mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,772
- 2,171
Mara nyingi Rais Magufuli anapokuwa katika ziara hunukuliwa akisema atatoa fedha zifanye hiki au kile.
Jambo hili limefanyika mara nyingi kiasi kwamba taswira inajengeka kuwa ili sehemu fulani ipate barabara, maji, kituo cha afya, n.k ni lazima Rais atamke.
Kwa uelewa wangu ni kwamba miradi yote inayotekelezwa nchini huwa inatokana na fedha zilizopitishwa na bunge kwenye bajeti husika.
Sasa kama ni hivyo, je ile kauli ya Rais kwamba anatoa fedha za kufanya hiki au kile ziko ndani ya bajeti iliyoidhinishwa na bunge?
Kama iko ndani je ni sahihi ya yeye kusema atatoa fedha? Kama haiko kwenye bajeti je pesa anayoitamka itatoka wapi?
Hayo ndo mambo yanayonichanganya.
Naomba nielemishwe.