Hili la Comoro Kutoka Suluhu na Misri

Comoro wameshaanza kutuacha wameifunga Togo na kudraw na misri wakati walikuwa ni vibonde si tutaendelea kupiga mdo wakati wenzetu wanafanya kweli
 
Nakumbuka miaka michache nyuma ilikuja timu ya Comoro hapa ikabezwa sana na tukaelezwa ile nchi haina hata Ligi..
Sasa nimesikia inchi hii imecheza na misri jana na kutoka Sare
Haya ni maajabu,Nini siri ya hawa wangazija?
Misri hawako vizuri msimu huu wiki iliyopita alisare na kenya
 
Nakumbuka miaka michache nyuma ilikuja timu ya Comoro hapa ikabezwa sana na tukaelezwa ile nchi haina hata Ligi..
Sasa nimesikia inchi hii imecheza na misri jana na kutoka Sare
Haya ni maajabu,Nini siri ya hawa wangazija?
Asee Comoro imepaa kwa haraka sana
 
Zamani Misri pamoja na kua na wachezaji wazuri Rais wa CAF aliepita alikua anawabeba sn. Huyu Rais wa sasa amejitahidi kukomesha huo mchezo mchafu. Ndio maana siku hizi kushinda ugenini imekua kawaida sehemu yoyote Africa
Soka sio karata mzee utasema ufiche, soka linapigwa hadharani kila mtu anaona
 
Nakumbuka miaka michache nyuma ilikuja timu ya Comoro hapa ikabezwa sana na tukaelezwa ile nchi haina hata Ligi..
Sasa nimesikia inchi hii imecheza na misri jana na kutoka Sare
Haya ni maajabu,Nini siri ya hawa wangazija?
Kiwango cha soka kinazidi kushuka duniani kila siku mpira unaochezwa leo sio ule wa miaka ile.

Fifa wamechangia kuharibu mpira kwa kuacha fedha iitawale mchezo. Wachezaji wanachezea maslahi tu na miaka kumi ijayo kombe la dunia litakosa mvuto kabisa.
 
Comoro sasa wamejipanga vizuri vijana wao sasa wamekuwa na kupevuka na sasa comoro inakwenda kucheza Michuano ya Afrika, Tanzania daah blaah blaah za Siasa katika michezo ndio zitatumaliza.
Hongereni Jirani Comoro tumejifunza kutoka kwenu!!!
 
Back
Top Bottom