Hili la kwenda shule na condom na ndizi liko sahihi wanajamvi?

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
10,911
13,229
Wasalaam,

Iko hivi, kuna shule moja ya msingi hapa mjini wa darasa la sita wameagizwa waende shule na kondom na ndizi kwa ajili ya practical ya somo la sayansi kujifunza jinsi gani ya kutumia kondom.

Binafsi nimebaki na maswali mengi kichwani mwangu kama inawezekanaje watoto wafundishwe kitu kama hicho, ila kama lipo kwenye syllabus naomba nijulishwe.
 
Sina uhakika kama liko katika mitaala ya masomo yao, bali kuna umuhimu wa watoto kujua tahadhari wanazotakiwa kuchukua wanapojikuta katika mazingira hayo, maana dunia hii ngono imeanikwa kila sehemu, ila uzuiaji uj a uzito/ maambukizi ni siri.
 
Mkuu mimi naona kama darasa la sita wa Sasa bado wadogo sana, mfano huyu dogo aliyokuwa analiongea kwa kuropoka bila aibu yoyote mpaka mimi nikaona aibu
 
Kuna haja ya wazazi kufuatilia kwa ukaribu yanayoendelea shuleni na wao pia kuwatahadharisha watoto wajue unyeti wa hilo suala na pia hatari zake. Kwa mtoto mdogo kams huyo kuliongelea kama suala la kawaida, inaelekea kalijua kutokea kwa waalimu ambao hawakutilia maanani umuhimu wa kuwa ni suala nyeti katika jamii na hasa umri unapohusika.
 
Kweli kabisa
 
Ni sawa kabisa kumfundisha elimu hiyo, kwani mtoto hua na kichwa chepesi sana cha kushika mambo, na pale ukimueleza madhara yake basi itamjenga kichwani kua ni kitu kibaya, hata siku ikija tokea mtu akamshawishi inakua rahisi kwake kutoka ndukiiiii.

Kizazi hiki cha dotcom hakika kipo kwenye hasara kubwa, kwani ni kizazi cha wajuaji, kizazi cha wadadisi, kizazi cha uwazi na ukweli,
Hivyo wazazi msisite kuzungumza na watoto wenu, mtoto wa miaka 12 wamuona mdogo ila akili yake ni kubwa na kuna waharibifu huko nje wanamtolea macho.

Naunga mkono hiyo elimu.
 
Sasa si ndio mwanzo wa yeye kufanya practical?
 
kufundisha watoto jinsi ya kutumia kondomu ni kuwaalika watoto wafanye ngono wanavyojisikia kwa kiburi cha kutokuambukizwa. hii si sawa kimaadili. kwanza ni wadogo sana. pili kondomu hata kwa watu wazima haikubaliki kimaadili kwani inachochea ngono nje ya ndoa na inapingana na mpango wa Mungu wa uumbaji. kwa watu wazima kama ni uzazi wa mpango upo wa asili na siyo wa kondomu na vidonge na sindano za kuzuia mimba.
 
Sasa swali linakuja, je lipo kwenye syllabus au mwalimu kaamua kufanya yeye
 
Ni muhimu kufundishwa Kwan bila ya Kufanya hivyo(kuwafundisha) madhara yatakuwa mengi sana binafsi nishawah kuona Kitaa mtot wa drsa la 6 kapewa ujauzito ,akifundishwa Itakuwa rahis kwake kuelew madhara yake Kwan mtoto huwa mwepes kuelewa.wazazi wasisite kuongea na watot wao coz utandawaz Uko juu sana siku hzi , nafikir hyo ni moja ya teaching aid mzur
 
nimeuliza walimu husika wamesema ni kweli kuna mafundisho juu ya namna ya kujikinga na maambukizi. ila kimaadili si sawa. hawa ni watoto wadogo. kuwafundisha kutumia condom ni kuwaambia wafanye tu. waelimishwe kwamba umri wao wa kufanya mapenzi ni mdogo wasubiri wakati ukifika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom