Hili nalo: Wanawake huwaibia waume zao mifukoni

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Gazeti la Mwananchi, Jumapili, Mei 1, 2016 limekuja na hoja hiyo hapo. Ni tarehe 1/5 ambayo ni siku ya wafanyakazi, duniani kote kusherehekea, hoja kama hiyo inavuta hisia za watu. Inavuta hisia kwa kuwa inagusa jinsia na hasa wanawake ambao wako katika mbio za kujitambulisha kwamba hawako tofauti na wanaume ila maumbile tu ya Mwenyezi Mungu kwa jinsi yake. Iweje wadokoe kutoka mifuko ya waume zao! Hii inanikumbusha 'post' moja humu jamvini ambayo mtoaji alikiri kuchungulia simu ya mmewe akakuta sms za mapenzi kati ya mme wake na mama yake!

Kupekuana (wanandoa au wapendanao) ni dalili ya wivu, kutokujiamini, au kutokumwamini mwenza! Nawasilisha.

CHAMBUA CHUNGUZA AMUA CHUKUA HATUA
 
hamn jamaa huo ni kuonyesha kwamba tuko pamoja kama mwili mmoja changu chake chake changu, ko achukue kikubwa ni taarifa tu
 
hamn jamaa huo ni kuonyesha kwamba tuko pamoja kama mwili mmoja changu chake chake changu, ko achukue kikubwa ni taarifa tu

Kwako wewe ni kuaminiana - changu chako chako changu au chako changu changu chako! Tunapanua mawazo.
 
Ukiacha buku tano ya chakula,halafu unarudi umepiga lager za kutosha yatakufika tuu!
 
Hii ilishatokea kwenye familia moja,mama alipoulizwa juu ya upotevu wa pesa mfukoni mwa huyo mzee hasa anaporudi nyumbani akiwa amelewa anakataa,alichokifanya yule mzee aliweka pakiti ya kondom mfukoni na kunywa bia moja tu ili asilewe,alirudi nyumbani akiwa anayumba na kujifanya amelewa sana nakujilaza kitandani bila yakuvua viatu,mama kama kawaida alimvua viatu mzee na kisha kuanza kumsachi mzee mfukoni ndipo akakuta kondom akaanza kung'aka akihisi mzee ni malaya,hapo mzee akamwambia leo nimekukamata na kithibitisho wewe ulikua ukinisachi na kuniibia mfukoni
 
Hii ilishatokea kwenye familia moja,mama alipoulizwa juu ya upotevu wa pesa mfukoni mwa huyo mzee hasa anaporudi nyumbani akiwa amelewa anakataa,alichokifanya yule mzee aliweka pakiti ya kondom mfukoni na kunywa bia moja tu ili asilewe,alirudi nyumbani akiwa anayumba na kujifanya amelewa sana nakujilaza kitandani bila yakuvua viatu,mama kama kawaida alimvua viatu mzee na kisha kuanza kumsachi mzee mfukoni ndipo akakuta kondom akaanza kung'aka akihisi mzee ni malaya,hapo mzee akamwambia leo nimekukamata na kithibitisho wewe ulikua ukinisachi na kuniibia mfukoni

Hahahaaaaa!!!

Kuna kisa hiki: mke alikuwa hamwamini mme wake na mara nyingi alipenda kupekua mifuko ya mme wake na simu kusoma sms. Mme akamtega kwa kujiandikia sms ya mapenzi kwa kutumia simu ya rafiki. Alipofika nyumbani alijifanya kuchoka sana hivyo kulala mapema.

Kama kawaida mke alimsachi mifukoni na simu akakutana na ujumbe "baby tukutane kesho sehemu ileile, nimekumiss sana". Mke roho ilimwuma, naye akaazimia kumkomoa mme wake.

Kesho yake mme alipoondoka kwenda kazini, mke alifungasha vitu vyake na kuvificha stoo. Muda wa mme kurejea, aliandika barua ikimfahamisha mme kwamba yeye mke ameondoka kurudi kwao kwa kuwa mme hampendi. Asubiri hati ya mahakama ikimtaka akatoe taraka. Mke akajificha chini ya uvungua, nia yake ikiwa kumtega mme ili ajue kama penzi la mme kwake bado lipo.

Mme aliporejea, alikuta vitu vingi sebuleni, vinavyomhusu mke wake, havipo, zikiwemo picha ukutani za ukumbusho wa harusi. Alipoingia chumbani pia kulionekana tofauti, kama vile chumba kitupu. Bahati mbaya kwa mke, nzuri kwa mme, mke chini ya uvungu mguu ulionekana.

Mezani kulikuwa na barua aliyoiandika mke, akaisoma. Baada ya kuisoma, moyoni alichekelea kwani alibaini nini mke alikitaka kutoka kwake. Alichofanya, alijifanya anampigia huyo mpenzi wake wa kufikirika simu, na kwa sauti alisema "darling, huyu mbaya wako kaachia ngazi. Najiandaa kuja tukavinjari. Kazi kwako sasa". Baada ya hapo, alingia bafuni kisha kujiandaa ili atoke.

Kabla ya kuondoka, naye aliandika machache kwenye hiyo barua ya mke wake aliyoandikiwa. Chini ya uvungu mke ni jasho na "pressure", akijua sasa mambo yameharibika kabisa.

Mme alivyoondoka alitoka uvunguni akilia kwa nguvu na uchungu hadi majirani wakaja kujua kulikoni. Alikua tayari kutoa uhai wake kwa kujinyonga. Rafiki wa karibu akahoji kilichojiri ndipo kueleza kisa na mkasa wote. Alichukua ile barua aliyomwandikia mme wake na kumpa shoga wake. Hakujua kwamba mme alikuwa ameijibu humo humo. Shoga kuisoma akashangaa na kumwambia mwenzake kuwa zengwe kalitengeneza mwenyewe. Kumbe mme alikuwa ameandika machache tu kwenye hiyo barua "mpenzi mke wangu, sikutegemea kuwa huniamini siku zote. Usomapo ujumbe huu, naenda kununua mahitaji ya humu ndani, nitarudi muda si mrefu. Baadaye".

Mke na mme tuaminiane. Hilo linawezekana tu ikiwa kila mmoja anajiamini. J2 njema wanajamvi.
 
Back
Top Bottom