Hili lilimgarimu Dr Slaa 2010-uchaguzu mkuu

Hili lilimgarimu Dr Slaa 2010-uchaguzu mkuu

Mpambanaji.com,

Hivi wewe umemaliza darasa la ngapi?? Nina hakika wewe ni wa ELIMU YA MADRAS! Bisha kama una ubavu!
Maneno yote niliyo yaonyesha kwa RED inaonyesha tu kuwa shule yako ni ya madras. Hufai kuingia kwenye ukumbi huu wa GThinkers maana unapoteza muda wako. Wewe nenda kaswalishe msikitini kwako na kufundisha madras zako ili uzungumze UTUMBO WAKO HUKO na siyo hapa.
Shangazi Makoye ninaamini yakuwa wewe ni mwalimu mzuri na nikiri kwa RED zako. Pia pole kwa majibu ya jazba kwangu.Sikuweka mada hii kidini kwani ni kuhakikishie hata mie ni Mkristo wa sala, elimu na kazi. Lengo la mada hii ni kuuchambua ukweli ulipo mioyoni mwa raia wengi wanaodanganyika kirahisi kwa hisia nyepesi bila kutafakari na ningependa uchangie kikamilifu kwani hata viongozi wa CHADEMA wasipojibu hapa naamini watapata maoni ya kujenga na kufuta hisia hizo zilizokwisha wekwa kwa wapiga kura wengi hususani vijijini na Ant-Christians. Singependa unnecessary over emotions u better quit if found it boredom to u.
 
jasusi kweli wewe, umejishusha kwa jibu lako.Nadhani unahitaji kuwa mbele kimawazo kudaka saikolojia za watu na tafakari za kina kabla hujajibu.Natamani nifahamu uchambuzi wa mada zako au wakati mwalimu anakuambia jadili ulikua unaline up! during or in this schooling days of urs.
Na wewe pia ni Great Thinker, eeh?
 
Nakushukuru sana kwa majibu haya na haya yanahitajika pia kwa baaadhi a wanJF kwani wengi wao wanaonekana kukurupuka tuu. Kwa maneno yako ya busara sina shaka wewe ni kiongozi wa juu wa Chama au Taasisi fulani.Napenda sana uchambuzi wa namna hii uwafikie watu wengi hususani vijijini.Huwa ni changamoto sana kuwaelimisha watu juu ya hisia zao na husasani itokeapo kiongozi wa chamba ambacho mie ni kada anaonekana wazi kutokutekeleza matakwa ya watu waliomchagua. U r a good leader.
Nasikitika sana kwamba watu wamwangalia Dr. Slaa kama individually. Hili ni tatizo, tena kubwa sana.Lakini pia si vema kutazama CDM au CUF kama ndiyo suluhu ya matatizo yetu. We're wrong. Slaa ni binadam kama watu wengine. Siku moja atakuwa amezeeka, au ameamua kuachana na siasa sasa hii hoja ya upadri itakuwa imetusaidia nini. Au CDM kesho na kesho kutwa ikaparaganyika kama vyama ilivyotokea kwa vyama vingine hii hoja ya ukristo au ukanda itakua na mantiki gani? Na, je matatizo yetu yatakuwa yamepata suluhu, mimi naona ni hapana. Ni kama tunajidanganya.

Mimi naamini ndani ya CCM bado tuna watu waadilifu humo, lakini pia si kila mtu kwenye upinzani ni mwadilifu. Hii ni kama ambavyo, si kila muumini anafuata kanuni zote za dini yake, mbona tunao wengi tu ambao mchana ni waumini wazuri lakini usiku ni firauni wa kutupwa. Kifike kipindi watu tujue kwamba hata ndani ya hizi dini zetu wapo viongozi ambao si waumini wa ukweli kama tunavyodhania. Wanaweza kuwapotosha watu kwa kuwalisha mafundisho machafu. Ni vizuri kutathmini haya mafundisho yanayokuelekeza kumwona mbaya jirani yako ambaye miaka yote umekuwa unaishi naye bila shida. Mmekuwa mkishirikiana, watoto wenu wanapenda na wamezoeana sana. Lakini leo hii kiongozi wako wa dini anakwambia huyo jirani yako ni adui yako eti tu dini yenu ni tofauti. Huu si uchuro. Miaka yote hiyo huo uadui ndo umeanza leo.

Nachosema hapa ni kwamba tuache unafiki. Ndiyo najua kila mmoja anapenda kibarua chake, lakini inapokuja hoja ya maslahi ya taifa, hebu tusimame pamoja. Tutetee maslahi yetu. Hebu tuache maslahi ya vyama vyetu jamani. Nijuavyo mimi, wapiga kura wengi si wanachama wa chama chochote. So, kiongozi unapoanza kuweka mbele maslahi ya chama chako unakuwa unawasaliti wapigakura wako. Haya mambo yanajitokeza sana pale bungeni, hili sitaki kusema sana.

Nihitimishe kusema kwamba wananchi wanahitaji maendeleo, wananchi hawamhitaji Slaa kwa kuwa yeye ni muumini mzuri wa dini, wananchi wamevutiwa naye labda ni kwa kuwa ameahidi kuboresha maisha yao. Wananchi wanavutiwa na vyama vya upunzani si tu kwa kuwa kuitwa mpinzani ni sifa fulani. La hasha, wananchi wanavutika huko kwa kudhania kwamba labda ukombozi wao utatokea huko pengine labda hawa ambao wamekuwa wakiwaamini kwa muda wote huo hawaonyeshi kujali matatizo ya wananchi.

Nahisi ni busara kuachana na kukimbizana na wapinzani mabarabarani, badala yake chama kilichopo madarakani kiisimamie serikali itekeleze wajibu wake kwa wananchi. Si rahisi hivyo kumwongoza mwenye njaa, mtu aliyekata tamaa ya kuishi maisha ya kubahatisha katika nchi ambayo ina rasilimani sawa sawa na South Afrika. Kibaya zaidi ni pale ambapo mwananchi mvuja jasho anaposhuhudia maisha anayoishi kiongozi aliyemwahidi maisha bora kwa kila mtu miaka michache iliyopita. Jamani tusimtafute mchawi, ni watu hawawajibiki kwa namna walivyotuahidi.

Sisi tutaishia tu kukabana ktk mambo yasiyo na maana yoyote.
 
shangazi wewe ni mgumu wa kufikiri chambua mada, tatizi sie wanaCHADEMA sometimes tupo very emotional na ndo kinachotugarimu wakati mwingine.
 
Nakushukuru sana kwa majibu haya na haya yanahitajika pia kwa baaadhi a wanJF kwani wengi wao wanaonekana kukurupuka tuu. Kwa maneno yako ya busara sina shaka wewe ni kiongozi wa juu wa Chama au Taasisi fulani.Napenda sana uchambuzi wa namna hii uwafikie watu wengi hususani vijijini.Huwa ni changamoto sana kuwaelimisha watu juu ya hisia zao na husasani itokeapo kiongozi wa chamba ambacho mie ni kada anaonekana wazi kutokutekeleza matakwa ya watu waliomchagua. U r a good leader.

Mkuu mimi sio mwanachana wa chama chochote, ni mpiga kura tu.

Sometimes ninaamua kutoa hisia zangu hapa ili angalau wenye nia ya kataka kuelewa waelewe.
Maana siku hizi wengi wanaendeshwa kwa emotions tu, hawana hoja ya kusimamia na ndio maana hawa jamaa tuliowaamini na kuwa dhamana ya maisha yetu wanautumia udhaifu huu kufanya haya unayoyaona siku hizi.

Usiwe na shaka mkuu tupo pamoja. Tanzania hii yetu, hatoki mtu hapa.
 
kwenye RED inaonyesha wewe umekata tamaa na ulicho bakisha ni kuburuzwa tu
alishinda urais akiwa na wabunge 22 kati ya 239 wa majimbo? mbona asingeweza kuunda serikali? acheni kujipa moyo uchaguzi 2010 mlichemsha! labda mjipange upya kwa mwaka 3045!
 
Waislamu tuache unafiki, ubinafsi na Ubaguaji. Mbona Rais Mwinyi alikuwa akiitwa Alhaji na hakuna Mkirsto
aliyewahi kulalamika kwamba tunaongozwa na kiongozi wa uislamu.

Leo kajitokeza Mkirsto ambaye kabobea kwenye mambo ya dini yake tunakimbilia kulalamika kwamba
hatuwezi kuongozwa na Padri achilia mbali kabisa kwamba Huyu mzee hajawahi kuwa na hicho cheo,
haya mambo ndiyo yanayotufanya tuonekane walalamishi na watu tusio na uwezo wa kufanya kitu
chochote kile zaidi ya kujivunia dini yetu.

Naomba tufanye maamuzi yetu katika msingi wa
1. kuondoa utawala ambao unakumbatia rushwa na ufisadi kama ambavyo uislamu unataka.
2. Kuondoa utawala ambao umeshindwa kutuhakikishia watanzania huduma za afya, elimu,
usafiri na miundombinu yake, chakula, mavasi, ulinzi,haki na heshima ya utu.

DR Slaa haendi Ikulu kuanzisha Ufalme wa Mungu wao, hilo liko wazi kwenye kitabu chao kwamba
wanayetegemea aulete ni Yesu Kristo sasa Dini yake sisi inatuhusu nini.

Anakwenda Ikulu kutuongoza kwa Mujibu wa Katiba ya nchi yetu, sisi sote, Makafiri na Waislamu,
ambayo tumekubali kuongozwa chini yake huku tukijua hakika kwamba tunakubali kuongozwa
katika misingi ambayo inawafurahisha hata Makafiri.

Tuache Unafiki. Tupiganie Mahakama yetu ya Kadhi, huo ndio Muongozo wetu wa kweli kabisa
wa uislamu, tupiganie na DR SLAA aingie Ikulu, Japo tufanikiwe kupata futari kwa bei ya chini
na kuila kwenye Mwanga badala ya Giza.

Tubadilike
Alai Wakbar

We Mnafiki tu! Huna Uislam na hata Uislam huujui.Huwezi kutusemea kwa kujifanya muislam! Laana ziwe juu yako na unafiki wako! Huna lolote ila kubabaisha akili za watu humu JF,babaisha wajinga wenzio.
 
Majitu humu ni mapumbavu sana, narudia tena, mapumbavu! mtoa mada ametoa kwa nia njema na amegusia uhalisia unaotoke nchini. jamii ya waislam bado inaamini slaa ni padre na cdm ikishika nchi tutaendeshwa kikanisa. ni point ya msingi kwa vile tunahitaji kura za wote ili kufanikisha azma ya kushika dola. sasa inapotokea mipumbavu na kuanza kashfa kama hizo hapo juu, ni hatari kwa jf na ni hatari zaidi kwa cdm ambao wanataka kuchukua dola. tunaposema waislamu, hatumaanishi public figures wachache, ila ule umati unaokusanyika pale msikiti wa mtoro, shekha issa magomeni, kwa ajili ya swalat ijumaa... kuweni wakubwa jamani!
 
Majitu humu ni mapumbavu sana, narudia tena, mapumbavu! mtoa mada ametoa kwa nia njema na amegusia uhalisia unaotoke nchini. jamii ya waislam bado inaamini slaa ni padre na cdm ikishika nchi tutaendeshwa kikanisa. ni point ya msingi kwa vile tunahitaji kura za wote ili kufanikisha azma ya kushika dola. sasa inapotokea mipumbavu na kuanza kashfa kama hizo hapo juu, ni hatari kwa jf na ni hatari zaidi kwa cdm ambao wanataka kuchukua dola. tunaposema waislamu, hatumaanishi public figures wachache, ila ule umati unaokusanyika pale msikiti wa mtoro, shekha issa magomeni, kwa ajili ya swalat ijumaa... kuweni wakubwa jamani!


Mkuu ni elimu tu ya uraia inahitajika hapa. Kimsingi hatutegemei elimu hiyo kutolewa msikitini wala kanisani kwa kuwa hizo ni sehemu nyeti kwa ajili ja watu kukutana na Muumba wao. Ukiona elimu ikitolewa huko, mimi niseme tu si mahali husika, kwa vyovyote kutakuwa na biasi. Sisemi maimam na wa kuu wa makanisa wasihubiri amani na kukemea uchafu, la hasha. Wafanye hivyo kwa nguvu zote. Nacho sisitiza ni kwamba wasipotoshe waumini wao eti kwamba maisha magumu kwa watu yametokana na influence ya dini fulani(hili nimeishalisema hapo juu). Vyema zaidi wakawahimiza waumini wao namna ya kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuinua vipato vya waumini mmoja mmoja.

Sio kweli kwamba waislam wanapenda maisha magumu yanayotokana na sera mbovu zinazosimamiwa na hawa tuliowaamini na kuwapa mamlaka. Njaa haiangalii dini ya mtu, ugonjwa kadhalika. Issue ya udini wa kiongozi si suluhu ya matatizo tuliyonayo. Tunahitaji sera zenye kutoa fursa sawa kwa wote na sio tu kusimamiwa, bali zionekane kusimamiwa kweli. Kwani nani kasema kuwa kiongozi lazima uwe na dini? Katiba inasema kuwa kiongozi wa kisiasa lazima uwe mwanachama ktk chama cha siasa sio dini.

Niseme tu kwamba waislam ni watu wazuri tu kihistoria, na linapokuja swala lenye maslahi kitaifa naamini wanafanya uamuzi kwa kuzingatia maslahi hayo. Kwanza, nani kasema waislam wote hawapendi chadema? Nani mwenye ushahidi kwamba Slaa hakupata hata kura moja ya muislam? Hii sio kweli. Ndio maana mimi huwa siamini katika generalization. Usije ukamkuta muislam mmoja anakula nguruwe kichochoroni ukaondoka hapo ukipiga mayowe kwamba waislam siku hizi wanafanya kitu kama hicho. Huu ni upuzi mkubwa. Uliyemkuta amekengeuka yeye kama yeye ila usikashifu dini safi ya watu. Mimi nitakuwa wa kwanza kukupiga mawe.

Ni kweli kwamba hizi kauli zinasikika sana mitaani, pengine na katika hizo sehemu za ibada, lakini nasisitiza kwamba wanaozitoa wanafanya hivyo kwa msukumo wa kibinadam sio wa kimungu. Ni wajibu wa muumini mmoja mmoja kupima mantiki ya kauli hizo na kuchukua hatua huku akitilia maanani kuwa uamuzi wake ndio utakaoamua hatima ya Tanzania ya kesho ambayo ni ya watoto wetu na wajukuu wetu. Sijui ni kwanini tunashindwa kujihoji kwamba je, tunaridhika watoto wetu(tulio wengi) waje waishi maisha kama haya tunayoishi? Je hii mitazamo ya kidini ndilo hitaji la watoto na wajukuu wetu?

Kiukweli hii sio changamoto kwa Slaa na CDM yake tu, bali zaidi ni changamoto kwa jamii ya kiislam. Nasema hivi kwa sababu kwa kiasi kikubwa waislam ndio wenye malalamiko zaidi. Wanalalamika vitu vingi tu, kwa waliomo ndani wanajua zaidi ya sisi tulioko nje. Na malalamiko mengi ukiyatazama kwa mtazamo wa kiimani ya mantiki, tena kubwa tu. Tatizo lililopo hapa ni kwamba kiukweli wameaminishwa kwamba matatizo yao yameumbwa na kikundi fulani cha watu. Swali, je Slaa ndiye kayaumba? Je, CDM ndio chanzo? Waislam wenyewe wanajua.

Hivyo basi tunapokuwa tukijadili hili, ni vema waislam wakawa wakweli.Wakubali kwa dhati kwamba mchawi wao si Slaa wala CDM yake ambao kiukweli hawana mamlaka yoyote hapa nchini. Waislam wakubali kwa dhati kabisa kwamba mchawi wao ni yule waliyemwamini wakampa mamlaka, lakini alipofika huko akawasaliti an kuziba masikio asisikie kilio chao, that's all. Mimi naamini waislam wana upeo mkubwa wa kung'amua mambo, sioni sababu ni kwa nini wasione kama huu ni mchezo mchafu wanafanyiwa. Kwani chadema ndiyo inazuia mahakama ya kadhi? Au chadema ndiyo ilifukia swala la OIC? Chadema wanahusika vipi ktk hili, wakati na wao kila kukicha wanafukuzana na huyo huyo mchawi wa waislam. Mbona kuna msemo unaosema Adui wa adui yako ni rafikiyo? Je uraki huu upo kweli? Na ndicho hiki ninasema kila mara kwamba huyu mchawi anajua impact ya huu msemo. Ameamua kuvunja daraja la huo urafiki ili aweze kudili na kila mmoja kwa namna yake, na kwa kweli amefanikiwa.

Lakini pia hii ni demokrasia, kila mtu yuko huru kuchagua kusupport chama chochote chenye sera anazoona zinaweza kumkomboa. Mbona vya viko vingi? Sio lazima upinzani, mtu anaweza akaendelea kuisupport ccm mradi tu ameridika na kuona kwamba ndicho chama kitakachomkomboa kutoka kwenye huu umasikini uliokithiri.Waislam(kama kweli wana uamuzi wa pamoja) wanaweza wakaamua kukisupport chama chochote watakachoona kina mwelekeo wa kutetea maslahi ya watanzania wote(si waislam tu) si lazima iwe chadema. Na ndiyo maana sioni mantiki ya kujadili issue ya waislam vs slaa au cdm. Hii ni demokras wanaweza kuamua kuwa ktk chama kingine na watu wote pengine tukaridhika na sera za chama hicho wote tukaungana tukakiweka madarakani na maisha yakaendelea.

Huyu mchawi anajua kabisa kuwa manung'uniko ya waislam ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote, na anajua kabisa kuwa hana mpango wa kuwatimizia mahitaji yao; na kwa kuwa ameona chadema wanakuja kwa kasi ya kimbunga, sasa katika kuhakikisha kwamba haya makundi mawili yenye nguvu hayaunagani ameamuwa kuwaloga. Amewatupia jini udini sasa kila mmoja hana imani na mwenzake, kwisha habari. Na bila kugundua hawa ndugu zetu waislam kweli wanaamini kwamba mbaya wao ni padri na chadema yao. Hii sio kweli.

Huyu mchawi ana akili kuliko tunavyodhani. Anatambua kabisa kwamba wanasiasa hata siku moja hawatakaa menza moja kuungana na kutengeneza kambi moja ya upinzani kwani kila mmoja anataka kuwa juu ya wengine, so huyu mchawi anajua kabisa kuwa nirahisi sana kwa waislam kwa hasira wakaamua kujiunga na chama cha upinzani chenye nguvu kwa sasa(chadema). Na hii mbinu haiishii hapa. Kesho na kesho kutwa kitaibuka chama kingine chenye nguvu zaidi ya chadema, na kama waislam bado watakuwa na manung'uniko yao, mtasiki habari nyingine tofauti.

Mind you, tatizo sio padre na chdema yake. Hii ni mbinu tu ya kuhakikisha chadema hakipaki support ya waisla ambao kwa miaka mingi wamekuwa denied and ignored by the cruel policy chini ya huyu mchawi ambaye kwa kipindi chote hicho waislam hawajamng'amua. Ole wake siku wakimng'amua na kuamua kuchukua hatua ya kumuadhibu!!!
 
Back
Top Bottom