Uchaguzi 2020 Lissu asema atafuta vitambulisho vya machinga kwasababu elfu ishirini wanayotozwa ni wizi mtupu, haijulikani inaenda wapi

Rebeka 1

Member
Aug 11, 2020
34
37
LISSU ATANGAZA VITA DHIDI YA WAMACHINGA TANZANIA. ASEMA, WAMEKUA KERO KWA WAFANYA BIASHARA WA KIGENI.

(kutoka Tunduma Mbeya)

Anayetarajiwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CHADEMA ndugu Tundu A Lissu ameweka wazi msimamo wake juu ya Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga. Machinga ni wale wote wanaofanya biashara ndogondogo wakiwa ni vijana, akinamama na wazee wachache.

Wengi wao mitaji yao inaanzia shilingi elfu moja hadi laki moja. Machinga wamekua wakifanya biashara kwa kuzunguka kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wengine hutembea kwa umbali wa kilometa hadi 30 kwa mguu wakiwa na bidhaa zao mgongoni ama kichwani, bidhaa hizo nikama mayai, sindano za kushonea nguo pamoja na vitambaa vya kufutia jasho nk.

Wafanya biashara hawa wamekuwa wakiteseka sana kwa kuugua na jua na wakati mwingine kunyeshewa na mvua. Mtakumbuka wafanya biashara hawa ni wale walioteseka sana kwa miaka ya nyuma kama kupigwa na migambo kunyang'anywa vitu vyao na kumwagiwa kabisa vitu vyao. Wamachinga waliwahi kuingia mgogoro na Serikali baada ya baadhi ya viongozi kuwapangia kufanya biashara katika maeneo yasiyo na mzunguko au mkusanyiko wa watu.

Tangu Mwaka 2015, Rais magufuli aliamua kutangaza kuwahurumia na kuwapa uhuru wa kufanya biashara mahala popote wanapotaka hata kama ni viunga vya Ofisi zote za umma kama vile kwa Mkuu wa mkoa au Wilaya bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Rais Magufuli alitangaza kiama kwa yeyote atakaye wasumbua na kuwanyanyasa machinga.

Rais Magufuli aliongeza jukwaa la waliosamehewa kuwa ni kuanzia mwenye mtaji wa Milioni nne kushuka chini. Hali hii ilipeleka kuongezeka kwa watu waliopata msaada wa kufutiwa ushuru chonganishi na ushuru bugdha. Hivyo kwanzia Bodaboda,wauza vinjwaji, mama ntilie na machinga wote kiujumla walipewa uhuru wa kufanyabiashara zao. Rais Magufuli alitangaza kuwa ameamua kuwasamehe na kuwalinda Machinga kwasababu ndiyo waliompigia kura.

Rais aliamua kuagiza halmashauri zote kuhakikisha wanatoa ile asilimia kumi ya mapato na kuielekeza kwa Vijana, akina mama na walemavu kama sheria inavyotaka na Kiongozi ambaye katika eneo lake angeshindwa basi yeye angemtimua kazi. Wote hao ni Machinga.

Rais Magufuli aliamua kuanzisha vitambulisho vya machinga tena kwa gharama za Serikali ili Machinga Watambulike Rasmi na wao kutambuana ili wasisingiziwe kwamba wao ni wazururaji wasio na kazi kama ilivyofanyika hapo awali. Leo Machinga wamekuwa na thamani kubwa na kuwa wenye tija kwa taifa. Wamekuza biashara na kuongeza soko la ajira na viwanda nchini.

Leo machinga wanaheshimika na kutoonekana vibaka kama hapo awali bali watuwenye mchango mkubwa katika jamii. Leo machinga wamekua na vikundi vyao rasmi ambavyo wanavitumia kusaidiana katika shida na raha kwenye masuala ya kiuchumi na kitamaduni.

Msimamo wa Tundu Lissu na CHADEMA juu ya Machinga Tanzania. Lissu Ametangaza kiama kwa wamachinga katika siku 100 za mwanzo endapo atakua amepata Urais. Lissu ameenda mbali zaidi kwa kusema akiingia madarakani atafuta vitambulisho vya machinga na hakutakua tena na urasmi wa machinga. Hii ni kwamba taifa litarudi tena kwenye mgogoro na Machinga kama hapo awali.

Machinga wengi watapoteza ajira zao na mitaji. Kwakua hakutakua na kutambulika tena Machinga wataitwa wazururaji, vibaka na wasio na kazi hapo awali. Lissu anawaona Machinga kama tatizo kwasababu hawaungi mkono harakati zake.

Kutangazwa kwa vita ya Lissu dhidi ya Wamachinga kumefanywa na Lissu mwenyewe kwa kushawishiwa na baadhi ya wafanyabiashara wakigeni Waliompakani Tunduma. Mbele ya Wafanyabiashara wakubwa wa kigeni mpakani Tunduma amaboa waliahidi kumsaidia katika harakati za kupata urais Lissu kwashart la kuondoa urasmi wa Machinga kwani wamekuwa kero kwa wafanya biashara hao, Lissu aliwaahidi kuwa atafuta vitambulisho ili Umachinga usiwe rasmi nchini.

Na alipokenda kwenye mkutano wa hadhara alitangaza kufuta vitambulisho hivyo.Hali hii imezua hofu kwa Wamachinga mwenyeji kuona kwamba siku zao zinahesabika. Wamachinga wanaona kuwa watakuwa na wakati mgumu sana endapo Lissu atakuwa Rais kwani watakimbizwa na kupigwa na migambo kama hapo awali na kupoteza biashara zao ukizingatia wengi wanalea na kusaidia familia zao kupitia biashara hizo.

Wako;
Philipo Mwakibinga
(Tunduma Mbeya)

=======

 
Wacha kupotosha. Lissu amesema atafuta vitambulisho vya machinga kwasababu hiyo elfu ishirini wanayotozwa ni wizi mtupu, haijulikani inaenda wapi.

Kama mtakumbuka vizuri hivyo vitambulisho siku vinatolewa kwa mara ya kwanza vilitolewa ikulu, hii ni sawa na kusema hivyo vitambulisho vya machinga ni biashara ya ikulu, hiki kitu ndio Lissu hataki kukisikia kabisa, Lissu yupo kwa ajili ya wanyonge wa nchi hii.
 
Sasa ivi kuna urasmi wa machinga ndio maana wamebambikiziwa kulipa elfu ishirini kama kodi, huo urasmi ukiondolewa utawasaidia machinga kufanya biashara zao kwa Uhuru ili kukuza mitaji yao bila kukimbizana na mgambo wa almashauri wanaowalazimisha kulipa elfu ishirini bila kuzingatia uwezo wao.
 
Hawa machingaz na bodaboda wanatakiwa wajiongeze, vitambulisho vikifutwa inamaana nao hawako rasmi kisheria wajiandae kuburuzwa kama wakimbizi katika nchi yao.

Katika watu wanaotakiwa wamuogope Lissu kama ukoma ni machingaz na bodaboda Wakimshadadia Lissu anaweza akawaweka katika wakati mgumu sana baada ya uchaguzi huu kwisha na pengine atakuwa kajirudia zake Ubeligiji huku akiwacha machingaz katika kilio na kusaga meno.
 
Bila kujua hivi vitendo vya kutoa propaganda za kijinga ndivyo vinawafanya watu waone CCM mbaya. Kwa nini mnataka kuwafanya machinga na wenye boda ni vijana wajinga wakati wana masikio na wamemsikia Lissu kasema nini?

Machingaz na bodaboda wanahitaji kusaidiwa wajielewe. Hizi wiki kama mbili hivi wameonekana hawajielewi wanataka nini ingawa si wajinga. Wameonesha ni watu wa kufuata mkumbo na kupekekwa pelekwa tu. Hivyo ni muhimu kama Watanzania wenzetu kuwasaidia wajielewe na wasitumiwe au kutumika.
 
Tangu Mwaka 2015, Rais magufuli aliamua kutangaza kuwahurumia na kuwapa uhuru wa kufanya biashara mahala popote wanapotaka hata kama ni viunga vya Ofisi zote za umma kama vile kwa Mkuu wa mkoa au Wilaya bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Rais Magufuli alitangaza kiama kwa yeyote atakaye wasumbua na kuwanyanyasa machinga.
Mtu mwenye mtaji wa buku hadi laki moja akaambiwa alipe kitambulisho cha 20,000 kwakua anahurumiwa
 
Wacha kupotosha. Lissu amesema atafuta vitambulisho vya machinga kwasababu hiyo elfu ishirini wanayotozwa ni wizi mtupu, haijulikani inaenda wapi.

Kama utakumbuka vizuri hivyo vitambulisho siku vinatolewa kwa mara ya kwanza vilitolewa ikulu, hii ni sawa na kusema hivyo vitambulisho vya machinga ni biashara ya ikulu, hiki kitu ndio Lissu hataki kukisikia kabisa, Lissu yupo kwa ajili ya wanyonge wa nchi hii.
Ni machinga mjinga tuu ndo atakayeona kuwa elfuishirini wanayotozwa ni wizi mtupu.lisu anawezaje kusema kuwa hajui hizo hela zinaenda wapi wakati hakuna mtanzania ambaye hajui kuhusu ujenzi wa miundo mbinu inayojengwa kwa spidi na JPM!? Punguzeni mahaba na ushabiki ushabiki wa vyama sio ushabiki wa mpira.
 
Tangu Mwaka 2015, Rais magufuli aliamua kutangaza kuwahurumia na kuwapa uhuru wa kufanya biashara mahala popote wanapotaka hata kama ni viunga vya Ofisi zote za umma kama vile kwa Mkuu wa mkoa au Wilaya bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Rais Magufuli alitangaza kiama kwa yeyote atakaye wasumbua na kuwanyanyasa machinga.
Mkuu sio huruma, ila lengo ilikuwa ni kukusanya elfu ishirini za machinga, na wakuu wa mikoa walioshindwa kufikia lengo walitumbuliwa. Muulize Amos Makalla
 
Machingaz na bodaboda wanahitaji kusaidiwa wajielewe. Hizi wiki kama mbili hivi wameonekana hawajielewi wanataka nini ingawa si wajinga. Wameonesha ni watu wa kufuata mkumbo na kupekekwa pelekwa tu. Hivyo ni muhimu kama Watanzania wenzetu kuwasaidia wajielewe na wasitumiwe au kutumika.
jibuni hoja nyie wa Lumumba. Kama hamuwezi kumjibu tulieni hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom