Hili la maiti kulipishwa madeni Hospitali za Serikali limekaaje?

Dada nlikuwa nakuona mtu mwenye akili kumbe zero kabisa.

Kwamba hospitali za serikali mnaweza kuuza nyumba kukomboa maiti?. Like seriously? Are you sane?

Naomba nikuulize swali dogo tuu, kwa nini msilipie gharama za matibabu kabla hajapatiwa huduma? Kwa nini msubiri mpaka wakati wa kuruhusiwa au mpaka afariki ndipo muanze kujenga picha ya kulipishwa maiti wakati kiuhalisia mnalipia huduma alizotumia ndugu yenu kabla hajafa?.

Unforgetable
mama yk akiumwa mpeleke pale wakamuwaishe ili upate kulithi pagale
 
Juzi tu hapa mtaani kuna jamaa kapata ajali akaenda kufia hapo wanaenda kufatilia mwili wanakuta deni laki tatu na usheee yaan ndani ya masaaa tu hapo nilichoka ...kwa kweli itafutwe namna ya kuwasaidia watu
Ha ha ha mkuu kwani huduma ya hospitali inachajiwa kwa masaa au kwa huduma mtu aliyopatiwa?

Hata ndani ya nusu saa tu unaweza ukachukuliwa kipimo chenye thamani ya laki 5
 















Wewe Mina cute unapenda sana kulalamika, unatamani kila kitu kingekuwa bure. Unaonekana ni mtu ambaye ukiwa na tatizo basi unahisi unastahili kuonewa huruma na kila mtu.

Lazima ujue palipo na haki pana wajibu na palipo na wajibu pana haki pia. Jifunze kutimiza wajibu wako pale unapotaka haki

manengelo
 
kwanza pole na kufiwa na mzee wako. hospital za serikali zinatoa huduma wala hazifanyi biashara na zinatumia kodi zetu lakini zimekuwa zikijali sana pesa kuliko utu zingekuwa hospital za private wala nisingeshangaa inabidi wajirekebishe
 
kwanza pole na kufiwa na mzee wako. hospital za serikali zinatoa huduma wala hazifanyi biashara na zinatumia kodi zetu lakini zimekuwa zikijali sana pesa kuliko utu zingekuwa hospital za private wala nisingeshangaa inabidi wajirekebishe
asnte
 















Wewe Mina cute unapenda sana kulalamika, unatamani kila kitu kingekuwa bure. Unaonekana ni mtu ambaye ukiwa na tatizo basi unahisi unastahili kuonewa huruma na kila mtu.

Lazima ujue palipo na haki pana wajibu na palipo na wajibu pana haki pia. Jifunze kutimiza wajibu wako pale unapotaka haki

manengelo
Ningejua ni mamaa malalamiko wala nisingejibishana naye

Kumbe alishaona hospitali za serikali hamna kitu lkn akampeleka baba ake hospitali ya serikali tena? What a zero brain.


Unforgetable
 
Mama wa vitonga

Screenshot_20191115-182012.jpeg
 
Unajifanya hujui kwamba kuna watu hawawezi hata kulipia hiyo bima.

Kwa kuwa wewe unalipiwa bima ndio unachukulia rahisi.
Unajua wanao lalamika wanapitia wakati mgumu kiasigani pindi wanapo kutana na janga kamahilo.

Acha kujifanya mjuaji.
Kwahiyo mwanafunzi anayepata division 0 huwa hawalipii ada?

(huo ni mfano mwepesiiii tu, maana unaonekana akili yako ni nzito sana)
 
Tatizo tunapenda lawama na kutafuta cheap popularity tu! Kabla ya kuwa Marehemu alikuwa mgonjwa na alihudumiwa kama mgonjwa na kupewa dawa. Kuna gharama zake. Alipofariki akawa Marehemu kuna gharama za kuhifadhi Marehemu. Jumla inakuwa laki 7. Je unataka kuniambia mgonjwa akifariki daktari alokuwa anamtibu asilipwe mshahara? Je akiwa Marehemu mortuary attendant, ajitolee bure, je umeme wa jokofu Tanesco wautoe bure? We need to be realistic na ndo maana bima ya Afya muhimu. Hakuna Huduma ya bure hapa TZ baada ya ujamaa ndugu yangu Mina cute
Mtanzania kukuelewa ngumu sanah.. Tunapenda sanah vya bure
 
Nini maana ya hospitali za serikali??
Mkuu watanzania ni watu wa ajabu sana,kuna mtu akishakuwa na uwezo wa kupata shilingi mia anaona anayepata hamsini au hapati kabisa ni mzembe kupitiliza. Tutaendelea kuburuzwa hivyo hivyo kwa mentality hizo. Jaribu hata kupima kauli ya yule muheshimiwa wa digrii nne,kuna ubaguzi wa kujiona yeye ni bora kuliko wengine
 
Habarini wapendwa,

Wiki hii mzee wetu alikuwa anaumwa Hernia, tarehe 07/11/2019 tukampeleka Mloganzila hospital akitokea hospitali ya Bagamoyo, kufika kule usiku akafanyiwa upasuaji, saa kumi alfajiri akafariki. Sasa tarehe 08/11/2019 tukaenda ili kuchukua mwili wa marehemu akazikwe.

Kufika pale tunaambiwa marehemu anadaiwa jumla ni Tsh 775,000/= tukalalamika mbona hela nyingi hivyo, wakatuambia nendeni ustawi wa jamii labda wanaweza kuwasaidia mkilalamika kuwa hamna uwezo, kwenda kule tukaambiwa kuwa hata iko kiasi mlichotajiwa kapewa punguzo sababu katokea hospitali ya Serikali kuja hapa, kukosa hivyo ingekuwa mara mbili yake.

Tukasema sawa, ndugu wakachangishana ikafika laki sita na ishirini, kuipeleka kule bado wakagoma, wakasema hadi hela itimie yote isipungue hata mia ndo maiti itatoka, basi tukapigia simu watu baki kuwakopa hela ikatimia tukaenda kupeleka tukapewa mwili wa marehemu. Sasa najiuliza hivi huu utaratibu wa kudai maiti ni haki kweli? Mtu amekufa bado mnamdai, sio laana kweli.

Kuna wapemba tumewakuta wanadaiwa milioni tatu za maiti wao, wameshauriana waende wakafanye kisomo cha kuswalia maiti pale hospitali, wakimaliza waondoke mwili wauache pale pale Mloganzila, wao wataisabu kama ndugu yao amekufia baharini na maiti haikupatikana kuliko kulipa hela hiyo.

Hii ni kweli jamani wala sio jambo la kutunga, marehemu katuachia madeni.

Zaidi, soma:


Kuna Mbunge mmoja nadhani Kahama alishalizungumzia hili lakini kama kawaida ya wabunge wetu wengine walicheka na wengine wakapiga makofi kana kwamba ni mzaa flani hivi,ila nakumbuka kauli yake moja tukumbuke sisi wote ni marehemu watarajiwa
 
Kimantiki kabisa ilipaswa kama mgonjwa akifia hospital basi gharama zote zifutwe..

na hilo lingeongeza ufanisi wa matabibu ktk kumhudumia mgonjwa

kuhakikisha wanapigana kufa na kupona mgonjwa aishi na wapate malipo stahiki kwa haki

nawasilisha
Hi unaamin mtu anaweza kukuponya kaam siku yako ya kufa imetimia kwel.?
Yaan ukipona jua n mpango wa Mungu tu kufa kupo pale pale n kwa vile hatujuibsiku wala saa.
 
Back
Top Bottom