Hili Ndilo Neno La Mama Salma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili Ndilo Neno La Mama Salma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TandaleOne, Sep 9, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Anayependa maendeleo atatambua mafanikio ya serikali-Mama Salma

  NA JACQUELINE LIANA, BAGAMOYO

  MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, amesema mtu anayependa maendeleo nchini, atatambua mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne.

  Akizungumza kwa nyakati tofauti na wanawake wa wilaya za Kibaha, Chalinze na Bagamoyo, mkoani Pwani jana {24.8.2010}, alisema mengi yaliyoahidiwa na Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2005, yametekelezwa.

  Mama Salma Kikwete alisema, katika suala la maendeleo na mustakabali wa nchi, ni lazima wanawake waangalie ni chama gani chenye sera na ilani makini, katika kuwaletea maendeleo yao, na jamii yote ya Watanzania.

  Alitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho kuwa ni ujenzi wa shule za sekondari za kata, zilizoondoa tatizo la watoto wanaofaulu na kushindwa kuendelea sekondari kwa kukosa nafasi.

  Mama Salma alisema, ujenzi wa shule za sekondari umeongezeka kutoka 1,745 hadi 4,102 katika kipindi cha miaka mitano, jambo ambalo ni mafanikio makubwa, lakini kuna watu wanaojifanya kutoyaona.

  Kutokana na kuongezeka kwa shule hizo, alisema idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka ambapo uandikishaji wa kidato cha kwanza hadi cha nne ulitoka kuwa wanafunzi 401,598, mwaka 2005, hadi 1,401,559 mwaka 2009.

  Kuhusu miundombinu, alisema ujenzi wa barabara zinazounganisha mikoa na wilaya nchini umewezesha wananchi kusafiri kwa haraka kutoka sehemu moja ya nchi kwenda nyingine, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa huko nyuma.

  "Zamani ilikuwa kutoka hapa (Kibaha), hadi Lindi tulilazimika kulala njiani, lakini sasa mambo ni mazuri," alisema na kupigiwa kofi.

  Alisema, Chama Cha Mapinduzi kimetekeleza ilani yake kwa mafanikio makubwa, na asiye na macho haambiwi tazama, kwani wengine wanaona mafanikio hayo lakini wanajifanya hawaoni," alisema.

  Mama Salma aliwaomba kina mama hao kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu katika mtindo maarufu wa CCM wa mafiga matatu.

  "Siku ya tarehe 31 mwezi wa kumi, ukifika kituoni piga kura kwa mgombea urais wa CCM, mgombea ubunge wa CCM na mgombea udiwani wa CCM hayo ndiyo mafiga matatu," Alisema.

  Akizungumzia kura za maoni za CCM kuwapata wagombea ubunge na udiwani, Mwenyekiti wa WAMA alisema, zilisababisha makundi tofauti kwa sababu wagombea walikuwa ni wengi.

  Kwa vile mchakato huo umemalizika na wagombea kupatikana, aliwasihi wanachama wa CCM kuvunja makundi hayo na kuwa na kundi moja la CCM kwa ajili ya kukipatia Chama Cha Mapinduzi ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.

  Kesho, (Agosti 25, 2010) Mama Salma Kikwete ataendelea na ziara ya kuzungumza na wanawake katika wilaya za Kisarawe, Mkuranga na Rufiji, na Agosti 26, 2010 anatarajiwa kuwa Mafia.

  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx  'Zingatieni masharti mikopo isaidie wengi'

  *Ni kauli ya Mama Salma kwa kinamama

  God Bless Our Country and protect it from liars,disorganized and crazy people

   
 2. dkims

  dkims Senior Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  so?????????
   
 3. S

  Safre JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katiba inamtambua huyu mama kama mwanasiasa au mke wa rais anaeomba ridhaa ya wananchi tena?
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu Mama alishawahi kutembelea zile shule za msingi alizokuwa anafundisha? Natumaini HAPANA - vinginevyo asingethubutu kutamka hayo maneno!

  BTW: Haya majengo (mengine hayana hata madirisha) yanayopewa jina "shule za kata" ni SHULE kweli?
   
 5. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Unamjua Michelle Obama????Na yule aliyepandishwa jukwaani na magwanda??Hii forum sijui inakuwaje.Mnaongelea watu badala ya ujumbe.Kweli waafrika.
   
 6. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Fuatilia utajua kama kweli unataka kujua aliwahi kutembelea au la.Wanafunzi wangapi wameenda form 5 na 6 kutoka shule za kata???Jiulize hilo swali.Acha ubinafsi.Kama si hizo shule wangekuwa wapi???Hakuna msomi makini asiyejua mapigano ya nchi masikini kutoka katika umasikini wake hupitia nyakati zipi.Nyakati za maopportunists na manabii wa uongo wa kisiasa ambao wanatupa mema yote na kusimama kusema mabaya kwa nguvu zao zote.Ila umma makini huwatambua.
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine ni busara kumuongelea mtu aliyetoa ujumbe kabla ya kuzama katika ujumbe wenyewe.
   
