Hili la Viwanja na NIDA lisisubiri hadi Julai 2021

Fatma-Zehra

Senior Member
Oct 18, 2020
192
1,062
Kama nilichokisikia ni kweli, naipongeza serikali kwa kubuni njia nzuri ya kupambana na ufisadi kwenye sector ya ardhi. Lukuvi anasema ataunganisha namba ya mmiliki ya NIDA na taarifa za kiwanja/viwanja anavyomiliki. Niliwahi kushauri kwenye thread moja iliyohusu kuondoa na ku-descourage informal settlements Dodoma nikisema kuwa watumishi wanaohusika na sector ya ardhi nchini ni wa kuchunguzwa.

Hata kama kwa sasa amehama kitengo. Hili la lukuvi la kuunganisha NIDA na umiliki wa viwanja utasaidia kutengeneza mwanzo wa kuondoa ufisadi kwenye ardhi. Team ya wizara (Lukuvi, Angel, pamoja na Mary) nawapongeza sana. Hata hivyo, naomba Lukuvi asisubiri hadi July kuanza hiyo kazi. Aanze sasa hivi. Anashindwa nini?Hatutaki watu wajipange kushambulia na kujinasua kutoka kwenye hii initiative ya serikali mapema.

Please "invade them" as soon as possible. Katika hii vita, natamani kuuona ujasiri wa JPM. Siyo vita ya level ya Lukuvi. I wish to see the president receiving the report and acting fast. Hii issue itaibua uchafu mwingi sana wa watu wa ardhi, vigogo, na sisi common wananchi. This is a scientific way of combatting corruption. JPM did well katika ghost workers. I believe he will succeed on this issue as well.

Jambo la muhimu ni kwamba kuna viwanja vingi ambavyo vimehodhiwa na wafanyakazi wa ardhi na hawajavilipia hata shilingi. Wananchi wala hawavijui. Wanachofanya watu wa ardhi ni kugeuka kuwa madalali wa hivyo viwanja. Imagine you need a land let's say kujenga hotel au residential house, unaambiwa havipo. Ila ukitoka tu unaitwa pembeni na kuulizwa wapi ulitaka. Unataja sehemu. Wanakwambia kuna sehemu wanauza 150mil. Unawauliza particulars za kiwanja wanakwambia hakijalipiwa ila what we will do ni kuwa serikali inataka kama 80mil. Hiyo tutakufanyia utaratibu na kiwanja kitatoka kwa jina lako halafu utatupa hiyo 70mil pembeni.

Na kweli wanafanya maana wako kwenye system. Huu mchezo uko sana Dodoma. Unakatisha tamaa wawekezaji. Imagine you need like 10 different plots of let's say 6000sqm. Serikali itapata 50% na nyingine zitaenda kwa wafanyakazi wahuni. Unfortunately, mwekezaji ambaye hapendi ubabaishaji anaachana na mpango huo. Serikali inakosa pesa. Uwezekezaji unaondoka. Mbaya zaidi kiwanja kinaendelea kutonunulika na kuwa developed.

Hivi viwanja hewa, kwa kutumia technology, serikali ivibaini na iviuze hata kesho. Itapata pesa nyingi sana. Ni vingi sana hata kama vina sqm 600 each. President Magufuli aliposema Dodoma inakuwa jiji kwa mfano, tuliitamani Dodoma. Lakini ndoto za wawekezaji waaminifu na wadogo zinahafifishwa na watu wa ardhi wasio waaminifu. Mimi kwa mfano, ninayatamani sana maeneo yaliyo karibu na Ikulu ya Chamwino maana ni deal lakini Jiji pia wameshindwa kuweka miundombinu wakati maeneo ambayo hayapimwa yana miundombinu. For example, Mtumba is a "future" hotcake na ni nzuri kwa hotels and other institutions.

Lakini cha ajabu, unakuta hakuna barabara, wala daraja la kuvuka makorongo kwenda kwenye 10,000 sqm hotcake plots ambazo serikali imepima yenyewe. Umeme na maji hakuna. Wekeni barabara na madaraja. Wekeni maji. Ujenzi utafanyika kwa haraka na umeme, internet, simu na mengine yatakuja tu. Jiji wanapima viwanja na kulala. I once said that Ikulu ya chamwino na mji wa serikali, lakini barabara na madaraja na miundombinu mingine kutoka barabara ya lami ya kwenda Dar (vikonje sijui buigiri) kupasua viwanja vya serikali vya mtumba na kupasua moja kwa moja hadi kikombo kule ni kichocheo cha uwekezaji lakini pia na other settlements ambazo zitaiingizia serikali mapato.

Statehouse haitakiwi kuzungukwa na squatters. Dodoma nimeona kuna fursa nyingi sana maana wafanyabiashara wa Dodoma wengi wao nimekuta customer service ikiwa almost zero. That's an opportunity.

Baada ya kuunganisha na NIDA, kuna madudu mengi mtayaona. Serikali itavuna mabilioni. Hongera sana serikali. Please act now. Msisubiri July.
 
Raia mwenye viwanja vingi kuchunguzwa na kuitwa muhujumu uchumi. Tujiandae.
 
Raia mwenye viwanja vingi kuchunguzwa na kuitwa muhujumu uchumi. Tujiandae.
Lengo la msingi ni kuboresha utambuzi na kwahiyo wale wanaomiliki ardhi kihalali ambao ndio wengi sana wao watanufaika, ila kwa wanaomiliki ardhi kwa malengo ya kujinufaisha,kujilimbikiziaa na kulangua watadhibitiwa.
 
Matatizo haya yote yalianzia huko kwenye Halimashauri kwa madiwani ambao wengi wao ni school failures, hili zoezi halihitaji kusubiri, vinginevyo serikali itapoteza fedha nyingi zaidi ikisubiri zaidi ya sasa
 
Matatizo haya yote yalianzia huko kwenye Halimashauri kwa madiwani ambao wengi wao ni school failures, hili zoezi halihitaji kusubiri, vinginevyo serikali itapoteza fedha nyingi zaidi ikisubiri zaidi ya sasa
Kama dhamira ipo na ni thabiti , Julai wala sio mbali.
 
Raia wa kawaida anaruhusiwa kumiliki viwanja vingapi?

Kama ni kiwanja kimoja kinachotambuliwa na kwa kutumia taarifa za kitambulisho cha Taifa (NIDA) je, haioneshi kwamba ndio chanzo cha watu kuanza kutumia majina ya watu wengine hivyo hatimaye kusababisha migogoro ya rdhi isiyo na maana yoyote? (Kama kauli iliyosikika kutoka kwa Waziri ni sahihi)

Kwanini waziri na naibu wake wanahimiza kila mtu kulipia ardhi au jengo wakati hata utambuzi kupitia Mkurabita haujafanyika kikamilifuna iwahusika kumilikishwa au kupewa leseni ya makazi?

Huyo mmiliki wa kiwanja au jengo atalipaje hiyo kodi wakati hajapewa namba ya utambuzi kwa malipo hayo hayo (electronic government payment control number)?
 
Umeanidika ukweli mtupu kwa Dodoma maafisa Aridhi wanashindana kuiba na kununua magari hii zaidi ya CDA
Ametoka mdudu mmoja likaingia dudu jingine. Bora yule mdudu tuliyekuwa naye hapo awali kuoiko hili dudu. Linawaza tu hela kwa maslahi binafsi.
 
Wacha tusubiri, ila watu wa ardhi ni matajiri niamini mimi
Nenda pale Geza ulole Kigamboni eneo kubwa unaweza kusema ni pori kumbe viwanja vya hao watu, tena wanauza bila stress yaan

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
MHH! TUSIJIONGOPEE..! HAO NIDA WENYEWE NOT SECURED, MAJITU YANAPATA NAMBA FOR A SIMPLE DETAILS..! (naskia skia lakini) 😌
 
Mpango ni mzuri na inawezekana ana nia njema lakini hawawezi kupambana na awa wahuni maana mpaka makatibu wa wizara wanahusika ata kwenye timu yake mle kuna wahusika naona anapambana na wauza unga bila kujua kampuni yake ndio wanunuzi.
 
Pesa hakuna anasakwa mbuzi wa kafara wa kukamuliwa ela hapo ikishapatikana na game is over....
 
Huu uzi una maelezo ya msingi, lakini nashindwa kuelewa, ukiisikiliza serikali na wapambe wake wanasema rushwa imedhibitiwa, na nidhamu imerejea kwenye ofisi za umma, lakini maelezo haya mazuri ya mleta uzi yanayoonyesha rushwa ni kubwa kupita kiasi, sasa kama Dodoma ambako ndiko makala makuu ya serikali bado kuna rushwa, huko kwingine kuna hali gani? Mimi na wengine tuliogoma propaganda mfu, ni kuwa bado rushwa ipo, na nidhamu bado ipo chini kwenye ofisi za umma.
 
Back
Top Bottom