipu! Yeye na watendaji wake watabweka usiku na mchana! Kwa ushauri wangu, ikiwa JPM anataka kuwa raisi mwenye maamuzi arudishe rasimu ya Warioba na aitumie kutawala TZ! Mbona mambo yatakuwa sawia kabisa?! Kinyume na hapo, tutegemee maigizo na matamko kila kukicha!

Maana kuna mawaziri wengine wamekosa tamko wanajisemea lolote linalokuja ili mradi tu wasikike! Mfano waziri anaposema eti vituo vya radio na tv vicheze miziki ya ndani 60% yeye ndo anawalipia kodi! Haya ndo maigizo yenyewe na tayari hili ni jipu!!

Wasalaam....!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ukiuliza hili watakiwa ueleze na ww kwani serikali ilipotaka kufuta hii misamaha ya kodi ililenga taasisi za kikristo pekee? Mbona wao ndio waliokuja juu na kutoa makaripio makali kwa serikali?
Mmejipangaje kushindana na shule za kanisa kwenye ufaulu? mkumbuke yule Dr Nadlichako kwa sababu ni msomi Rais amemteuwa kuwa waziri wa elimu. wewe kalia porojo tu sisi tunaongeza mashule, mahospital na vyuo vikuu, nyinyi ongezeni madrasa tu majibu mtayapata
 
Misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini imekuwa ikiipotezea serikali mabilioni ya pesa. Taasisi za dini inatumia mwanya huu kufanya biashara. Kuna taasisi moja iliwahi kuagiza gari aina ya V8 kwa ajili ya mfanya biashara mmoja mkoani Tanga. Kuzingatia hili serikali ya awamu ya 4 iliwahi kupeleka azimio la kufuta misamaha hii ya kodi wakati huo waziri wa fedha akiwa Mustafa Mkulo, taasisi za dini za kikristo wakiongozwa na Pengo walilipinga hili kwa nguvu zao zote hadi serikali ikasalimu amri,
Kwa mantiki hii taasisi hizi za kikristo zinanufaika sana na misamaha ya kodi na zinahusika sana na suala la kuikosesha mapato mengi serikali, hili ni jipu ambalo JPM hatoweza kamwe kulipasua kwani yy mwenyewe anaogopa hata kuliangalia na hata kulikaribia hatoweza. La kujiuliza ni nani atakaeweza kumwambia rais kuna jipu hili lahitaji kutumbuliwa? Ni waziri wa fedha? Ni waziri mkuu? Je Magufuli mwenyewe hajui kuwa hili ni jipu? Au tatizo ni kuwa viongozi wake wa dini wananufaika?
 
Pamoja na kwamba umeonesha bias kwa dini za ki-Kristo, lakini naomba nikueleweshe tu kwamba taasisi hizi ni wadau wakubwa wa serikali kwenye swala zima la kutoa huduma za kijamii kama vile Elimu & Afya! Serikali itakapoweza kujizatiti kutoa huduma hizo kwa utoshelevu kwa walipa kodi wao, basi itakuwa pia na jeuri ya kubana misamaha husika ya kodi! Kwamba kuna ubadhirifu kwenye misamaha kwa baadhi ya taasisi ni jukumu la serikali kuthibitisha hilo na kuchukua hatua stahiki za kisheria! Unapokuwa na serikali dhaifu, basi mianya ya ubadhirifu nayo inakuwa mingi!
Hili jambo haliingia akilini, eti serikali ishindwe kutoa huduma hizo lakini taasisi za dini ziweze wakati taasisi hizo hizo za dini zinatumia misamaha ya kodi halafu huduma za afya na kielimu ktk taasisi hizo zipo juu sana.
 
Kama sijakosea bajeti ya 2015/16 ilifuta misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini. Hili limekuwa ni chaka la wafanyabiashara wengi kuingiza biashara zao kupitia taasisi hizi
 
Only in Tanzania. Hatuwez kuishi kwa kutegemea miundombinu ya Taasisi za dini. Ifike mahali Taasisi hizi zilipe kodi. Favor waliyopatiwa inatumika ndivyo sivyo. Kwa hakika hili ni jipu sawa na mengi mengine,litumbuliwe mbali! Naamini serikali yenyewe ina uwezo wa kutoa huduma bora kwa raia wake. Tuache propaganda kuwa Taasisi za dini ndiyo msaada mkubwa. Huo ni uongo sema tu labda serikali imeamua kuwapa favor lakini la kusema ni mchango mkubwa kwa Taifa ni kuendekeza mambo bila tija na mwishowe kunufaisha wachache.
 
Mmejipangaje kushindana na shule za kanisa kwenye ufaulu? mkumbuke yule Dr Nadlichako kwa sababu ni msomi Rais amemteuwa kuwa waziri wa elimu. wewe kalia porojo tu sisi tunaongeza mashule, mahospital na vyuo vikuu, nyinyi ongezeni madrasa tu majibu mtayapata
Na zile figisu figisu za ndalichako kule necta unazisemaji? Pamoja kuwa nakubali kuwa ni msomi, ila usomi wake uwe kwa manufaa ya wananchi wote
 
Abuu Muhammad unatakiwa ufanye utafiti vizuri kuanzia July2015 mashirika ya kidini yanalipa VAT na kodi zingine sema kuna vitu vichache sana ndo bado vinapewa msamaha .... sasa labda kama tatizo lako ni udini tuambie
 
BAKWATA walikuwa wanapitisha Semi Trailers pale Bandarini bila kulipia kodi....

Sasa sijui zilikuwa zinatumika kusafirisha misaafu au Majamvi ya misikitini...
 
Abuu Muhammad unatakiwa ufanye utafiti vizuri kuanzia July2015 mashirika ya kidini yanalipa VAT na kodi zingine sema kuna vitu vichache sana ndo bado vinapewa msamaha .... sasa labda kama tatizo lako ni udini tuambie
Hapana mkuu, tatizo langu si udini. Tatizo langu misamaha hii iondolewe
 
Back
Top Bottom