Uchaguzi 2020 Hili la kuondoa vitambulisho vya machinga umebugi stepu

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,301
10,347
Mh Lissu katika pitapita yake kasema atafuta vitambulisho vya machinga. Hapa amechemka mwambieni Bora aseme ataboresha usimamizi.

Hivi vitambulisho vimewasaifia kuondokana na misako ya maofisa wa TRA na mgambo wa jiji. Kumbuka wengi wa wenye hivi vitambulisho Ni wenye vibanda vidogo mtaji wao haufiki 5m, wauza screpa wauza chupi, vibanda vya mpesa, wachoma chips, mamalishe.

Hawa ndio walikuwa chumaulete wa mabwana afya, afisa biashara, tra mgambo wa jiji, maafisa wa zimamoto, wenyeviti wa mitaa, watendaji kata, Hawa wote walikuwa wakipitisha msako na kuchuma fedha.

Leo hii kijana anauza madela kaweka kitambulisho Cha machinga haguswi, ukivifuta manake waanze kusakwa Tena. Kwahili aliyekuambia useme changanya na za kwako.
 
Lilikuwapo la
1. Covid 19
2. Machinga vitambulisho
3......

Awe na watu wamsaidie aache hii
One man show
La sivyo tutajua hawajajipanga, hata hivyo sio rahisi kushinda hata kwa kura za kuhesabu mikono.

Humu mitandaoni tudanganyane tu.
Niko hapa Itope nakula usipa
 
Jaribu kuwa muelewa, kinachotakiwa kumlinda mmachinga sio kitambulisho, bali kuwepo na kanuni zinazotambua haki za machinga kisheria.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
Tatizo kubwa la hawa vijana wa Lumumba huwa wana soma kichwa cha habari tu. Wasamehe maana ndio mwisho wa uelewa wao.

Ukiwauliza hizo 20,000/ zina kwenda wapi hakuna mwenye jibu. Ukiwauliza zina fanyia nini hakuna atakae kujibu. Yaani ni tatizo sana kujadiliana na slow learners.
 
Wajasiriamali duniani kote ulindwa na sera bora sio kitambulisho!
Term kitambulisho inawatoa akili mno.

Wewe uliwahi kuwaza kuwa wamachinga watachangia pato la Taifa lao?

Nyie ndo mnaopiga ramli nchi iendeshwe kwa mikopo na misaada ya kipuuzi kutoka nje.

Tutakopa mikopo yenye akili
Tutakusanya kodi
Tutaendesha nchi
 
Jaribu kuwa mwelewa, kinachotakiwa kumlinda mmachinga sio kitambulisho, bali kuwepo na kanuni zinazotambua haki za machinga kisheria.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
Kumbuka ukiweka kanuni pia watalazimika kukaa maeneo maalum tofauti na sasa ambapo utawakuta hadi masaki.

Kwa hiyo bado watarudi kule kule walikotoka na wengi wao hawaamini kukaa sehemu moja.
 
Matumizi ya hivi vitambulisho vya wamachinga si sawa, vinatumika vibaya kwani kuna wafanyabiashara wenye mtaji mkubwazaidi ya 20m wanavitumia.

Kinachohitajika ni sera na sheria nzuri ziwekwe ili kuwalinda na kuwainua hao wamachinga.

Hivi vitambulisho ni mradi wa watu fulani ndiyo maana wamekuwa anauwezo wa kuvitengeneza lakini vitambulisho vya Taifa vimewashinda.
 
Wajasiriamali duniani kote ulindwa na sera bora sio kitambulisho!
Wanatakiwa pia wawe na Bima pamoja na micro pensheni. Wakizeeka nani atawatibia na kuwapa huduma zingine?
India, USA ni miongoni mwa nchi zenye hizi programs kwa streets Vendors wao. India mpaka mwendesha Mkokoteni ana bima na pensheni
 
Matumizi ya hivi vitambulisho vya wamachinga si sawa, vinatumika vibaya kwani kuna wafanyabiashara wenye mtaji mkubwazaidi ya 20m wanavitumia.
Kinachohitajika ni sera na sheria nzuri ziwekwe ili kuwalinda na kuwainua hao wamachinga.

Hivi vitambulisho ni mradi wawatu fulani ndiyo maana wamekuwa anauwezo wa kuvitengeneza lakini vitambulisho vya Taifa vimewashinda.
Hivi Leo mama anataka kuuza majimbi yake lazima awe na kitambulisho? Siungi mkono kitambulisho
 
Tatizo kubwa la hawa vijana wa Lumumba huwa wana soma kichwa cha habari tuu. Wasamehe maana ndio mwisho wa uelewa wao.
Ukiwauliza hizo 20,000/ zina kwenda wapi hakuna mwenye jibu. Ukiwauliza zina fanyia nini hakuna atakae kujibu. Yaani ni tatizo sana kujadiliana na slow learners..
Kile kitambulisho ukikiangalia kwa nyuma kimeandikwa 'Kwa matumizi ya TRA'. Fedha zinazotokana na vitambulisho zinaingizwa kwenye akaunti za TRA kwa mfumo wa Control number ambazo zinatolewa na TRA.

Kwa maelezo hayo kama unajua matumizi ya fedha nyingine zinazokusanywa na TRA basi utakuwa umejua na ya zitokanazo na vitambulisho
 
Wewe sio mfanyabiashara hujui adha ya hivi vitambulisho. Kwanza tunakosea sana kuviita vitambulusho. Hii ni kodi ya 20,000 ya kila mwaka kwa mfanyabiashara mdogo.

Kitambulisho ni kama risiti tu kuwa umelipa 20,000. Kibaya zaidi hii pesa inaenda moja kwa moja kwenye office ya Rais na haiwi audited. Tungekuwa na bunge imara uhalali wa hii pesa kwenda office ya Rais ingehojiwa.
 
Term kitambulisho inawatoa akili mno.

Wewe uliwahi kuwaza kuwa wamachinga watachangia pato la Taifa lao?...

Kumbe mnajua bado tunakopa kwa mabeberu? Si tunaambiwa tunajiendesha kwa kodi zetu? na hii ya kitambulisho ni kukurupuka kwa mtukufu anavyopenda breaking news, wazo la TRA wala halikuwa hivyo yeye na masifa yake na kurukia mambo ili aonekane ni wazo lake.

Hata Leo nenda TRA ukadiriwe mtaji wa milioni 3 uone kama hujatakiwa kulipa zaidi ya laki mbili kwa mwaka, lakini Leo hii tunaona vibanda vingapi barabaran vina bidhaa zaid ya hiyo milion 3 na vinatumia vitambulisho? Je ni kiasi gani serikali inapoteza mapato?

Awamu hii Tumekuwa na vibanda bar vina friji, mziki na viti kwenye service roads kisa vitambulisho vya machinga, kama unabisha nenda Dar Mwenge stendi ya daladala za bunju tegeta pale ujionee. Acheni kutetea maujinga kwa vijisent vidogo mnavyopewa huko.....huu sio ushabiki wa simba na yanga.haya ni maisha ya binadam wenzenu.laana itawauwa.
 
Vitambulisho vya machinga ni biashara ya Ikulu na hii lazima lisitishwe! Hatuwezi kuwa na kiongozi asiefata taratibu za nchi, We uliona wapi watu wakifanya biashara barabarani? Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya soko tameisha? Tusitetee Ujinga ambao hauna mantiki yoyote.Je sheria zinasemaje kuhusu machinga?
 
Back
Top Bottom