Washa king'amuzi cha Azam, tune channel namba 122. Halafu jikumbushe historia ya maisha ya Diamond Platinumz, kutoka kwenye kuiba cheni ya mama yake hadi sasa kuweza kumiliki TV, acha tu namna analipaisha jina la Tanzania katika tasnia ya muziki, acha tu anavyowalazimisha wageni kujifunza kiswahili ili waweze kuimba nyimbo zake, ukishayatafakari hayo bila shaka utajua kwa nini anapata heshima ya kutambulishwa. Usisahau pia kuwa ni muwakilishi wetu katika mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika huko Russia. Bila kusahau kuwa ndiye yeye pekee aliyepeperusha bendera ya Tanzania katika kombe la mataifa ya Africa.