 8. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Wakati mwingine ila si wakati wote.
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Tandale

  Takwimu ya Salma hii hapa:

  Takwimu ya waliofanya mtiahani Form SIX 2010 kutoka NECTA hii hapa:
  Kama kujiandikisha Form I-IV umefikia 1.5mil sasa inakuwaje wanaomaliza Form VI hawafiki hata 100,000?
   
 10. dkims

  dkims Senior Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  [

  Takwimu ya waliofanya mtiahani Form SIX 2010 kutoka NECTA hii hapa:


  Kama kujiandikisha Form I-IV umefikia 1.5mil sasa inakuwaje wanaomaliza Form VI hawafiki hata 100,000?[/QUOTE]

  u gat a point?? kuna uongo hapo, au na yeye anpewa takwimu za uongo kama mume wake??????????
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Matokeo ya 2009/10 ya Shule Za KATA kwa Mkoa wa Dar es Salaam:

   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mbona alishaanza!! Siku mme wake ameanguka jangwani na yeye alianguka pia.

  Ila ananikera kweli kwa kitendo cha kujivunia ujenzi wa shule ambazo watu tuliuza hadi vijiko ili tutoe michango ya ujenzi wa hizo shule! Sijui kwanini hao anaowahutubia hawamuulizi haya? Mwenzake Mkapa alitekeleza MMEM bila kututoza hata shilingi moja. Sasa huyu Kikwete katuchangisha hadi senti ya mwisho bado anajisifia.
  By the way, shule ni majengo pekee au ni muungano wa majengo, wanafunzi, walimu, vifaa vya kufundishia na samani? Huyu jamaa inaonekana hakutaka kabisa kujifunza kutoka kwa Mkapa wakati anatekeleza MMEM, kwa sababu mwenzake pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi almost kwa asilimia 100, bado hakukuwa na shida kubwa ya walimu na vifaa vya kufundishia kama ambavyo imekuwa kwake. Nina wasiwasi na aina ya watu anaowahutubia. Manake katika hali ya kawaida, hotuba kama hii inapaswa kuwa na maswali kibao.
   
 13. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  If wishes were horses.Masaa.
   
 14. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Unajua vijana wangapi wako pale UDSM kutoka hizo shule unazozizarau???Leo wangekuwa wapi kama si hizo shule??Acheni ubinafsi.Watanzania wanasoma comments zenu na wanaona upungufu wa akili zenu.
   
 15. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  u gat a point?? kuna uongo hapo, au na yeye anpewa takwimu za uongo kama mume wake??????????[/QUOTE]

  Mwambie Dr.Slaa akutafutie takwimu za kweli.
   
 16. dkims

  dkims Senior Member

  #16
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwambie Dr.Slaa akutafutie takwimu za kweli.[/QUOTE]
  witch hunt????it wont work out.!!!!!!!
   
 17. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Tandale one, hizo shule JK kazijenga lini na hao waliosoma wamefika UDSM lini? Umeshauona huo mpango wa MMES wenyewe, plan yake na implementation yake? Umeshasoma evaluation report ya hiyo MMES? Be careful my friend jaribu kuongea kwa Data.

  MMES ni mpango wa Mkapa wa mwaka 2004, wakati huu mipango ilikuwa ni kuongeza shule kidogo kidogo kila mwaka kulingana na uwezo wa serikali. Shule zilizodahili wanafunzi mwaka 2005 chini ya serikali ya Mkapa, zilikuwa na walimu wa kutosha kiasi na atleast wanafunzi kadhaa waliweza kuendelea na masomo ya A-level kutoka katika hizi shule mwaka 2008. Mwaka 2006/7, ndipo akina Lowassa wakaja na mkakati wa kujenga tu majengo yasiyokuwa na idadi ambayo hayakuendana na uwezo wa serikali kusomesha walimu na kununua vifaa vya kufundishia. Ndipo ikaja idea ya voda fasta, ambayo haikuwa na mafanikio. Wanafunzi wale ambao walisoma katika mfumo wa elimu wa akina Lowasa na Kikwete (kuanzia 2006) ndio hao waliomaliza form four mwaka jana ambao bado hawajafika chuo kikuu.

  Sasa wewe unaongelea wanafunzi gani walioko UDSM chini ya MMES ya Lowassa na Kikwete? Au wao wamefuata mfumo gani wa Elimu? Wamemaliza form four na kuingia UDSM?
   
 18. l

  lwangwa Member

  #18
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  uwezo wako wakufikiri wewe unayeisifia ccm ambayo imezeeka haina jipya haina mtazamo mpya kazi kuturudisha na kututesa na umaskini cha uhanga wa ujinga wewe huoni umaskini uliotopea huwenda wewe pia nifisadi
   
 19. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Nahisi baada ya JK kuondoka Ikulu mapendo yao yatapungua kidogo!
   
 20. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huyu TandaleOne kama Malaria Sugu vile! yaani wanafikiri kwa umbali wa pua, I doubt his/her level or eductaion and in that matter his/her thinking ability! Maana hapa tunaweza kuwa tunajaribu kumuelewesha mtu kumbe uwezo wake wa kufikiri ni wa Form four ya shule za kata!
   
Loading...