Nuraty J
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 1,729
- 3,829
Habarini wapendwa,
Wiki hii mzee wetu alikuwa anaumwa Hernia, tarehe 07/11/2019 tukampeleka Mloganzila hospital akitokea hospitali ya Bagamoyo, kufika kule usiku akafanyiwa upasuaji, saa kumi alfajiri akafariki. Sasa tarehe 08/11/2019 tukaenda ili kuchukua mwili wa marehemu akazikwe.
Kufika pale tunaambiwa marehemu anadaiwa jumla ni Tsh 775,000/= tukalalamika mbona hela nyingi hivyo, wakatuambia nendeni ustawi wa jamii labda wanaweza kuwasaidia mkilalamika kuwa hamna uwezo, kwenda kule tukaambiwa kuwa hata iko kiasi mlichotajiwa kapewa punguzo sababu katokea hospitali ya Serikali kuja hapa, kukosa hivyo ingekuwa mara mbili yake.
Tukasema sawa, ndugu wakachangishana ikafika laki sita na ishirini, kuipeleka kule bado wakagoma, wakasema hadi hela itimie yote isipungue hata mia ndo maiti itatoka, basi tukapigia simu watu baki kuwakopa hela ikatimia tukaenda kupeleka tukapewa mwili wa marehemu. Sasa najiuliza hivi huu utaratibu wa kudai maiti ni haki kweli? Mtu amekufa bado mnamdai, sio laana kweli.
Kuna wapemba tumewakuta wanadaiwa milioni tatu za maiti wao, wameshauriana waende wakafanye kisomo cha kuswalia maiti pale hospitali, wakimaliza waondoke mwili wauache pale pale Mloganzila, wao wataisabu kama ndugu yao amekufia baharini na maiti haikupatikana kuliko kulipa hela hiyo.
Hii ni kweli jamani wala sio jambo la kutunga, marehemu katuachia madeni.
Zaidi, soma:

Waziri Ummy Mwalimu, hili la kuzuia maiti ni unajisi wa mila zetu za kiafrika. Litazameni vizuri
Kwa muda sasa watu wamepaza sauti kuhusu mamlaka za taasisi zinazotoa tiba za kisasa-hospital na zahanati kuzuia wafiwa kuchukua miili za wapendwa wao mpaka walipie gharama za matibabu. Mantiki yake haieleweweki na wala haikubaiki kwa mila zetu sisi waafrika. Haikubaliki pia kwa wafrika...
www.jamiiforums.com
Hatimaye Muhimbili wameturuhusu kumzika mpendwa wetu!
Salaam! Wadau mtakumbuka wakati nikichangia uzi wa mdau mmoja juzi uliohusiana na Muhimbili hospital nilieleza kisa cha binti wa darasa la tatu kuungua moto na baada ya kufariki wazazi waliambiwa wanatakiwa kulipa milioni 40 zilizotokana na matibabu ndipo waweze kupewa mwili. Binti huyu wa...
www.jamiiforums.com