UWEZO_WAKO
Member
- Nov 17, 2010
- 39
- 4
Nawaomba kwa dhati ya moyo na hapa natoa pendekezo langu Wabunge wa CDM wakae na uongozi wa chama wakubali kila mbunge akubali kutoa asilimia 10 ya mshahara wake kila mwezi kwa kipindi cha miaka 5. Hizi fedha ziende kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo (elimu, maji, nk) katika majimbo yao. Hili litakuwa bao la pili la uhakika baada ya lile bao walilofunga pale Bungeni walipochukua uamuzi mgumu wa kihistoria kupata kutokea Tanzania, kwa kutoka na kukataa kusikiliza hotuba ya JK. Uamuzi wao wa pale Bungeni ni msingi imara ambao ni lazima tu utazaa matunda ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi...hapa mlikuwa wabunifu kweli kweli, maana serikali ya....kwa kutumia polisi wake wao walikariri tamko kama hilo litatokea kwa njia ya maandamano tu. Sasa tunataka jambo hili la pili kwa wabunge la kutoa asilimia 10 za mishahara yao kwani nina hakika litazaa matunda ya muda mrefu. Sisi tutafuata nyuma kuchangia miradi ambayo watakuwa wameichangia.
Mandela akiwa Rais alitoa moja ya tatu (asilimia 33.3) ya mshahara wa kila mwezi kwa muda wa miaka 5 kwa ajili ya kuanzisha kile kilichokuja kuitwa "The Nelson Mandela Children's Fund". Kwa upande wa Nyerere shuhuda mmoja anaripoti kama ifuatavyo "The period of campaigning for independence was a very difficult time for Julius and Maria. Julius refused to take any salary from TANU. He said that the party needed all its funds to gain independence. At the same time Oscar Kambona took a salary to support himself and his family. Maria opened a small duka (shop) to sell soap, sugar, salt, cooking oil etc. in their small home in Dar es Salaam to earn a little money to support the family. She also had a heavy burden of cooking for the many African visitors that came to visit Julius. It is the custom to cook a meal for all visitors. In his position as President of TANU he received many visitors every day. Julius one day told me that any other woman other than Maria would have left him long ago, but Maria stayed during this very difficult time"
NO PAIN NO GAIN. Ningependa kurudia tena kiongozi bora ni kama rafiki wa kweli ni vigumu kumpata, haiwezekani kumuacha na kamwe hasahauliki. Mandela hawezi kusahaulika na Nyerere japo amekufa angali akinena...kuna bibi mmoja nasikia uchaguzi huu ulioisha aligoma kupiga kura akisisitiza aonyweshwe sehemu ya kumpigia Nyerere maana ndie aliyetaka kumpa kura yake.
Sisi wananchi hatufurahishwi na utoaji wa rushwa ili kumchagua kiongozi, kwanza mbali na kuwa rushwa hizo huenda kwa watu binafsi ni kinyume cha sheria, utu wa binadamu na sumu ya maendeleo. Tunataka kitu kinachoenda kwenye mifuko ya jamii sio mtu binafsi. kama wabunge wa CDM atatoa asilimia 10 (itapendeza isiwe si chini ya hapo) kwanza watakuwa wameonyesha uzalendo wao na pia kuunga mkono mawazo aliyokuwa nayo mgombea wa urais kupitia CDM kuwa atapunguza mishahara ya wanbunge na mawaziri akichaguliwa kuwa rais. Hata kama CDM haikupata urais haina maana hatuwezi kutekelleza hilo kwa vitendo. Nakuhakikishia kwa kufanya hivyo wabunge wa CDM mtakuwa tayari mmeshatangaza ushindi wa kurudi bungeni kwa kipindi cha 2015-2010. Mambo menginne mtaendelea kufanikiwa kwa kufanya hivyo mtawavutia wengi wenye kupenda kuchangia maendeleo huwa tu wanakatishwa tamaa na aina ya viongozi wa sasa tulionao wanaopenda kuvuna tu na sio kuchangia.
Hivyo fanyeni hima mkatende kwa busara na ujasiri kuhakikisha majimbo mliyonayo hamyaachii 2015, nawatakia kila la kheri wengine pia wanaopenda au kufikiria kuwatumikia wananchi kwa nafasi za ubunge basi nao pia watafute namna ya kuwa karibu na wananchi kwa kushughuli za kimaendeleo huku wakipanga namna ya kuchukua majimbo mengine yote yaliyobakia.... Inawezekana timiza wajibu wako. KAMA JIBU LA WABUNGE LITAKUWA NDIO AU LENYE KUFANA NA MTAZAMO WA MATOKEO MAZURI NITAFURAHI. NASUBIRI JIBU LA WAHESHIMIWA WABUNGE ILI NA MIMI NIJIUNGE NA CDM.