Hili limenikuta ktk test ya pspf

Hili limenikuta ktk test ya pspf

MY LOVE

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
161
Reaction score
68
Jana nilienda kufanya test ya PSPF pale DUCE post ya compliance officer grade II niliyo yaona sikuamini macho yangu na nilipigwa na butwaa nisijue hatua gani ya kuchukua na mwisho wa siku nikaaamua kumwachia Mungu maana sikutaka kuongeza maadui maishani mwangu.
Ni hivi kwawalio kuwepo watanielewa, nilikaa upande wa majina ya E,F,G NA H na mbele yangu alikaa dada/mama mmoja ambae alikuwa na answer sheet mbili, ila tulizopewa ni moja je hiyo ya pili yeye kaipata wapi? na alizibana pamoja ili mtu asigundue kuwa anazo mbili na nilivyo iyona ilikuwa imeshajazwa kabisa ni swala la kuandika jina na kukusanya tu. Ilinikera sana na kuamini bado kuna tatizo kubwa la kupata ajira kwa haki, kama test zenyewe zinavuja hivyo then utasema washindi wamepatikana kihalali? INGEKUWA WEWE NI MIMI UNGEFANYAJE? JE NINGELILIPUA PALE Holini ingekuwa sawa au ningechafua mazingira? Hata number yake niliishika kabisa na niliporudi home nikaangalia majina na jinalake linaanzia na E.......
 
Mkuu ajira bado ni tatizo hapa nchini,hivyo kufanya watu wafanye kila mbinu wapate hizo kazi.
 
Wenyewe watakuja hapa kukanusha
 
Pole sana. Tena kwa Social Security Funds zote kupata ni tabu sana maana ndiko vimemo vimejaa. Kwa kifupi kupata kazi zile taasisi nzuri za serikali (zinazolipa kama BOT, security funds, EWURA, TPA, you mentin all) ni kazi kubwa kama huna memo. Unafaulu interview na hupati kazi,anapata wa kimemo hata sifa nzuri hana!! So sad, nepotism still on.
 
binafsi nnahisi lile lilikuwa desa, wewe ungemlipua tuu, ndicho ulichotakiwa kufanya, kwa sasa ni sawa kelele za chura
 
Alipewa majibu na Roho mtakatifu na atatoa ushuhuda mungu alimpatia majibu, wizi mtupu
 
Jana nilienda kufanya test ya PSPF pale DUCE post ya compliance officer grade II niliyo yaona sikuamini macho yangu na nilipigwa na butwaa nisijue hatua gani ya kuchukua na mwisho wa siku nikaaamua kumwachia Mungu maana sikutaka kuongeza maadui maishani mwangu.
Ni hivi kwawalio kuwepo watanielewa, nilikaa upande wa majina ya E,F,G NA H na mbele yangu alikaa dada/mama mmoja ambae alikuwa na answer sheet mbili, ila tulizopewa ni moja je hiyo ya pili yeye kaipata wapi? na alizibana pamoja ili mtu asigundue kuwa anazo mbili na nilivyo iyona ilikuwa imeshajazwa kabisa ni swala la kuandika jina na kukusanya tu. Ilinikera sana na kuamini bado kuna tatizo kubwa la kupata ajira kwa haki, kama test zenyewe zinavuja hivyo then utasema washindi wamepatikana kihalali? INGEKUWA WEWE NI MIMI UNGEFANYAJE? JE NINGELILIPUA PALE Holini ingekuwa sawa au ningechafua mazingira? Hata number yake niliishika kabisa na niliporudi home nikaangalia majina na jinalake linaanzia na E.......[/QUOTE

Ndugu daima namwambi mdogo wangu mashirika ya wazungu au ngo ambazo wazungu ndio wanaointerview watu awana ubabishaji kama unafaa wanakuchukua ufai wanakuambia ni sehemu gani ujafanya vizuri.Hila kwetu Mungu atusaidie na mfumo ubadilike.Jipe Moyo Kama ipo ipo tu japo itachelewa,kumbuka mlango mmoja ukifungwa Mungu anafungua mwingine tena 7 kuwa mwaminifu kwake naye atakupa aja ya moyo wako.
 
Pole ila ucjal labda nawe utakuwa miongon ya waliochaguliwa blv!.
 
Bora ulikaa kimya. maana hata kama atapita hii ya kwanza ya pili atachemka ambayo ni oral.alaf yeye kuingia na desa hakukunyimi nafasi ya wewe kukosa at the end of the day inawekwa limit labda 75% kama yeye kavuka na wewe umevuka mtapambana mbele ya safari ..ALIEBEBWA HAJUI UMBALI WA SAFARI
 
Wajuaje kama hana maswali ya oral tayari?utashangazwa ndugu
Bora ulikaa kimya. maana hata kama atapita hii ya kwanza ya pili atachemka ambayo ni oral.alaf yeye kuingia na desa hakukunyimi nafasi ya wewe kukosa at the end of the day inawekwa limit labda 75% kama yeye kavuka na wewe umevuka mtapambana mbele ya safari ..ALIEBEBWA HAJUI UMBALI WA SAFARI
 
kwa njia moja au nyingine wote tunadanganya!!!!!!!!!!!!, sijui alilipa nini!!! bora wewe ulikomaa..
 
Mungu atupe rehema.

Kama huna ndugu ofisini, usithubutu kutuma vyeti vyene ufaulu wa juu, vitaishia kwenye shredder wakati wa sorting.
 
Dah..inakatisha tamaa sanaa...wala hoi tutatoka kwell..,??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom