Hili la NSSF kutokutoa mafao yetu ni kweli?

Hii ni kweli? Kama ndivyo basi huu utakuwa ni uonevu kwa Watanzania walio poteza ajira na wana hakiba zao huko NSSF
 
NSSF haikuwa na wateja wengi kama PPF,wamekaza upande mmoja(PPF) ili kuinusuru NSSF,sasa PPF nayo wateja hamna kama zamani NSSF inafungiwa kuipa ahueni PPF,huu ndio mchezo ninao uona hapa
 
Nasikia wanatoa baada ya miazi SITA ila kama hujapat kaz sehemu yoyote na Kama umepata kazi huwezi pata nnsf
 
Kwa sasa wameruhusu ila kwa sharti kua lazima mtu awe terminated au amekimbiwa na mwajiri au anataka kwenda kusoma,hapo atapewa mpunga wake bila zengwe.ila kwa resignation hakuna fao badala yake utaambiwa katafute kazi nyingine.Asanteni
 
Hii ni kweli? Kama ndivyo basi huu utakuwa ni uonevu kwa Watanzania walio poteza ajira na wana hakiba zao huko NSSF

Akiba zinawekwa benki, huo ni mfuko wa pension. Hata jina lake tu linajieleza.
 
Jamani mwenye kufahamu kuhusu mafao ya PPF kama wameshaanza kutoa mafao yetu anijuze niko kijijini nalima .niliona nirudi kijijini baada ya kuachishwa kazi nilipoenda ppf nikaambiwa nirudi baada ya miaka 55 nimebakiza miaka 19 kufika 55 .
 
washaanza kutoa toka trh 10 mwezi uliopita
 
Jamani nasikia nnsf wanakutana tarehe kumi na moja ili kujadili kuzuia mafao ya mwanachama hili limekaaje wakuu
Huu ni uonevu mkubwa sana uongozi wa hii mifuko(serikali) inawafanyia watu wake,hizi pesa ni mwanachama amekatwa na zikawekwa humo si za serikali,hivyo ule utaratibu wa mtu ajira yake inapokoma kwasababu yoyote ile kulipwa pesa zake hili zikamsaidie kujikimu na maisha ikiwemo kutumia kama mtaji wa biashara ni muhimu sana serikali iache hii mifuko iwe huru,hizi pesa ni za wanachama,serikali inapaswa tu linda maslahi ya wanachama na si kutengeneza mazingira ya kuwadhulumu!
UCHAGUZI MKUU UJAO 2020:-
Hii inapaswa kuwa ni ajenda inayopaswa kutumiwa na wafanyakazi wote wa tanzania kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020,mtu atakayejali na kulinda maslahi ya wafanyakazi apewe nafasi!
 
Back
Top Bottom