Naam, wana JF!
Katika pita pita zangu kwenye majiji na miji ya kibiashara nimeshuhudia jinsi ambavyo nguvu ya Chadema miongozi mwa wajasiriamali wadogowadogo maarufu kama wamachinga inavyopungua kwa kasi. Kitendo cha Raisi kuagza wamachinga wasibugudhiwe na baadaye wizara ya fedha kuja na sera ya kuwatambua wamachinga na kurasimisha shughuli zao, limepunguza kwa asilimia zaidi ya 90 vijana ambao walikuwa muda wote tayari wako kufanya maandamano kwani hawakuwa na cha kupoteza.
Kwa sasa vijana wengi wamejikita kwenye ujasiriamali hivyo imekuwa ngumu sana kutumiwa na wanasiasa kuandamana bila sababu zisizokuwa na maslahi yao. Kwa miaka ya nyuma tulikuwa tukishuhudia jinsi makundi ya vijana yalivyojitokeza kuhudhuria kesi za akina Mtikila na Mrema lakini jana pamoja na Chadema kutangaza na kuhamasisha mahudhurio kwenye kesi hiyo kuoitia mitandao hadi ahadi ya posho lakini mahudhurio yalikuwa hafifu na waliohudhuria walikuwa ni 'makamanda'. Wengi walitoka wanasikitika kwani walikuwa wanataka itokee fujo ili angalau mabomu ya machozi yapigwe lakini ikawa kinyume na matarajio yao.
Niseme tu hili ni pigo kubwa kwa Chadema inayotegemea kuendeshwa kwa kutumia maandamano, vituko na kesi.