Hili la Serikali ya Magufuli kuwatambua wamachinga ndilo pigo kuu dhidi ya CHADEMA kuelekea 2020

Basham

JF-Expert Member
Oct 10, 2014
743
429
Amani iwe kwenu Wana Jamvi

TRA imeamua kuwasajili wamachinga wote kutambulika ili waweze kulipa kodi kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi yetu

Kwa hili kwa kweli sina budi kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuliona hili litasaidia sana kuongeza mapato na kuweza kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo mbele

Ila cha msingi wawawekee mazingira rafiki ya kufanyia kazi, Kadirio la kodi liendane na kipato cha machinga

Nawasilisha
Bm
 
Naam, wana JF!

Katika pita pita zangu kwenye majiji na miji ya kibiashara nimeshuhudia jinsi ambavyo nguvu ya Chadema miongozi mwa wajasiriamali wadogowadogo maarufu kama wamachinga inavyopungua kwa kasi. Kitendo cha Raisi kuagza wamachinga wasibugudhiwe na baadaye wizara ya fedha kuja na sera ya kuwatambua wamachinga na kurasimisha shughuli zao, limepunguza kwa asilimia zaidi ya 90 vijana ambao walikuwa muda wote tayari wako kufanya maandamano kwani hawakuwa na cha kupoteza.

Kwa sasa vijana wengi wamejikita kwenye ujasiriamali hivyo imekuwa ngumu sana kutumiwa na wanasiasa kuandamana bila sababu zisizokuwa na maslahi yao. Kwa miaka ya nyuma tulikuwa tukishuhudia jinsi makundi ya vijana yalivyojitokeza kuhudhuria kesi za akina Mtikila na Mrema lakini jana pamoja na Chadema kutangaza na kuhamasisha mahudhurio kwenye kesi hiyo kuoitia mitandao hadi ahadi ya posho lakini mahudhurio yalikuwa hafifu na waliohudhuria walikuwa ni 'makamanda'. Wengi walitoka wanasikitika kwani walikuwa wanataka itokee fujo ili angalau mabomu ya machozi yapigwe lakini ikawa kinyume na matarajio yao.

Niseme tu hili ni pigo kubwa kwa Chadema inayotegemea kuendeshwa kwa kutumia maandamano, vituko na kesi.
 
magufuli kuwin wamachinga ni pigo kubwa saba kwa chadema..

leo magufuli akipita tu kariakoo wamachinga wanamshangilia mpaka unahisi upinzani haupo tena...

magufuli akiwawin na boda boda tu na mama ntilie chadema itapata shida sana na sana uchaguz ujao na ujao na ujao...
 
Usifikili wamachinga ni wajinga kama wewe.
Kuwatambua ili muweze kuwakamua hadi noti yao ya mwisho?
Wamachinga hawa wanaokula sasa mulo mmoja ndio uanaosema wanampenda malaika mtukufu?
Machinga hawa ambao wengi wao wameshindwa kupeleka watoto shule kwa kushindwa kupata mahitaji yao ndio wamshangilie mkulu
Wamachinga hawa ambayo wengi wao wamefunga biashara zao kwa mzunguko mdogo wa kifedha ndio hao waje kumshangilia malaika?
Ukitaka kuona wamachinga hawako pamoja na uchwara wako hebu ruhusu democrasia ifanye kazi uwone.
Unajua ni ujinga usio kifani kumsifia bondia wako kuwa ni hodari ulingoni wakati wapinzani wake unawafunga mikono wakati wa mapambano.
Aibuuuu!!¡!!
 
Mkojo wa Lissu umekuwa deal Lumumba wanaupigania kwa udi na uvumba kwamba ni kimiminika muruwa sana.
 
Mnasema wamachinga wakati mmeongeza rate ya unempolyemnt? Kuna vjana kibao wanasubir hyo 2020 muibe kura. Na waliojitahd kujiajir kwa mitaji ya kuungaunga wako wanasumbuliwa na TRA.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom