Hili la Mnyika litajibiwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la Mnyika litajibiwaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiswigo, Aug 9, 2012.

 1. K

  Kiswigo Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miongoni mwa hoja alizozitoa Mnyika kuhusu watuhumiwa wa kashfa ya rada, ni kuwafikisha mahakamani wahusika walioisababishia hasara nchi yetu katika sakata la rada. Hii ni kufuatia maelezo ya Waziri Chikawe kwamba hakuna ushahidi kwamba kulikuwa na rushwa.

  Kwa vile mashitaka siyo ya rushwa tu, kwa nini isifikiriwe kwamba wale waliohusika kushauri na kufanya maamuzi wachukuliwe hatua za kutumia madaraka vibaya au chochte ambacho DPP ataoma kinafaa, badala ya kufunga milango tu as if hakuna kilichotokea. Tumeshuhudia haya kwa akina Mramba na wenzake, Liyumba na hata Jengo wa Benki Kuu na wenzake.
   
 2. n

  ndutu Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika heshima ya seriakali hii imewekwa rehani kama wataalam watashindwa kushauri hatua stahiki kwa wahusika hata kama ushahidi wa tuhuma za rushwa haupo. Kufukia jambo hili chini ya busati kutalifanya liibuliwe miaka michache ijayo.
   
 3. T

  Tiote Senior Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hasa Chikawe amekuwa mwepesi sana kulikanusha hili mpaka unafikiri kwamba ana maslahi binafsi. Huyu jamaa ameamua kufunga ndoa na mafisadi wenzie!
   
 4. w

  watenda Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo la mambo kama haya ni kwamba wakifikishwa mahakamani, hawa hawa ambao leo wana dhamana watakimbilia mahakamani kuwatolea ushahidi na hapo ndipo ninapochoka.
   
 5. m

  mudavadi Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi zile sheria za China huku haziwezi kuletwa? Au tunaogopa kunyimwa misaada? Inakera sana.
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kulingana na sheria zetu, mtanzania anayeishi Tanzania akitaka kufungua account nje ya nchi lazima aombe kibali BOT. Kufungua account nje ya nchi bila kibali cha BOT ni kosa la JINAI na adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka mitatu JELA. (Ingawa hii sheria ni MBOVU kwa maoni yangu).

  I'm sure 100% Chenge wakati anafungia account yake katika kisiwa Jersey hakuomba kibali BOT. Hivyo kama serikali ingekuwa na nia ya kumfunga Chenge ingetumia sheria hiyo kumfunga jela.

  Lakini wapi Chenge afungwe? Nchi itayumba! No wonder aliuwa wale wasichana wawili wa MZA, tena akiendesha gari ambalo halina insurance. Ikaja ikagundulika kwamba alijaribu kugushi insurunace kwa ku back date (kugushi ni kosa la JINAI). Unajua adhabu aliyopewa na mahakama? Tanzania kuna watu wapo juu ya SHERIA na mmojawapo ni ANDREW CHENGE MBUNGE WA BARIADI CCM.
   
 7. b

  banyimwa Senior Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika Tanzania inahitaji muujiza wa Mwenyeezi Mungu maana hapa tulipofika ni pabaya na sijui kama Mungu atakuja kutunusuru kupata viongozi wenye mapenzi ya dhati na watu na nchi hii na kuwaokoa. Sijui nani alimuumba Lowassa na hawa wenzake. Ooh maskini nchi yangu.
   
 8. K

  Kiswigo Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili pia laweza kuwa shitaka la pili na nina hakika wabobevu wa sheria wanafahamu mengi kuhusu maeneo yanayoweza kumtia hatiani huyu jamaa na wale washirika wake. Feleshi upo?
   
 9. K

  Kiswigo Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheria ni ya mwaka 1992 na kwa hakika mazingira sasa yamebadilika. Wanahitaji kuiboresha na kuziba mianya au kuipa meno zaidi kama inavyosemwa kwa lugha ya sasa.
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nina ghadhabu sana!
   
 11. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mahakamani kwenda kufanya nini? Toka lini kesi ya nyani akapewa ngedere? Kwa maoni yangu hiyo itakuwa ni kupoteza muda kwani kuanzia Mkuu wa kaya mpaka choka mbaya wote wanahusika na ufisadi huu wa rada. Kipeni nafasi kikaango cha 2015 kifanye kazi yake
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  It is not possible simply are they not Tanzanians but they are CCM MP and CCM members mwisho .
   
 13. K

  Kiswigo Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo sasa munkari boss. Kwani Mramba siyo CCM?
   
 14. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,336
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  hivi kama leo hii vita ya ndani tunaishindwa tutaweza ya nje? kama tunashindwa kuwakemea na kuwaadhibu waliotuibia na tunawaona wakitunyanyasa tutaweza kweli kulinda mipaka yetu kikamilifu?sijui?
  lakin ushauri wangu kuna aja ya jamii forum ukurasa wa rada uwekwe upya ikiwezekana toka mikataba ilivyokuwa na ukae kwa muda mrefu ili tuendelee kupiga kelele kwa vidole vyetu labda tutapata ufumbuzi. na pia wanasheria acheni uvivu tupeni mazingira ya maana ya kutosha ni kwa vip ihuyu mtu anaweza kushitakiwa ikiwezekana sisi kama jamii tuipeleke kesi mahakamani kama tunaweza kushida.
  nimechoka kuangalia gari zao walizopata kwa kututhurumu.
   
 15. K

  Kiswigo Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na huko Kisutu Mahalu ameibuka kidedea wakati dunia nzima inajua jamaa aliiba. Halafu mnadai independence ya judiciary ambayo ni incompetent. Aibu kubwa!
   
 16. m

  mwabakuki JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  chini ya sheria mpy ya kudhibiti na kuapambana na rushwa MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA ni moja ya makosa yaliyooreshwa na kimsingi yanashitakika na adhabu zake zimeainishwa...kinachoendelea ni sarakasi tu..lakini kwa vile haya mambo ni jinai mbeleni tutashuhudia mengi...ofcoz if n only if CCM is not in power
   
 17. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Mmojawapo wa mashahidi wakuu upande wa utetezi wa Mahalu alikuwa ni yule yule mzee wa 'uwazi na ukweli' ambaye dakika za mwisho za ukaazi wake pale Magogoni kwa mfugarushwa alijimilikisha mgodi wa umma wa Kiwira. Baada ya wanaharakati kuuvalia njuga huo WIZI akina 'Maisha bora kwa kila Mtanzania' na LIWALO NA LIWE wakamsihi aurejeshe kimya kimya serikalini. Haya sasa peleka hizo kesi Kisutu: pesa ambazo zingeweza kutumika angaa kuwatoa watoto wa shule sakafuni na kuwaweka katika madawati zitaishia kuendesha kesi FEKI.
   
 18. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  haya yote ni majambazi na yanaiba huku yamevaa suti mchana kweupe na wakati mwingine na viyoyozi vinayapepea, mi ninauhakika haya majambazi ipo siku tutayachoma moto hata kama ni makaburi yao potelea mbali hata kama yatakuwa yalishakufa. naomba Mwenyezi Mungu atujaalie uzima tulitimize siku moja. tujitahidi kuwahamasisha wanavijiji huko waamke, tulipige chini hili li ccm jamaniiii Arrrrrrrrrgggggggggggggghhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Nilipatwa na mshtuko siku Benjamin Mkapa alipoenda kutoa ushahidi akimtetea Prof. Mahalu, nilidhani kesi imeishia pale. Kwa yaliyojiri leo nadhani nilipaswa kuamini hisia zangu siku ile.

  Mahakama na sheria zetu kwa ujumla ni kwa ajili ya kuumiza wanyonge na kuwafaidisha wakubwa. Kama hapakuwa na ushahidi wa kumtia Prof hatiani why all the fuss? kwanini serikali ilifungua kesi? Kwa gharama ya nani? Kwa faida ya nani?

  Huu usanii na uzebe utakoma siku tu ccm wakiwa mojawapo ya vyama vya upinzani nchini Tz.
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Unauhakika ni yeye aliyewagonga wale wasichana? au kwa vile yeye alikubali kuuvaa uhusika wa tukio lile? Hii ni Tanzania ndugu yangu.
   
Loading...