Hili la Kuteua Mwenyewe na Kutengua liangaliwe kwa umakini kwani litakuza kiwango cha Upigaji na Rushwa nchini

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,892
109,610
Nashauri Rais anapoapishwa tu apewe muda fulani kwa Kutulia ili aweze Kuchagua Watendaji alio na uhakika nao Kiufanisi ili anapowateua basi wafanye Kazi na siyo kuteua Watu (Watendaji) kwa Kubeti au Kubahatisha kama inavyoonekana sasa.

Kwa Mtazamo wangu GENTAMYCINE hasa kwa hii tabia ya sasa ya Marais Wetu Kuteua na Kutengua itazalisha Upigaji na Rushwa Kuongezeka kwa Watendaji Wanaoteuliwa kwakuwa watakuwa wanajua hawana uhakika wa Kudumu katika Nafasi zao hivyo cha Msingi ukishateuliwa (Ukishaula) anza Kwanza Kuiba (Kupiga) na Kuchukua mno Rushwa ili hata Rais akija Kukutumbua tayari Wewe umeshajikamilisha Kiutajiri na kwamba hutoathirika Kimaisha.

Na. nina uhakika hiki nilichokielezea hapa ndiyo kipo sasa on the ground ndiyo maana unaona wale Wote wanaotumbuliwa hakuna mwenye Kujali au mwenye Nyuso ya Huruma au hata ile ya Usununu (Kuchukia) bali Wote huwa Kawaida huku wakichekea Matumboni mwao, wakimcheka Kimoyomoyo aliyewatumbua kuwa amechelewa kwani Wameshajitajirisha vya Kutosha kwa muda aliowaamini kwa Mtindo wa Kubeti na Kuwabahatisha.

Wateuliwaji waaminiwe ili Wadumu!
 
Yes/No, kwangu ni kuwa na Katiba Mpya, katiba hii itampa sitting president uwezo wa to hire and fire only cabinet members, wengine wote ni lazima waombe na interview zifanyike kwa kuhusisha Bunge, wanapoharibu ni wajibu wa Bunge kuchukua hatua, na kuwafukuza ni lazima 2/3 ya MPs waridhie,hawa CEOs ni kama mkuu wa police, DPP, Mkuu wa Majeshi etc etc, kinyume chake tutaendelea kushuhudia haya.
 
Back
Top Bottom