Hili la Mama Kanumba linajitaji tafakuri ya kina

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
277,402
720,836
Si wakati wa kumcheka ama kumsimanga bali ni wakati wa kumsaidia kwa kila hali... Haya anayopitia yanahitaji faraja na kupewa moyo... Lakini ni lazima tafakuri iwepo ili tupate cha kujifunza.

Ni mama maarufu na umaarufu wake ungekuwa maradufu kama mwanae Kanumba angekuwa hai kama ilivyo kwa mama chibu dangote.... Lakini pia amefanya jitihada nyingi ili asisahaulike kwenye ulimwengu wa media za kibongo... Kupitia waandishi uchwara.

Ni mwanamke ambaye kwa wakati mmoja alijiona mwenye bahati kubwa na kushukuru uzao wa tumbo lake wenye matunda yenye faida... Marehemu Steven Kanumba alitarajiwa kuja kuwa future legend wa sinema za kibongo... Alikuwa na kipaji na nyota ya jaha ikamuangukia... Hakuna mzazi asiyependa mwanae asiwe kama Kanumba... Upcoming artist mwenye kipaji na ndoto nyingi.

Ni katika hatua hii ya kusimama.. Maisha ya Kanumba yakakatishwa ghafla... Si kwa ajali ya gari kama marehemu James mtoto wa Dandu.... Wala si kwa ajali ya ugomvi wa visu mapanga na shaba... Ilikuwa ajali ya kujihami kwa mpenzi wake mdogo Lulu... Ajali iliyotokana na wivu wa mapenzi... Kanumba akazimika ghafla... Lulu katika umri wake mdogo naye nyota ikiwaka na Bola uzoefu wa mikikimikiki ya maisha akaenda lockup kwa kesi ya mauaji

Lilikuwa ni tukio lililoleta taharuki kubwa na maumivu mengi kwa familia zote mbili pamoja na wapenzi na mashabiki wa pande zote mbili

Habari kamili inaanzia hapa.. Mama Kanumba akaonesha rangi zake halisi juu ya mtuhumiwa wa mauaji ya mwanae... Akamlaani kiasi cha kufikia kumuita shetani mkubwa... Na siku Lulu anahukumiwa huyu mama aliangua kicheko cha furaha... Kosa kubwa sana hili la kwanza

Likaja kosa la pili... Kuamini kuwa Kanumba hakufa. Yuko hai mahali fulani.. Akalia na kusononeka kiasi cha kumkufuru Mungu kama vile yeye ndio wa kwanza kufiwa. Wauza habari uchwara wakapata pa kupigia bingo... Akaitwa huku na kule akafanyishwa mahojiano mengi... Akafunguka mengi... Kamwe hakukubali kuwa ile ni kazi ya Mungu na maisha lazima yasonge.

Ni kwenye kilele cha hili ndio habari za kwamba kanumba yu hai zikazidi kushika kasi. Manabii na mitume bandia nao wakaingia humo humo... Wachawi na walozi pia hawakubaki nyuma. Kila mmoja akijinasibu kumfufua marehemu Kanumba. Wa mwisho alikuwa nabii Flora wa mwanza huyu aliweka live event kabisa lakini naye akaishia blah blah tu huku akiwa keshajitangaza na kupiga ndefu.

Baada ya tukio hili ndio mama Kanumba akagundua kuwa anatumika tu na hakuna ufufuo wala ufufuko wa mwanae mpendwa... Lakini hili lilikuja kwa kuchelewa mno na baada ya kukufuru sana..

Maisha sio leo na siku hazigandi. Lulu alitoka kifungoni kwa msamaha... Kapitia aliyopitia lakini yuko hai... Akiwa na majinamizi mengi moyoni.. Mama Kanumba aliyejaaliwa watoto wawili tu nadhani wa kiume. Mmoja aliyefariki Kanumba na huyu Seth ambaye sasa kafanyiwa upasuaji wa mgongo na anaweza kuwa mlemavu maisha yake yote yaliyobakia....

Ni maumivu makubwa kwa Seth. Ni pigo pia kwa familia ndugu jamaa na marafiki. Natamani ufanyike muujiza apone. Lakini nabaki najiuliza je kuna wakati matendo ya mzazi hayawezi kuleta mapigo kwa watoto?

Kama mama Kanumba alimuona Lulu ndio shetani aliyeta madhila makubwa kwenye familia hata kufikia kukufuru... Je huyu anayeumwa sasa tena ugonjwa wa kupooza atamlaumu nani?

Kuna hili pia la mzazi wa pili.. Tunayemjua na kumfahamu sana ni mama Kanumba je baba watoto hawa yuko wapi? Je kuna mahali wazazi hawa walishindwa kuelewana na kuneneana mabaya?

Huwa nayatazama maisha kwa tafakuri ya tahadhari mno. Kwakuwa kila kitu kina majira yake na mashaka yake na kushinda kwake na kushindwa kwake na furaha zake. La muhimu ni kuchunga mdomo wakati wa furaha kubwa na simanzi pia.

Tuungane pamoja kwenye hii tafakuri huku tukimwombea Seth pale kitandani ili kama kuna maapizi na malipizi ya wazazi vimpitie mbali.

Katika vitu ambavyo huyu Mama alikosea ni kumnenea mabaya Mzee mwenzie(Baba Kanumba), na yule Mzee alikuwa mstaarabu aliyepitiliza, kwani aliomboleza kifo cha mwanaye kimya kimya.Mama Kanumba yeye alisimama kwenye mali, hakutaka alichochuma mwanaye kiguswe na Baba Kanumba, labda tokana na bifu walizoachiana toka enzi,
Mungu mkali R.I.P Kanumba.
 
Usisahau hata lulu na mamake walimtukana mama kanumba,ndo huyu mama akashikwa na uchungu kuona mwanae kafa na mdhaniwa kaachiwa nje na badala ya kumfariji anamtukana.

Ni mzunguko wa matukio.hata lulu nae ana yake kesho hayajui.
Kikubwa ni pale unapokumbwa na haya mambo ya kuumiza uombe Mungu akupe hekima ikuongoze.mfano kwa sasa lulu hatakiwi kumcheka wala kufurahia haya.Bali aonyeshe hururma na support na kufanya kama vile hakikutokea kitu kutoka kwa huyu mama.
Nawashangaa Wanaonishangaa Mimi Kucheka Mahakamani Wakati Lulu Anaukumiwa Hata Mimi Nililia Wakati Wengine Wakila Bata- Mama Kanumba
 
Mmh yaliyomo yamo
Katika vitu ambavyo huyu Mama alikosea ni kumnenea mabaya Mzee mwenzie(Baba Kanumba), na yule Mzee alikuwa mstaarabu aliyepitiliza, kwani aliomboleza kifo cha mwanaye kimya kimya.Mama Kanumba yeye alisimama kwenye mali, hakutaka alichochuma mwanaye kiguswe na Baba Kanumba, labda tokana na bifu walizoachiana toka enzi,
Mungu mkali R.I.P Kanumba.
 
Sina uhakika ila mwezi uliopita hapa Kijiweni kuna mwenzetu bajaji yake ilipinduka. Akasagika uti wa mgongo, ikafanywa opereshen kwa tahadhari kua hatotembea tena, ila bahati mbaya juhudi hazikuzidi mapenzi ya Mungu.

So reference ya swali langu ni hiyo scenario as uzi umesema upasuaji wa mgongo na siyo upasuaji wa uti wa mgongo.
Tofauti ninini?
 
... .. Mama Kanumba aliyejaaliwa watoto wawili tu nadhani wa kiume. Mmoja aliyefariki Kanumba na huyu Seth ambaye sasa kafanyiwa upasuaji wa mgongo na anaweza kuwa mlemavu maisha yake yote yaliyobakia.....
Si kweli kuwa alikuwa ana watoto wawili tu. Kabla ya Kanumba, alishazaa watoto wawili wa kike, kutoka kwa wanaume wawili tofauti. Kanumba alikuwa ni wa tatu kuzaliwa, ambaye naye alikuwa ana baba yake.
 
Asante ndio maana nikatumia neno NADHANI pia kwenye mahojiano na babayake nimeona akiwataja hao wengine... Asante kwa ufafanuzi bila kashfa wala kejeli
Si kweli kuwa alikuwa ana watoto wawili tu. Kabla ya Kanumba, alishazaa watoto wawili wa kike, kutoka kwa wanaume wawili tofauti. Kanumba alikuwa ni wa tatu kuzaliwa, ambaye naye alikuwa ana baba yake.
 
Tofauti ni ndogo sana kati ya uti wa mgongo na mgongo... Kwakuwa kwa asilimia 90 mgongo unaundwa na uti
Sina uhakika ila mwezi uliopita hapa Kijiweni kuna mwenzetu bajaji yake ilipinduka. Akasagika uti wa mgongo, ikafanywa opereshen kwa tahadhari kua hatotembea tena, ila bahati mbaya juhudi hazikuzidi mapenzi ya Mungu.

So reference ya swali langu ni hiyo scenario as uzi umesema upasuaji wa mgongo na siyo upasuaji wa uti wa mgongo.
 
Katika vitu ambavyo huyu Mama alikosea ni kumnenea mabaya Mzee mwenzie(Baba Kanumba), na yule Mzee alikuwa mstaarabu aliyepitiliza, kwani aliomboleza kifo cha mwanaye kimya kimya.Mama Kanumba yeye alisimama kwenye mali, hakutaka alichochuma mwanaye kiguswe na Baba Kanumba, labda tokana na bifu walizoachiana toka enzi,
Mungu mkali R.I.P Kanumba.
Dah dunia inakwenda kasi sana
 
Kwa mzazi yeyote hili ni pigo kubwa sana,ikimaanisha uzao wake umekuwa ni wa mateso hakuna furaha.Kwa wakati huu huyu mama anahitaji faraja pamoja na mazingira mengine yanayohusu maisha yake na mtoto wake waweze kuishi vizuri.Kwa sasa haina haja ya kumfikiria yeye 'negatively',kwa sababu kilichomkuta kinaweza kumkuta mtu yeyote yule.Na ubinadamu ni kujaliana kwenye shida na matatizo.
 
Mheshimiwa umeongea kitu kizuri katika maisha ya binadamu,Mungu ni wa wote,tumwombee tu atamponya.
 
Back
Top Bottom