Hili ndilo tatizo la Zitto Kabwe

Nikusumulie.. umejuaje ni mako... unayojidai kuyaita huku 💉💉💉 zimekuingia muruwaaaaa
nina makengeza ya macho aise maana naona maneno yanaenda mbele na kurudi nyuma ndiyo nikaomba msaada kutoka kwako maana umemaliza yote inaonekana umeingiza kitu kichwani kwako.
 
Hebu atusaidie kufafanua haya yaliyotendwa na upande anaouamini
1.Polisi walitueleza watu wangapi waliuawa wakati wa Operesheni Tokomeza na je, taarifa yao ilikuwa sahihi?
2.Alipouawa Imran Kombe Tuliambiwa ni jambazi, je, ni kweli DG wa TISS mstaafu alikuwa amegeuka jambazi baada ya kuataafu?
3.Vijana wafanyabiashara wa Mahenge akina Chigumbi waliuawa kwa maelekezo ya RCO DSM Zombe, tukaambiwa waliouawa na majambazi hatari waliompora Mhindi. Ilipoundwa Tume ya kimahakama kuchunguza sidhani kama ukweli uliendelea kuwa huo, labda atueleze yeye.
4.Wabunge walipopiga kelele bungeni kuhusu Korosho walitishiwa kupigwa wao na shangazi zake Waziri Mkuu, lakini wakulima wakagoma kuuza korosho zao kwa hasara, mpaka sasa sijajua Nani alikuwa sahihi, Wabunge au Mpigashangazi?
5.CAG alipotoa ripoti ya kutoonekana 1.5T walijitokeza mawaziri kukanusha na mwingine akamsimamisha CAG hadharani akanushe ripoti yake. Juzi tumeambiwa utaratibu uliotumika awali kuzima hoja ya CAG haukuwa sahihi. Hapa napo sina hakika Nani alikuwa sahihi?
 
mi sasa hivi nikisikia huyu ni prof. wa udsm.. na nikisikia mtu ni polisi automatically imani juu yake inapotea.......
 

Akikujibu swali lolote kati ya haya uliyouliza na ukaridhika naomba uni-tag mkuu.
 
Na wewe mbona unajifanya unajua sana?
 
Weka na namba yako ya simu kwa ajili ya taarifa ya uteuzi
 
Nchi hii Ukijua sheria mtu akuonei, na woga unakuwa una zitto ni miongoni atawasumbua na mahakamani atashinda na ajua kujenga hoja
 
Usicho kijua bora kukaa kimya kuliko kuongea usilo lielewa
 
Yale ya Chuo kikuu ni upuuzi wa kisomi.
 
Mtoa mada nakupongeza kwa mada yako umeongelea juu juu kuhusu ujuaji wa mh zito bila kuweka data .ukosefu wa data unakunyima credit ya hoja yako nchi Kwanza chama badae
 
Pamoja na weaknesses zake Zitto ni kati ya watu wanaojua kujenga hoja na anajiamini sema kwa akili ya watanzania na St. Kayumba zetu ni vigumu kumuelewa.
Hata aliposema tshs 1.5 ripoti ya CAG zinaonekana zimepigwa kuanzia mawaziri, mwenye nchi mpaka bwana slo slow wote walimshikia bango, lakini jana CAG mwenyewe kathibitisha kuwa Gavana wa BOT na yeye wameitwa mbele ya kamati ya PAC kuhsu hilo suala.
Zitto Kichwa sana aisee
 
Kweli mkuu Zitto ni tofauti na wasomi wengi wa nchi hii jamaa anajua mambo mengi na uelewa wake ni watofauti maana hata mwenye nchi alisoma ripoti hakuona tshs 1.5 tilion kuwa hazionekani ila jana GAvana wa BOT na CAG mwenyewe wameitwa mbele ya kamati ya bunge ya PAC kuhusu hilo swala.
 
Nashukuru MUNGU sijasoma maana ningesoma ningeishia kumtukana tu.
 
Yaani afadhari hata usingewataja maprofesa maana ndo wamejipotezea heshima yao kabisa!
 
Kama anayosema MTU mmoja Zito Kabwe,siyo ya kweli,kwanini serikali inatumia nguvu na hila kumnyamazisha,??si mjibu hoja zake tu,kuliko kutusomea takwimu nyiiiingi,
Lile kongamano,halina tofauti na mkutano wa kisiasa wa CCM,Waziri kabudi alikuwa anatiririka matakwiiiimu mengi yasiyo na maana kwa mwananchi wa kawaida,
Kama anayosema Zito ni ya uongo,wekeni ukweli wenu,kwa hoja,siyo kutunga sheria za kuzuia watu wasiseme,muawaache waseme,nyie leteni ukweli wenu.
Vijana waliochangia kwenye kongamano lile na wao,ni bure kabisa,wanaendekeza njaa tu,MTU anasimama,anasema yeye alikuwa kiongozi hapo UD,akiongoza umoja wa vijana wa CCM!!!,sasa hii inamsaidia nini anayesikiliza,zaidi ya kuwa ni gia za kutafuta kuonekana na chama na serikali ili wapate uteuzi!!!,njaa tupu,
Simama,sema Mimi mhitimu wa UD,kozi Fulani ya uhandisi,Nina Kampuni,nimefanya hiki,natatua hiki..,sio kuleta story za kibishoo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…